Kuzuia mchanga wa dhahabu, Magufuli anastahili pongezi. Tusiishie kwenye madini tu, na gesi je?

KWANZA MPAKA SASA SIAMINI ETI TANZANIA TUNASHINDWA KUFANYA PROCESS HIYO HAPA...MBONA KUNA WATU TUNAWAJUA NA WALIKUWA WANACHUKUA MATOLEO YA KWENDA KUFANYA KAZI YA KUTENGANISHA DHAHABU,SHABA,FEDHA KUTOKA KWENYE MCHANGA,NA WAMEKUWA WAKIFANYA HAPAHAPA HYO KAZI

OVA
 
Unazungumzia mikutano ya hadhara ya kisiasa, sisi Watanzania tusio na vyama kwetu hata ruzuku ya vyama ni ufisadi, hivyo tumeshauri ifutwe
https://www.jamiiforums.com/threads...ie-mbali-ruzuku-hii-ni-ufisadi.1129220/page-3

Paskali
Paskal,

Naona umejirudi.
Tutumie akili na uelewa wetu kwa manufaa ya taifa. Sio hii miluzi ya kupuuz isiyo na tija.

Ni kweli ngoja wafungue tuone, yawezekana ni semi processed gold, wengine wanaita kibongobongo 'Carbon'

Ujue inauma kaka.
Ni bora kufunga tuwaachie wachimbaji wadogo wazawa wajiachie huu ni upuuz.
 

Wanalipaga Kodi hao??????
Acha tuwachenjie tu Mara kibao wanadai wamepata hasara na kuondoka hawaondoki

In short ni kwamba gharama ya kusafirisha Mchanga inaathiri faida, faida ikiathiriwa hata kama ni kwa makusudi wanajustify tusipewe chochote lakini pia inatoa mwanya wa kupigwa.

Nani anayeshehudia kinachoendekea Japan
 
unafiki huo , unazuia mchanga wakati huo huo
1. unajenga airport chato nje ya bajeti.
2. Unamlipa lipumba mshahara wakati hakuna kazi anayofanya
3. unamlipa bashite mshahara wakati anatumia vyeti vya kuazima
4. unametea bashite na kumlipa mshahara wakati ni jambazi wa kuvamia vituo vya TV na kuwatishia watu.

Hizi ndio akili za mgabe, kuwakomoa wazungu wakati mwenyewe unafanya madudu .
 
Hizi dola milioni 300 tunazopewa sio tunalambishwa asali, kisha turuhusu mchanga uendelee kusafirishwa, ama tunajenga smelter, tuuchenjue, tujue kilichomo, ndipo tupigiane mahesabu na mwizi wetu!.

Ila pia wajemeni, moja shika sii kumi nenda rudi, tupokee tuu hiki kidogo kilichotolewa, wakati tukiendelea kukifuatlia kikubwa. Rais Magufuli na Prof. Kabudi, tuwapongeze kwa hili japo ni kidogo, lakini ni something, na something is better than nothing!, tuwe na shukrani katika madogo, ili tujaaliwe makubwa!.

Paskali
 
Nafanya tuu rejea, usikute zile demokrasia na haki za binaadamu katika nyaraka zile ni bangusilo tuu, the real issue ya kumtikisa Magufuli ni hii ya vita vya kiuchumi.

Lets wait and see.

P,
 
Nafanya tuu rejea, usikute zile demokrasia na haki za binaadamu katika nyaraka zile ni bangusilo tuu, the real issue ya kumtikisa Magufuli ni hii ya vita vya kiuchumi.

Lets wait and see.

P,
Kaogeshe watoto mkuu kama umekosa kazi ya kufanya.
 
Nafanya tuu rejea, usikute zile demokrasia na haki za binaadamu katika nyaraka zile ni bangusilo tuu, the real issue ya kumtikisa Magufuli ni hii ya vita vya kiuchumi.

Lets wait and see.

P,
It is simple,atekeleze yale maazimio 14 aache la ushoga mambo yatakwenda sawa.Shida ni kuwaachia wapinzani hapo anaona kama crime
 
Wanabodi
Katika bandiko hili, kuna kitu nilikisema kuhusu huu mchanga wa dhahabu.

Mazungumzo yamemalizika rasmi na makubaliano yamefikiwa, hivyo subirini tutangaziwe rasmi kisha tukumbushane vizuri kuhusu viapo vya watu kujiapiza kwa nguvu kweli kweli, halafu, wakiishwa labishwa tuu asali...
Mchanga huo unaondoka.

Huu mchanga ukiondoka bila sisi kujua kilichomo, kiukweli kabisa sitashangaa kwa sababu naelewa the games people plays.

Tusubiri, tukumbushane.
P
 
Ahadi ya fedha hizi dola milioni 300 ilikuwa ni goodwill kuonyeshea nia njema ya kuzungumzia deni letu lote la dola bilioni 191.

Sasa mazungumzo yamemalizika wamefikia makubaliano ya mwisho, fedha hizo sasa ndio kifuta machozi chetu na kusamehe deni letu lote.

Kwa vile mimi sio authority, tusubiri taarifa rasmi.

P.
 
Wanabodi nimeiona draft agreement ya mazungumzo ya serikali na Barrick, hakuna lolote kuhusu kuchenjuliwa kwa mchanga!.

Tuliuzuia mchanga kwa sababu tulihisi tunaibiwa kwa kutokujua kilichomo. Tume mbili za rais ile ya Prof. Mruma na Prof. Osoro zikathibitisha ni kweli tunaibiwa. TRA wakapiga hesabu deni likaja dola billions 193.
Kwenye mazungumzo tumekubali kufuta deni hilo kwa kulipwa kufuta machozi cha dola million 300 ambazo zitalipwa ndani ya miaka 7.

Sherti la kwanza ni tukubali kulipwa down payment ya dola million 100 mchanga uondoke na zuio liondoewe.

Kama tuliuzuia mchanga usiondoke kwa sababu hatujui kilichomo ndio maana tunaibiwa, leo tunambiwa mchanga utaondoka bila sisi kujua kilichomo, then tuliuzuia wa nini?!.

Kina kitu nilikisema humu kuhusu mchanga huu na mambo ya kulambisha asali!.

Kama kwenye sakata la Acacia, the bone of contention ni ule mchanga, kwa sababu hatujui kilichomo, mgogoro huu utaishaje bila kujua kilichomo?.
Kiukweli kabisa mchanga ukiondoka sitashangaa tuu bali nitaamini nilicho kisema humu kuhusu mchanga ni kweli.
P
 
Pongezi za nini wewe kikaragosi!?😳

 
mkuu una maana kuna kitu uliandika ambacho wewe mweneyewe hukiamini lakini unataka sisi tukiamini? tutake radhi sisi tuliokujanjarusha mapemaaa!!!

walambishwe kina Ngeleja pekeyao!!!? aa wapi, "wanaume" wamekata kitu kidogo.

sisi tusiopambania uteuzi haturembirembi kama Pascal Mayalla
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…