INAUZWA Kwa anayetaka kufungua biashara ya kuuzia watu filamu au nyimbo (softcopy) karibu tufanye biashara

Shukrani sana, mimi kwenye mapato sina wasiwasi nitafanya kama ulivyoelekeza, kilichokuwa kinaniumiza kichwa ni kuhusu usalama wa vifaa tu na umenipa wazo.
 
Mbona mimi nimeweza sema watu wanaogopa kujaribu nimeenda mtaani nikaongea vyema nikapata Tb 2 kwa 20000 inawezekana tena anafunguka kila kitu kuhusu hii biashara itategemea umejenga ukariburi kwa namna gani ila inawezekana Ndugu.
Kwa kua wewe umeweza na umekiri umeweza, nataka nikuonyeshe utofauti wa hao waliokuwekea movie 2TB na mimi.

Kaa kwenye mashine yako,ukiwa tayari naomba mimi niwe mteja wako halafu nakupa list ya movie Uniambie unazo au hauna.

Kuna BORA MOVIE na kuna MOVIE ZA KAZI, hapa twende kwa screen shot, nikikwambia movie una screenshot kisha UNANIONYESHA ukiwa tayari njoo.
 
nikapata Tb 2 kwa 20000
2TB kwa 20,000 hata kama mmeongea ukapga sound ukaeleweka nina uhakika kwanza ume enda ofisi ya "wasio jielewa" na wasio jua wanafanya nini,hiyo 1.

Au umeenda ofisi ukamkuta mwenye ofisi hayupo,ulie mkuta si muhusika so ni mtu asie elewa kazi na thamani ya biashara za watu (tunarudi kule kwenye point ya 1,ofisi ni ya wasio jitambua).

Ndio wale vijana wanao achwa ofisini na wao wanaacha watu, hapo kijana alie kabidhiwa ofisi na boss wake morani112 nayeye kageuka boss kamuacha kijana ofisini.

Mzigo wa 2TB unawekea mtu kwa 20,000 (hii sio bei halisi) ni bei ya kijanja janja na kiwizi wizi, nina uhakika kuna namna ktka hiyo ofisi au huyo aliekuwekea movie.

Sishangai kuona iphone 13 inauzwa 100k,haina maana hiyo inayouzwa 200k sio iphone,ila wote tunajua bei ya iphone 13 ni kiasi gani,hata kama ni used used used vipi haiwezi uzwa 100k.

ila mtu akija akiniambia kanunua 100k sitobisha yawezekana kanunua simu ya wizi kutoka kwa mateja au kibaka hivyo sitobisha.

Kwahiyo bwana KIKAZI hiyo bei usije fikiri ni dodo ila kuna janja janja imefanyika au otherwise una tupanga.

morani112 UMEONA MFANO HAI sasa hao ndio vijana unaowaacha ofisini unaona ile kitu nilikua nakwambia yakumuwekea TARGET? anauza 2TB kwa 20k jioni ukienda anakwambia umeme ulikatka hakukua na biashara, Umeona michezo yao hiyo...

Ndio maana mimi nimewawekea target na moja ya masharti yangu ni marufuku kuuza movie JUMLA ni mimi tu ndie ninae ruhusa ya kuuza movie jumla au kutoa go ahead ya biashara hiyo,bila hivyo utatafuta mchawi kumbe mchawi ni wajinga wajinga unaowaita wafanyakazi ukawapa ofisi.
 
We jamaa uko expensive sana,millioni NNE ukidaka watu 100 si unaanza kuitwa millionaire muuza movie?,shusha bei upate wateja wengi ili uwe na mzunguko ambao utakuingizia pesa nyingi sana kuliko kusubiri watu wa millioni NNE ambao unaweza kuwapata wawili au wasipatikane kabisa.
 
