Kwa ajili ya kumbukumbu: Magufuli hatojiongezea muda

Kina Kabula,Sundi ndo wanavaa CL na wanaendesha Audi 9.
Kuhusu kuongeza mhula. Tuombe uzima tu Wabunge wataongeza muda na Magufuli atajifanya kaombwa hivyo kakubali unless afe kabla ya 2025.
we dada una shida sana...hao watu umewataja wataeza kukuletea balaa kubwa sana..!
 
Nyani Ngabu na Paschal Mayalla wote ni wasukuma, na msukuma hata aishi New York hawezi acha ushamba na ujinga flani hivi wa kumsifia msukuma mwenzake hata akila kinyesi
Rudia kusoma tena post yako!
Inawezekana ukaanza kujiuliza kama ni wewe uliye post hii kitu.
 
They want to ride the gravy train for as long as they can?
Of course.

Nyerere alilisema hili katika hotuba yake moja.

Alisema kila alipotaka kujiuzulu, wapambe wakawa wanamwambia "Mwalimu nchi inakuhitaji sana, nchi inakuhitaji sana".

Akawa anaaahirisha miaka mitano.

Baada ya miaka mitano, akisema tena anataka kung'atuka, akawa anapewa habari zile zile.

Baadaye akaja kustuka, hapa kuna nchi kunihitaji au hawa watu wanapata faida mimi nikiwa rais na hawajui rais ajaye atakuja na watu gani?

Akaamua kujiuzulu.

Alilisema wazi hili katika moja ya hotuba zake.

Na hii si Tanzania tu.

Kuna uchaguzi mmoja wa Zimbabwe Mugabe alishindwa na Morgan Tsvangirai.

Mugabe akasema yupo tayari kukubali kushindwa. Kukubali matokeo.

Vyombo vyake vya usalama vikamwambia tulia mzee, hakubali matokeo mtu hapa.

Ukikubali matokeo ikaja serikali ya wapinzani hapa, tutafungwa wote kwa ushenzi tuliowafanyia.

Hii habari inajirudia Tanzania.

Mimi sioni kama Magufuli atataka kuongeza muda. Ingawa naye hatabiriki.

Amesema mara kadhaa kwamba hana nia hiyo. Na hilo ni jambo zuri.

Lakini wapambe wake ni kama hawataki kukubali hilo.
 
Body/silent language inaonyesha wazi kinachotakiwa kuwa. Ni mtoto mdogo tu anayeweza kudanganyika.
Kwani Mu-7 anakula bata gani pale uganda? mbona anang'an'ania pengine mpaka mauti yamkute kwenye kiti?
Watu wanaopenda kusujudiwa na kuishi kama wafalme ni matatizo makubwa sana katika jamii ya wastaarabu
 

Huu uzi utaukimbia baada ya muda. Kunajisiwa kwa uchaguzi huu ni maagizo yake, na lengo lake ni kupata wanaccm wengi watakaomuongezea muda wa kukaa madarakani. Anajidai hataki kuongezeka muda mbele ya camera, lakini off camera, yeye ndio streling wa kukaa madarakani zaidi ya 10yrs.
 
Wizi mkubwa wa kura aliousimamia katika uchaguzi huu ni maandalizi ya project yake ya kubaki madarakani kwa kisingizio cha kusimamia white elephants zake, alishadokeza hilo
 
Kama hataongeza muda basi atakua mfano wa kuigwa sababu kila kitu kipo ndani ya uwezo ni yeye tu aamue.Loop holes za kubadili katiba zipo nje nje.Let’s wait and see!
 
Kama mambo yataendelea kuwa kama yalivyo sasa kwa miaka mitano ijayo anaweza akaachia madaraka lakini kama yatajitokeza majanga makubwa ya kukwamisha miradi mikubwa aliyoianza story inaweza kubadilika kamanda anayepiganisha vita hawezi kutoka kwenye commanding post katikati ya mapigano

Sent from my SM-N910H using JamiiForums mobile app
 
1. Kama Jiwe anaona uraisi ni Mzigo kwa nini amegombea the second term?

2. Kama unadhani hawezi kuturudisha tulipotoka kwa nini anaturudisha tulipotoka in so many ways, repressive laws, moves za kuua upinzani, kuminya uhuru wa habari etc
Mkuu kwani si mlisema Membe ni kiboko ya jiwe?
 
Nyani Ngabu na Paschal Mayalla wote ni wasukuma, na msukuma hata aishi New York hawezi acha ushamba na ujinga flani hivi wa kumsifia msukuma mwenzake hata akila kinyesi
Bwashee humu hatutambuani kwa makabila yetu bali kwa hoja, Bwashee hoja kubwa hapa ya Nyani ngabu ni Magufuli kutojiongezea muda wake,Abusive lunguage for Sukuma Community is unacceptable comment.
 
Kama hataongeza muda basi atakua mfano wa kuigwa sababu kila kitu kipo ndani ya uwezo ni yeye tu aamue.Loop holes za kubadili katiba zipo nje nje.Let’s wait and see!
Mwinyi, Mkapa na Kikwete walishafanya.

Yeye anakuwaje mfano hapo?

Ukiniambia rais Mwinyi ameweka mfano wa kuheshimu term limits, nitakuelewa.

Maana ndiye alikuwa rais wa kwanza kufanya hivyo.

Sasa rais wa nne kufanya hivyo ameweka mfano kivipi wakati mfano tulishauona toka kwa Mwinyi?
 
Nyani Ngabu na Paschal Mayalla wote ni wasukuma, na msukuma hata aishi New York hawezi acha ushamba na ujinga flani hivi wa kumsifia msukuma mwenzake hata akila kinyesi
Umegonga penyewee!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…