Kuzuia mchanga wa dhahabu, Magufuli anastahili pongezi. Tusiishie kwenye madini tu, na gesi je?

Kuzuia mchanga wa dhahabu, Magufuli anastahili pongezi. Tusiishie kwenye madini tu, na gesi je?

Wakuu hali sio nzuri kwa upande wa wawekezaji na wafanyakazi wa acacia kuna baadhi ya contractor washasitishiwa mikataba na pia kama hii hali haitakua resolved mapema basi kuna wafanya kazi watakosa ajira kabisa hili swala raisi angetumia busara sana warudi kwenye mikataba wafanye review. Kuna watu wanapewa likizo zisizo na malipo mpaka mambo yatavyokuwa poa sasa shangilieni afu ikifikia mahali tukianza kudaiwa tutaanza kutaftana
 
Mtoa mada,je umethibitishaje kama mule ndani ya makontena kuna mchanga kweli?? je kama unadanganywa?? Jiulize hayo makontena yana muda gan pale bandarini?? hao walioyapokea hawakuthibitisha mule ndani kuna nini?? ina maana waliyapokea na walithibitisha kuwa mule ndani kuna mali salama na siyi mchanga, watanzania tusiwe mashabiki kwa tusichokifahamu,maigizo hayafai,tuthibitishe kwanza ndipo tusifie tusiuziwe mbuzi kwenye gunia tunaambiwa mchanga kumbe hakuna kitu,mbona kontena la magari walifungua,hayo makontena ya mchanga mbona hayajafunguliwa tukaonyeshwa kama kawaida yao.

Mmiliki wa hayo makontena mbona hajatajwa kama kweli kuna mchanga?? Ni mgodi gan unamiliki hayo makontena?? Mazingaombwe hayafai jamani,tusimame katika uhalisia na ukweli tu tusijaribu kuzigilibu akili za watanzania kutuaminisha kuwa hiki ni kipande cha almasi kumbe ni kipande cha chupa,watanzania wa sasa siyo mazuzu wotte ni waelewa tu.
 
Lengo ni zuri tatizo ni ukurupukaji. Hili zoezi lilihitaji majadiliano baina ya pande 2. Ikumbukwe hii si mara ya kwanza kwa zuio hili chini ya JPM. Mara ya kwanza lilifeli.

Kuchenjua madini kunahitaji uwekezaji mkubwa wa mitambo. Hivyo wawekezaji walipaswa kupewa muda mf miezi6 au mwaka kwa makubaliano ya pande zote 2. Huku kukurupuka ni sawa na zoezi la Viroba. Hakuna muda wa mpito kwa Mwekezaji.

Naskia migodi imesitisha mikataba na kampuni zote, wafanya kazi wote wamesimamishwa kazi, mafunzo yote yamesitishwa, nk. Kodi tunapoteza, ajira kwa watu wetu zinapotea, biashara za jirani zina athirika, nk.
Ukiagundua Mwanao wa kike anaviziwa na mwathirika wa HIV unamwacha tu waendelee kwa vile huyo mwathirika ni tajiri na atakupa pesa nzuri ya mahari?!

Hebu msiwe wajinga
 
Mifano ya kijinga karne ya 21
Kama mapato yanayopotea tuseme ni 30%(mfano), unadhani mishahara ya wafanyakazi unaojaribu kuwaonea huruma inafikia asilimia hata tano ya pato hilo? Tunahitaji watu wanaoweza kufikiri kwa akili.
 
Pamoja na nia nzuri ya rais wetu, lakini tukubali tukatae Tanzania hatuna uwezo huo rais Magufuli aliodhania tunao, kati ya wazalishaji wakubwa wa Dhahabu duniani, Tanzania ni nchi ya 15. Kati ya nchi hizo 15, ni nchi 4 tuu za mwanzo ndizo zenye smelter zanye uwezo huo, hivyo kama nchi za Ghana na África Kusini zilizoko kwenye 10 bora hazijawa na uwezo huo, what are the chances ya Tanzania kujenga uwezo huo?. Mambo mengine jameni sio tunashangilia tuu kisha baadae tunakuja kurudi kule kule! .


Mkuu Pascal Mayalla . Muda mwingine tutumie akili. Mwizi ajijengee uwezo wa kukuonyesha anaibaje?.
Suala siyo uwezo bali nia hakuna maana kupitia mpango huo wa kusafirisha mali ghali ulaya ndiyo dili zenyewe.
Nadhani hatua ya Raisi ni nzuri hata kama tunapoteza trilioni za Dola.Lakini kuzuia Mchanga bila njia mbdala nayo si uamuzi sahihi.
 
Kama mapato yanayopotea tuseme ni 30%(mfano), unadhani mishahara ya wafanyakazi unaojaribu kuwaonea huruma inafikia asilimia hata tano ya pato hilo? Tunahitaji watu wanaoweza kufikiri kwa akili.
Tatizo washauri wa Rais wa sasa ni dizaini kama zako. Wakurupukaji.

