Nadhani waTanzania tuna lawama nyingi zisizo za msingi. Serkali au vyombo vyako havipo kwa ajili ya kuingilia maamuzi ya kila mtu. Wewe una akili zako tena timamu, unawekeza laki moja na unapata elfu sabini kabla ya mwaka. Hii sabini ingekuwa kwa mwaka hiyo ingekuwa inerest ya 70% kwa mwaka. Hiyo inetrest haipo duniani. Kwa nini usitambue kuwa hizo pesa ulizopata ni chambo tu. Ukisha lainika na kupata uroho wa kupata pesa ambayo hukuifaniya kazi , wenzako wanatayarisha pigo kubwa.
Interest hizo kwa kifupi hazipo. Hivi unataka serkali ifanye nini? Ulipoenda kuwekeza ulipata ushauri toka serkali? Je, uliijulisha BOT unayotaka ikusaidie? Je, ulienda kwenye chombo chochote kuhusu uhalisia wa waliokupiga? Ulipoingia uliingia kimya kimya na ukaonjeshwa kafaida ili uweze kukusanya watu. Hivi vyote ulifanya kwa siri buila serkali kujuwa na sasa unataka ikusaidie.
Kuna watu wanasema eti wahusika wamesajiliwa. Ukweli ni kuwa BRELA haiwezi kukataa kusaili biashara kama wametimiza masharti. Lakini baada ya kusajiliwa, kazi ya BRELA imeisha. Sasa wanabaki na biashara yao na wanavyoiendesha na kuhakikisha wanalipa kodi. Hawa walisajili biashara ya kuuza bidhaa kimtandao. Je mliyotapeliwa mliwaomba kuonyeshwa wameidhinishwa kufanya bioashara gani? Labda mungefanya hivyo mngeona wanafanya kitu tofauti na walichosajiliwa kufanya. Kila mtu anatakiwa kujuwa kuwa hakuna biashara ya pesa inalipa interest ya 70%, 50%, n.k. Nilishaandika humu kama unataka interest nzuri nunu BOT bonds au weka fixed savings account, lakini hata hizo hazitoi interest kubwa kama hizi mnazodanganywa nazo.