Mkuu unanipinga bure tu hapa mjini hakuna kinachoshindikana mjini ukitaka maisha ya kila aina unaweza kuishi yani ya juu au ya chini ili kupunguza gharama ni wewe tu kuchagua tu sipo hapa ili kukupotezea deal lako ila nimepata tena taarifa nyingi zaidi kanipatia kuhusu mzigo mpya unatoka kila siku gani ya wiki kwahiyo mtu akiamua kuingia mtaani hakuna kitacho shindikana pakuanzia pako tena kwa gharama ndogo zaidi huku kila wiki unaigiza mzigo mpya katika stock yako mwisho unakua na mzigo wakutosha.
 
unabishana na ukweli hakuna kinachoshindikana mtaani wewe mwenyewe unajua sema unaleta ubishi tu boss hapa ndiyo bongo dar es salaam nimefuata wazo la mdau mmoja mwanzo kabisa wa uzi na kweli wazo lake limezaa matunda hivyo basi ilikupunguza gharama kwasababu ni mwanzo ni vyema wadau wakaingia kitaa kama mimi nimepata Tb2 kwa 20000 nina amini ata wao wanaweza kupata ili kupunguza gharama za kuanzisha huu mradi maana mpaka taarifa ya mzigo mpya unatoka lini kwa kila wiki utafahamu mwisho hakuna kinachoshindikana chini ya jua ila ninashukuru kwa wazo lako zuri boss.
 
Tunashukuru kaleta wazo zuri la biashara ili tujiwamue vijana ili ukipata deal unaweza kujiongeza mtaani hakuna kinachoshindikana ili kupunguza gharama unabonga vyema na wadau wanakuuzia mzigo kwa bei rafiki kwa maana ndiyo unaanza biashara tena utapata na maelezo wanapochukulia mzigo kila wiki ili kuongeza stock ya mzigo mwisho wa siku hizo 20Tb unzifikia mdogomdogo ndugu.
 
Nimeona, vijana wanaangalia cha juu tu na si thamani ya anachokitoa. Anaweza uza mzigo hata kwa bei ambayo ni pato la siku, maana yeye anaona kama hana anachopoteza kama huyu aliyetoa mzigo kwa 20k.
Sijapinga kuokota dodo kama huyu bwana ila hawezi kuhalalisha hili jambo.
 
Umepata sehemu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nikiweka gharama na thamani halisi ya Movie ninazouza utagundua kuwa milioni 4 ni pesa ndogo na ya Chini sana Mkuu.

Milioni 4 kwa alie serious na anataKA Mzigo wangu ni offer siwezi punguza mkuu japo kuna namna nawasaidia vijana wenzangu wanao enda kuanza.

Nina bei za kusaidiana sana kwa walio serious na wanataka kuanza,Walionifata PM n mashahidi na siku si nyingi mtawaona wakija na shuhuda zao wao wenyewe binafsi.
 
Kwa wanaofanya hii biashara ,Kuna Majanga Matatizo ya Kimaisha ya hapa na pale najua binadamu hawapendi binadamu wenzao wafanikiwe.

ukipatwa na lolote lililokurudisha nyuma au lililopelekea ofisi yako kuyumba na unataka kuanza Upya tena hujakata tamaa,Karibu sana.

Sitokuuzia kwa bei ninayouzia wengine,nitakupa punguzo la almost 50% kwa kila utakachohitaji na vingine nitakupatia BURE kabisa.

Hii ni kwa wale waliowahi anza biashara na wakapata matatzo ya aina yyte Tutasaidana hivyo ondoeni hofu,msiogope nitafuta.
 
Nimekufuata pm hadi namba za simu nimekupa lakini umekaa kimya! Hizo movie unauza kweli au unatupanga tu?

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Nimekufuata pm hadi namba za simu nimekupa lakini umekaa kimya! Hizo movie unauza kweli au unatupanga tu?

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
Yawezekana nawapanga,mpaka waje hapa niliowafanyia kazi ndio utaamini,Sina muda wa kupanga mtu maana sifaidiki na chochote nikifanya hivyo.

Unajua kwanini sijakutafuta?!