Hakuna anaepinga zoezi ila taratibu na majadiliano vilipaswa kufuatwa.

Kinu cha kuchakata na kuchenjua dhahabu gharama zake ni Us $ 800m. Na minimum yrs to instal ni 5yrs.

Ushabiki wa vitu vya ajabu haupashwi.
Je una fahamu Capita Gains tax ACACIA ina lipa ni shs ngapi? Coz kulikuwa na majadiliano ya mgodi kuuzwa kwa US $ 4.4 billion.
Je unafahanu Loyalty ya ACACIA ni shs ngapi,
Je unafahamu Corporation Tax ya ACACIA ni shs ngapi?
Je una fahamu PAYE ya wafanyakazi ni shs ngapi?

Je unafahamu kuwa ACACIA kwa sasa imesitisha uzalishaji ni hasara kiasi gani kwa Taifa?

Je unafahamu mikataba ACACIA imesaini na serikali na hasara ya kuzikiuka/kuzivunja?
 
Umetaja nchi zenye smelters hata ulaya hamna ukataja china,urusi,japan na ukasema afrika hamna nchi yenye smelter.

Hili ndo naomba ulifanyie utafiti boss maana nyie waandsh tunawategemea sana.
Afrika hakuna ndio maana tunapeleka Japan
P.
 
Tatizo washauri wa Rais wa sasa ni dizaini kama zako. Wakurupukaji.

Hakuna anaepinga zoezi ila taratibu na majadiliano vilipaswa kufuatwa.

Kinu cha kuchakata na kuchenjua dhahabu gharama zake ni Us $ 800m. Na minimum yrs to instal ni 5yrs.

Ushabiki wa vitu vya ajabu haupashwi.
Je una fahamu Capita Gains tax ACACIA ina lipa ni shs ngapi? Coz kulikuwa na majadiliano ya mgodi kuuzwa kwa US $ 4.4 billion.
Je unafahanu Loyalty ya ACACIA ni shs ngapi,
Je unafahamu Corporation Tax ya ACACIA ni shs ngapi?
Je una fahamu PAYE ya wafanyakazi ni shs ngapi?

Je unafahamu kuwa ACACIA kwa sasa imesitisha uzalishaji ni hasara kiasi gani kwa Taifa?

Je unafahamu mikataba ACACIA imesaini na serikali na hasara ya kuzikiuka/kuzivunja?
Hawawezi kukuelewa mkuu na kuna tetesi mchina ndo anavizia sasa ndo hujuma zitakuja hata zaidi ya hawa wazungu
 
Wanabodi
Hatua ya rais Magufuli kuzuia kusafirishwa kwa kinachoitwa mchanga wa dhahabu kupelekwa nje ya nchi kwa lengo la kulinda rasilimali za taifa, kitendo cha kishujaa cha hali ya juu sana kinachostahili pongezi za dhati kwa sababu kiukweli Tanzania lilikuwa ni shamba la bibi, tumekuwa tunaibiwa sana mchana kweupe kwa sababu hiki kinachoitwa mchanga wa dhahabu, kiukweli sio mchanga wa dhahabu bali ni makinikia ya dhahabu, ni gold concentrate yenye shaba na fedha, uwezo wa kutenganisha dhahabu, shaba na fedha, sio Tanzania hatuna, bara zima la África hatuna wala ulaya hawana. Wenye smelter ya uwezo huo ni Japan na China na Urusi ambao wanatumia umeme wa nuclear reactor.

Miongoni mwa vitu vizuri rais Magufuli alivyovitaja ni kujiapiza kuwa mchanga huo hautoki, hata kama tunashindwa kuusafisha mchanga huo, then ikibidi hata hiyo migodi ifungwe na ifungwe mpaka Tanzania tupate uwezo wa kuuyeyusha huo mchanga.

Huu ni uzalendo wa hali ya juu sana. Mwingine aliyefanya hivi ni Mwalimu Nyerere, alizuia kuchimbwa madini mpaka tupate uwezo, bahati mbaya alipoondoka na kuingia Mwinyi, akatoa rukhsa kuchimbwa kwa dhahabu yetu na kiukweli tumeishia kuibiwa kwa kupata peanut na wenye migodi wakikomba faida yote.

Pamoja na nia nzuri ya rais wetu, lakini tukubali tukatae Tanzania hatuna uwezo huo rais Magufuli aliodhania tunao, kati ya wazalishaji wakubwa wa Dhahabu duniani, Tanzania ni nchi ya 15. Kati ya nchi hizo 15, ni nchi 4 tuu za mwanzo ndizo zenye smelter zanye uwezo huo, hivyo kama nchi za Ghana na África Kusini zilizoko kwenye 10 bora hazijawa na uwezo huo, what are the chances ya Tanzania kujenga uwezo huo?. Mambo mengine jameni sio tunashangilia tuu kisha baadae tunakuja kurudi kule kule! .

