Kwa alichokiongea Heri Mzozo, Tshabalala ataenda Yanga

Kwa alichokiongea Heri Mzozo, Tshabalala ataenda Yanga

Kulipwa milioni 1.5 hii inatokana na mkataba aliosaini au vp?
Lakini kwa pale simba nijuavyo mshahara huo kwa sasa labda anakula ally salim...
 
Huu mjadala ukiuangalia kwa makini umesababishwa na kukosa weledi kwa meneja wa Mohamed Husein. Tujiulize ni Mohamed Hussein peke yake ambaye anamaliza mkataba wake au kuna wachezaji wengine wapo wanaomaliza mikataba yao? Kwa nini kila chombo cha habari kiwe kinamzungumzia Mohamed Husein pekee? Hiyo haijatokea kwa bahati mbaya tu bali ni mkakati uliopangwa mahususi.

Kilicho wazi ni kuwa ni kweli Mohamed Husein anamaliza mkataba hivi karibuni. Na ni kweli kuwa kiwango ch a Mohamed Husein kimepanda sana kwa hii misimu mwili na hasa zaidi huu unaoishia. Ni kweli kuwa kuonekana kwenye ligi ya mabingwa Afrika sasa hivi Mohamed Husein anaweza akapata dili kwenye vilabu vikubwa kaskazini ya Afrika au Afrika ya Kusini. Lakini anachokifanya Henry Mzozo ni mambo ya mameneja wa kizamani kabisa. Kutafuta waandishi wa habari kuongea nao halafu waandishi wa habari wa redio na magazeti kuipeleka hewani habari za uongo na za kweli ili kumpandisha dau Mohamed Husein. Hayo mambo/mbinu za ovyo na ya kizamani kabisa na kama Mohamed Husein anataka maendeleo yake acheze kimataifa basi haraka sana atafute meneja mwingine. Alichotakiwa kufanya Henry Mzozo ni kuwatafuta watu wenye weledi ambao tayari wameshaenda kimataifa kama Jamal Kisongo amsaidie namna ya kumpaisha kimataifa Mohamed Husein hata kama atampa kamisheni kidogo. Aachane na hizo mbinu za kishamba na za kizamani za kutumia baadhi ya waandishi wa habari na watangazaji. Njia hiyo inaleta mtafaruku sana na kuharibu "future"ya mohamed Husein. Na Henry Mzozo kutafuta watu wamsaidie kumpaisha Mohamed Husein kimatifa sio dhambi na zaidi atajifunza namna ya biashara ya kimataifa ya wachezaji inavyoenda vinginevyo atabaki kuuza wachezaji kutoka Kagera Rangers kwenda Simba, Yanga na vilabu vingine vya ligi kuu huku wenzake kama Jaml Kisongo wanatafuna "dollar" kuanzia Mbwana yupo Kongo, Belgium, Uk na sasa Turkey. Hivi Mzozo alishajaribu kumsikiliza Kisongo anavyoongea kwa weledi kwenye vyombo vya habari kuhusiana na wachezaji anao wasimamia. Kama hajawahi aingie kwenye mtandao ili ajifunze kwani elimu haina mwisho.

Nitamwelewa zaidi Mzozo iwapo atazungumzia kumpeleka Mohamed Husein kimataifa na sio kumchezesha hizo ngoma za Simba na Yanga kwani atakuja kuishia kuwa wa hapa hapa kama Ngasa.

Kwa upande wa Simba nitawalaumu sana uongozi wao kwa kuchelewa kumpa mkataba mpya juu ya mkataba wa zamani Mohamed Husein ili hali wapo na mchezaji kila siku na wanaona kiwango chake kinapanda siku hadi siku. Vinginevyo labda kama mchezaji mwenyewe alikuwa anakataa hapo sawa. Kwa sasa Simba hawana ujanja inawabidi wakubali kukaa chini na uongozi wa Mohamed Husein waisikilize ofa yao na wao waangalie bajeti yao kama inaruhusu. Wakishindwa basi waachane naye waangalie wachezaji wengine kama yule beki wa KMC (jina nimelisahau) au Manyama aliyekuwa Namungo sasa hivi yupo Ruvu wataisadia sana Simba japo viwango vyao havijafika kwa Mohamed Husein. Lakini wakipewa nafasi naamini watafika na hata kupita kiwango cha Mohamed Husein kwani hata yeye alipoanza hakuwa na kiwango hicho alichonacho leo.
 
Nimesikia interview ya kaka mkubwa Heri Mzozo. Kwa alicho kisema Ni wazi kuwa Zimbwe ataenda Yanga.

Kikubwa wanacho kitazama wao kama walezi na management ya Tshabalala ni maslahi ya kijana wao.

Kwa alicho kisema Mzozo kuhusu malipo anayo lipwa Zimbwe pale Msimbazi, kusema ukweli Simba hamumtendei haki kijana wetu na kusema ukweli sintakuwa nimekosea Kama nikisema mnafanyia dhulma.

Hata shabiki wa Simba anae jitambua hawezi kufurahishwa na Jambo hili.

Kweli Tshabalala wa.kulipwa milioni moja na laki tano kwa Mwezi? Hapana.

Imebaki miezi miwili mkataba wake kumalizika.bado hamjafanya nae mazungumzo ya kuongeza mkataba. Kweli?

Mnataka kumtema au mnataka kumlalia mwishoni mwa MSIMU wakati wa dirisha la usajili?

How comes Chikwende analipwa Milioni kumi na nane kwa Mwezi halafu Zimbwe analipwa Milioni moja na nusu?

Signing fee yenyewe nasikia ilikuwa Milioni nne.

Mnamuonea kwa sababu darasa la Saba mtoto wa masikini?

Simba acheni dhulma.

I declare interest Mimi Ni Yanga Lia Lia but I am open minded. Nataka kuona vijana wa kitanzania wanakula matunda ya jasho lao.

Tshabalala karibu Yanga ucheze Mpira ulipwe maslahi yanayo endana na kipaji alicho kujaalia Mwenyezi Mungu, Simba wanamleta Shabani Djuma ndio maana wanakuona wewe haufai Tena.

Pamoja na kwamba tunapitia mapito ya kiuchumi but hatuwezi kukulipa kidhulma Kama unavyofanyiwa Simba.

Narudia maneno ya Mzozo. " Tunacheza Mpira ili tupate pesa na sio majina na umaarufu
UKIONA HIVYO UJUE MENEJA WAKE NFIYE KAMTAPELI. WE UNANWONAJE MZOZO??
 
Back
Top Bottom