Umenifata PM kutaka kuonana na mimi nikushauri mawili matatu, na nilikujibu pale pale kuwa mimi sipatikani ofisini wala sionekani maana sikai ofisini mimi.

nikakwambia siku ukitaka kuniona Jipange uje tufanye kazi niambie uko tayari umekuja tufanye kazi ila sio uje tushauriane, ushauri wote maswali na majibu nayajibu hapa hapa kwenye thread sio OFISINI kwangu.

sio wewe tu,nimeshawakatalia zaidi ya watu 10 wote wakitaka kuja kunitembelea tupge story,Mkuu sina muda wa story na nikisema nikaribishe kila mtu aende ofisini tukae tupge story nadhani haitokua ofisi tena.

Ukiwa tayari kwa Kazi karibu PM niambie upo tayari kwa kazi,halafu utaona kazi yako itafanyika au haitofanyika,nawapanga au siwapangi.

ila kama ni kama ulivyokua ukitaka PM kuja tupge story tupeane mawili matatu Mkuu hapa hapa kwenye thread uliza unachotaka kukijua nitakujibu kwa faida ya wote.

PM ukija ni KAZI, yani ukija PM unaniambia "Mkuu nahitaji mzigo nakupataje naomba utaratibu",nikikutana na ujumbe wa namna hiyo Utaona nitakavyokuchangamkia, ila maswali na majibu ni hapa hapa kwenye hii thread.

au kama hupendi uliza hapa,jipange ukiwa tayari kuja kufata mzigo Utakutana na vijana au kama ukibahatika utakutana na mimi utahoji maswali yote unayohitaji kuyajua.

Narudia tena kama nilivyokuambia PM muda wa kuonana na mimi ni mchache sana sifanyi biashara 1 ya movie useme nitakaa ofisini muda wote. Asante.
 
Ngoja aendelee kuamini kuwa unatupanga! Mimi sio mchangiaji mada sana na sidhan nishawahi kucomment kweny huu uzi. Ila nilipoelewa nachotakiwa kufnya nilienda direct inbox na nikapata majbu na hvi ninavoandika tayari nishapata Mzigo wangu.

Siandiki kumshawishi mtu ila baada ya maswal kadhaa na ushaur kutoka kwa boss mwenyw! (Jina kapuni maake sina ruhusa ya kumtaja japo haitachukua muda kumfahamu pindi ukiamua kufnya nae kazi). Nilijrdhisha nikafuata utaratbu alionipa na nashukuru alifanya zaid ya nilivotegemea na vingne alifanya favor.

Simfahamu kwa sura wala ofis yake ilipo ila nilijirdhisha nikafanya nae kazi. Na kwa uaminifu mkubwa akanitumia mzgo wangu nikiwa mkoani. Umbali mrefu kwel na ili upokee mzgo ilichukua siku mbili ila sikuwa na waswasi.

Tuendelee kupambana vijana, nlichojifunza kutoka kwa huyu mwamba licha ya story mbili tatu tunazopiga. Hii biashara inaweza kukutoa sana kama utajua unachokifanya na ukaamua kuwekeza kwel sio ubahatishe au uige wanachofanya mtaan!. Inatakiwa kuwa tofaut na ufanye zaid ili uwape wateja sabbu za kuja kwako.

Na mwsho zaid UVUMILIVU ni mtaj mwingne hasa kwa sisi tunaoanza. Usitangulize kuingiza elfu 50 wkt hujaandaa hayo mazingira.
Asante
 
Nilikuwa serious nahitaji mzigo ila nilichokuwa nahitaji kutoka kwako ni mawili matatu kuhusu hii biashara na hilo lingeweza kufanyika huku mzigo ukiwa unawekwa kwenye hard disk .....anyway naona haikuwa ridhiki yako kwani nilinunua external hard disk za tb 2 na 4 na nilifanikiwa kuzijaza movie 18000 kwa jamaa mwingine nilieunganishwa na ndugu yangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…