Kuna vitu kuvifanya kunahitaji tuu nía ya dhati, na kuna vitu kuvifanya kunahitaji uwezo. Wachumi wa sekta ya madini tusaidieni, kwa umeme huu, na gold kiduchu hii kwa hizo smelter za uwezo huo jee Tanzania tunaweza? . Kama mikataba ya migodi hiyo huo ndio uliokuwa utaratibu wao, maamuzi kama haya yanamaana gani kwenye investment climate yetu? .

Kwa vile rais wetu ameonyesha nia kulinda rasilimali zetu, Tanzania tusiendelee kufanywa shamba la bibi, nashauri tusiishie kwenye mchanga tuu wa dhahabu, kwanini tusiende na kwenye gesi maana nako tunaibiwa!.
http://www.jamiiforums.com/threads/...anzania-tunaibiwa-mchana-kweupe.298561/page-3
Hakuna hata kitalu kimoja cha gesi kinachomilikiwa na Watanzania, kwa sababu hatuna uwezo wa kumiliki hata kitalu kimoja tuu!, sasa kama tumeshindwa hata kuchangishana mifuko yote ya hifadhi za jamii na mabenki yote kumiliki angalau kitalu kimoja tuu, what are the chances ya kumiliki gold smelter la nuclear power reactor?!.

Niliwahi kushauri
https://www.jamiiforums.com/threads...ye-uchumi-we-have-to-choose-or.1189637/page-3

Ili hizi zisije kuwa ni siasa tuu, Tanzania tunahitaji uniform standard formula na rules za kulinda rasilimali zetu zote kwa manufaa ya Watanzania na sio double standards kwa kuzuia tuu mchanga wa dhahabu huku gesi tunaibiwa, Tanzanite tunaibiwa, kwenye vitalu vya uwindaji, light aircrafts zinatua na kupaa huku no body cares zinabeba nini huku tembo wetu wakizidi kuyeyuka!.
To hell with mikataba ya kinyonyaji, to hell with wawekezaji majambazi wanaotuibia kwa kisingizio cha umasikini wetu, to hell with FDI dependence kwenye uwekezaji, tujenge uwezo kwa Watanzania kuijenga nchi yetu, kwa kutumia mitaji na rasilimali zetu za ndani kumiliki uchumi wetu, swali linabaki ni moja tuu "kwa kutumia nini from where and how? .

Paskali
Kama hujawahi kufanya kazi migodini, hii ishu ya mchanga huwezi ukaielezea kwa mapana yake...
 
Magufuli kuzuia mchanga wa DHAHABU sio swala la kupongeza bila kuangalia madhara yake madhara yake ni kushitakiwa Serikali na kuingiza hasara ya kulipa fidia kwa kodi zetu wtz hivi Serikali inalipwa mrahaba kwnn mwekezaji akitaka kupeleka kwake umzuie? Wanapotoa DHAHABU %20 hadi25 DHAHABU inabaki nabidi wakatolee watakotaka wao na eneo hilo la kutolea ni km tatu au NNE tu dunia nzima wanadai kila siku kiasi cha Us dollars 1 million zinapote how comes? Tusubilie tuone kifuatacho rais hashauriwi au kuomba maelekezo hili ni swala la kusubili hili sio swala la kopongeza Bali tufarijiane ni shida!
 
Nadhani walioruhusu mchanga kuondokana wangali HAI na mmoja wao ni Mh Benjamin Mkapa. Hebu asijifanye yeye ni "Alfa na Omega"

Na kama ana NIA ya DHATI ya kuuzuia mchanga basi asitumie mabavu. Dunia ya Leo ni ya watu wenye maarifa na weledi, "misuli" haina nafasi. Achukue ushauri wa Mh Tundu Lissu.
Mtu unaibiwa...alafu wajinga wanasema usitumie mabavu kuzuia wahalifu...zimo kweli wewe au wenyewe wamekushikia?
 
It's so sad, hizi papara na maamuzi ya kukurupuka is not very good at all kwenye investment climate.

Tuliwahi kushauri humu
https://www.jamiiforums.com/threads...ye-uchumi-we-have-to-choose-or.1189637/page-3

Ukifanya jambo kwa papara with a negative preconceived ideas, then atakapokuja kuambiwa ukweli kuwa Tanzania hatuna umeme wa kuendesha hizo smelter za ku separate gold, silver and copper, sura itamshuka!.

Watu wana mikataba ya uwekezaji, sheria, taratibu na kanuni zipo, papara za nini? .

Paskali
Kama hatuna smelters ndo justification ya kutuibia au kuto declare kilichomo ndani?
 
Back
Top Bottom