Kuzuia mchanga wa dhahabu, Magufuli anastahili pongezi. Tusiishie kwenye madini tu, na gesi je?

Wakuu hali sio nzuri kwa upande wa wawekezaji na wafanyakazi wa acacia kuna baadhi ya contractor washasitishiwa mikataba na pia kama hii hali haitakua resolved mapema basi kuna wafanya kazi watakosa ajira kabisa hili swala raisi angetumia busara sana warudi kwenye mikataba wafanye review. Kuna watu wanapewa likizo zisizo na malipo mpaka mambo yatavyokuwa poa sasa shangilieni afu ikifikia mahali tukianza kudaiwa tutaanza kutaftana
 
Mtoa mada,je umethibitishaje kama mule ndani ya makontena kuna mchanga kweli?? je kama unadanganywa?? Jiulize hayo makontena yana muda gan pale bandarini?? hao walioyapokea hawakuthibitisha mule ndani kuna nini?? ina maana waliyapokea na walithibitisha kuwa mule ndani kuna mali salama na siyi mchanga, watanzania tusiwe mashabiki kwa tusichokifahamu,maigizo hayafai,tuthibitishe kwanza ndipo tusifie tusiuziwe mbuzi kwenye gunia tunaambiwa mchanga kumbe hakuna kitu,mbona kontena la magari walifungua,hayo makontena ya mchanga mbona hayajafunguliwa tukaonyeshwa kama kawaida yao.

Mmiliki wa hayo makontena mbona hajatajwa kama kweli kuna mchanga?? Ni mgodi gan unamiliki hayo makontena?? Mazingaombwe hayafai jamani,tusimame katika uhalisia na ukweli tu tusijaribu kuzigilibu akili za watanzania kutuaminisha kuwa hiki ni kipande cha almasi kumbe ni kipande cha chupa,watanzania wa sasa siyo mazuzu wotte ni waelewa tu.
 
Ukiagundua Mwanao wa kike anaviziwa na mwathirika wa HIV unamwacha tu waendelee kwa vile huyo mwathirika ni tajiri na atakupa pesa nzuri ya mahari?!

Hebu msiwe wajinga
 
Mifano ya kijinga karne ya 21
Kama mapato yanayopotea tuseme ni 30%(mfano), unadhani mishahara ya wafanyakazi unaojaribu kuwaonea huruma inafikia asilimia hata tano ya pato hilo? Tunahitaji watu wanaoweza kufikiri kwa akili.
 


Mkuu Pascal Mayalla . Muda mwingine tutumie akili. Mwizi ajijengee uwezo wa kukuonyesha anaibaje?.
Suala siyo uwezo bali nia hakuna maana kupitia mpango huo wa kusafirisha mali ghali ulaya ndiyo dili zenyewe.
Nadhani hatua ya Raisi ni nzuri hata kama tunapoteza trilioni za Dola.Lakini kuzuia Mchanga bila njia mbdala nayo si uamuzi sahihi.
 
Kama mapato yanayopotea tuseme ni 30%(mfano), unadhani mishahara ya wafanyakazi unaojaribu kuwaonea huruma inafikia asilimia hata tano ya pato hilo? Tunahitaji watu wanaoweza kufikiri kwa akili.
Tatizo washauri wa Rais wa sasa ni dizaini kama zako. Wakurupukaji.

Hakuna anaepinga zoezi ila taratibu na majadiliano vilipaswa kufuatwa.

Kinu cha kuchakata na kuchenjua dhahabu gharama zake ni Us $ 800m. Na minimum yrs to instal ni 5yrs.

Ushabiki wa vitu vya ajabu haupashwi.
Je una fahamu Capita Gains tax ACACIA ina lipa ni shs ngapi? Coz kulikuwa na majadiliano ya mgodi kuuzwa kwa US $ 4.4 billion.
Je unafahanu Loyalty ya ACACIA ni shs ngapi,
Je unafahamu Corporation Tax ya ACACIA ni shs ngapi?
Je una fahamu PAYE ya wafanyakazi ni shs ngapi?

Je unafahamu kuwa ACACIA kwa sasa imesitisha uzalishaji ni hasara kiasi gani kwa Taifa?

Je unafahamu mikataba ACACIA imesaini na serikali na hasara ya kuzikiuka/kuzivunja?
 
Umetaja nchi zenye smelters hata ulaya hamna ukataja china,urusi,japan na ukasema afrika hamna nchi yenye smelter.

Hili ndo naomba ulifanyie utafiti boss maana nyie waandsh tunawategemea sana.
Afrika hakuna ndio maana tunapeleka Japan
P.
 
Hawawezi kukuelewa mkuu na kuna tetesi mchina ndo anavizia sasa ndo hujuma zitakuja hata zaidi ya hawa wazungu
 
Kama hujawahi kufanya kazi migodini, hii ishu ya mchanga huwezi ukaielezea kwa mapana yake...
 
Magufuli kuzuia mchanga wa DHAHABU sio swala la kupongeza bila kuangalia madhara yake madhara yake ni kushitakiwa Serikali na kuingiza hasara ya kulipa fidia kwa kodi zetu wtz hivi Serikali inalipwa mrahaba kwnn mwekezaji akitaka kupeleka kwake umzuie? Wanapotoa DHAHABU %20 hadi25 DHAHABU inabaki nabidi wakatolee watakotaka wao na eneo hilo la kutolea ni km tatu au NNE tu dunia nzima wanadai kila siku kiasi cha Us dollars 1 million zinapote how comes? Tusubilie tuone kifuatacho rais hashauriwi au kuomba maelekezo hili ni swala la kusubili hili sio swala la kopongeza Bali tufarijiane ni shida!
 
Mtu unaibiwa...alafu wajinga wanasema usitumie mabavu kuzuia wahalifu...zimo kweli wewe au wenyewe wamekushikia?
 
Kama hatuna smelters ndo justification ya kutuibia au kuto declare kilichomo ndani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…