MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Huu uzi ningeshauandika kitambo ila wakati nataka kuandika ndo likatokea janga la moto huko Marekani. Wataalamu wameshaongea kuhusu sababu za moto na kutaja kuwa chanzo ni moto wa mwituni ulioenea kwenye makazi ya watu. Ni janga la asili. Wakati uchunguzi ukiendelea ndo wamejitokeza baadhi ya watu wenye imani za kishirikina kwa mwonekano wa dini zao na kuanza kuhusisha hilo janga na mambo ya kiimani. Kuna baadhi ya wakristo na waislamu wamedai ni adhabu ya Mungu kwa watu wa Los Angeles kwa dhambi wanazofanya. Hawa ni wa kupuuzwa.
Nikirudi kwenye mada kuu ya huu uzi ni kuwa kuna uwekezaji unafanywa nchini na nchi zingine za kiafrika ambao hauna faida yoyote kimaendeleo. Kwa sasa karibu kila kanisa utakaloenda kuabudu kuna mchango wa ujenzi wa kanisa. Waumini wanakamuliwa walicho nacho ili kujenga makanisa. MIMI SIUNGI MKONO HILI SUALA.
Nchi maskini zinahitaji mambo mengi sana ya kimaendeleo zaidi ya haya makanisa na misikiti. Utakuta mchezaji mkubwa wa kimataifa kapiga hela badala hata ya kufungua academy ya kukuza vipaji anaenda kujenga misikiti mitano. Kwangu mimi ni sawa na ujenzi wa magereza ya kifikra. Mtu aliyetekwa na imani yake ni kama yuko gerezani.
Nchi inahitaji viwanda, huduma bora za kiafya na kielimu, usafiri na mambo mengine muhimu. Tuachane na ujenzi wa haya makanisa na misikiti kwa muda. Tukiabudu hata chini ya mti Mungu anasikia.