Kwa aina ya ukamataji wa jeshi la polisi Tanzania, ni wazi wanakaribisha vitendo vya kiharifu nchini

mshale21

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2021
Posts
2,517
Reaction score
6,074
wakuu, kwa mtindo wa ukamataji wa jeshi la polisi, ni wazi kabisa wanakaribisha matendo ya kiharifu nchini, maana huwezi kuwa na uhakika kuwa huyu ni askali polisi kweli au kibaka.

Nadhani , ni wakati muafaka kwa jeshi la polisi kukaa na kujitasmini kama ukamataji wa watuhumiwa unafuata taratibu na madhara yake katika jamii, maana ni rahisi kwa kibaka kuingia kwa gia ya ukamataji wa polisi wetu, maana sio ukamataji tena , bali ni utekaji,

Wanakamata wakiwa hawana uniform wala vitambulisho, vile vile kwa tukio la April 24 ambalo Murilo alikana kuwakamata wananchi mbele ya mahakama, basi ni wazi kabisa kuna vibaka wanavaa nguo za jeshi la polisi na vitambulisho arafu wanashughulikia wananchi

Wito wangu, kama polisi hawataki kufuata taratibu za ukamataji, basi ni muhimu wananchi tukachukua tahadhari, tusiruhusu mtu kuchukuliwa na watu wasiojulikana , wasio na uniform au vitambulisho na wasioeleza wazi ni kwa nini wanakamata mtu, maana kuna mwanya unaotumika na vibaka kwa mgongo wa jeshi la polisi
 
1746381631152.png
 
Walifanyweje tra
Mkuu umewasahau wale jamaa walio enda kumblock ndugu mmoja maeneo ya kibo complex, jamaa akabiga mwano kuomba msaada akisema wasiojulikana wanamteka, then wananchi wakaingia mzigoni na mawe jamaa kujikwamua watembea na cruiser yao ila mmoja alijeruhiwa sana baadae alikata moto, umesahau au hukufatilia?
 
Polisi wakija kukukamata usibali kifala fala. Watakukamata watakupiga badae watasema sio wao hawahusiki.
Back in those days 2010, walinikuta maeneo ya maziwa mida ya jioni na tenga Lao wakaanza kunipiga eti niingie kwenye tenga twende central, na wamenikuta eneo nalofanyia biashara, hawajaniambia nina kosa gani , niliwaambia mtapeleka maiti central police na sio mimi nikiwa mzima zikaanza kuchapwa , soon raia wakajaza nzi wakapanda tenga Lao wakateleza, yaani ni uonevu mtupu
 
wakuu, kwa mtindo wa ukamataji wa jeshi la polisi, ni wazi kabisa wanakaribisha matendo ya kiharifu nchini, maana huwezi kuwa na uhakika kuwa huyu ni askali polisi kweli au kibaka.

Nadhani , ni wakati muafaka kwa jeshi la polisi kukaa na kujitasmini kama ukamataji wa watuhumiwa unafuata taratibu na madhara yake katika jamii, maana ni rahisi kwa kibaka kuingia kwa gia ya ukamataji wa polisi wetu, maana sio ukamataji tena , bali ni utekaji,

Wanakamata wakiwa hawana uniform wala vitambulisho, vile vile kwa tukio la April 24 ambalo Murilo alikana kuwakamata wananchi mbele ya mahakama, basi ni wazi kabisa kuna vibaka wanavaa nguo za jeshi la polisi na vitambulisho arafu wanashughulikia wananchi

Wito wangu, kama polisi hawataki kufuata taratibu za ukamataji, basi ni muhimu wananchi tukachukua tahadhari, tusiruhusu mtu kuchukuliwa na watu wasiojulikana , wasio na uniform au vitambulisho na wasioeleza wazi ni kwa nini wanakamata mtu, maana kuna mwanya unaotumika na vibaka kwa mgongo wa jeshi la polisi
Inasikitisha sana
 
Back in those days 2010, walinikuta maeneo ya maziwa mida ya jioni na tenga Lao wakaanza kunipiga eti niingie kwenye tenga twende central, na wamenikuta eneo nalofanyia biashara, hawajaniambia nina kosa gani , niliwaambia mtapeleka maiti central police na sio mimi nikiwa mzima zikaanza kuchapwa , soon raia wakajaza nzi wakapanda tenga Lao wakateleza, yaani ni uonevu mtupu
Safi sana
 
Back
Top Bottom