Kwa ardhi tuliyonayo tunashindwa nini kuzalisha alizeti tukawa wauzaji wa mafuta kwa Afrika

Kwa ardhi tuliyonayo tunashindwa nini kuzalisha alizeti tukawa wauzaji wa mafuta kwa Afrika

Huwa tunasingizia tunaimarisha miundombinu ya barabara ili zipitike mpaka mashambani wakulima wasije kukosa kuuza mazao yao.

Lakini Muhindi, Mchina wao wanakuja na hayo mazao yanatoka mpaka huko vichochoroni na wanaondoka nayo. Ufuta mnunuzi mkubwa ni Muhindi na nafikiri Alizeti mnunuzi mkubwa ni Mchina.

Hii nchi baada ya mkulima kulindwa yeye ndiye amegeukwa na kufanywa furushi la dili. Kahawa wameua kwa bei za kijinga wakati wenzetu wa jirani wana bei nzuri sana. Jana nimeona wakulima wakilalamika utitiri wa tozo kwenye hilo zao kitu ambacho kinasababisha bei ya mwisho kwa mkulima kuwa kiduchu sana. Na ipo hivyo kwenye mazao mengi tu..

Tutakapoamua kuwa serious na kilimo tuna ardhi kubwa ya kulima na kubaki na baki kubwa tu tutakaloweza kuuza nje na kubalance trade yetu. Leo hii unakuta asilimia zaidi ya 80 ya mazao yanayotoa mafuta tunauza nje alafu kesho tunaagiza mafuta ya kula kwa haohao tuliowauzia na wakatipiga bei mara tatu zaidi.

Ningependa sana awamu hii tumalize hii miradi yao wanayoiita ya kimkakati then kuanzia 2025 tupate serikali itakayopambana kumkwamua mkulima. Mkulima hatuwezi kumkwamua kwa kumpa mbolea ya rudhuku tu bali kuimarisha mnyororo wote wa thamani kuanzia anapoaanza kuandaa shamba mpaka anapopeleka mazao yake sokoni. INAWEZEKANA!!​
Hivi Bashe hayupo humu? au serikali cyber wao ni kuangalia kinanani wametukana viongozi basi
 
Wale wakianza kilimo kwa uchache wanaanza na ekari 200. Unamkuta mtu ana shamba la ekari 3,000 na lote linazalisha.

Enzi Zimbabwe inaitwa Rhodesia, unamkuta settler ana shamba la ekari 3,000 ndani ana shule kwaajili ya watoto wa wafanyakazi, zahanati na mini supermarket.

Rhodesia ilizalisha mahindi ya kutosha kulisha Afrika.
Hao jamaa wanayo mitaji mikubwa. Wanakuwa pia wanakopesheka benki hata billioni 5 anaweza kupata benki. Unakuta anakuwa na shamba kama eka 4000 au zaidi Halafu lina chanzo cha maji cha uhakika kama mto, bwawa, visima vikubwa. Ameajiri wafanyakazi wake na anawajengea nyumba humohumo wanaishi shambani na wanalipwa vizuri. Mifumo ya kisasa ya umwagiliaji sprinklers, drip irrigation. Matrekta ya kulima na kupanda automatically. Mitambo ya kuvunia, ma godown ya kuhifadhi mazao, mpaka makontena ya 40ft ya kuexport mazao baada ya kuvunwa. Au hata kiwanda humohumo ndani ya estate.

Bongo kupata mtaji au mkopo kama huo labda uwe na ghorofa posta au hati ya kiwanja au sheli kwenye "prime area" na uwe umejenga ghorofa kubwa ndani yake. Kiufupi sisi huku bado tutaishia kuongeaongea tu.
 
Hiki kilimo cha jembe la mkono hakitatutoa katika umasikini, mipango ikiwa mizuri na kila mwananchi anaependa kulima apewe ekari mbili za kilimo na ardhi nyingine iwe kwa commercial farming.

Wawekezaji wapo lakini huwa wanaangalia politica stability, ndiyo maana hawa Makaburu wamekwenda kuwekeza New Zealand na Australia na hawakununua ardhi katika nchi za Afrika ambako tangu Uhuru upatikane viongozi wamekua mabeberu weusi.
 
Kilimo katika nchi hii hakina tofauti na forex, wafanyabiashara ni wanyonyaji sana wanajua kuchezesha bei. Mfumo uliopo unaumiza sana wakulima serikali imelala usingizi tu.
Labda ulime bangi na mirungi
 
Ivi wakuu , alizeti inakubali songea?

na maeneo gani Kwa huko songea unaweza Lima ukapata mavuno mazuri?
 
Sehemu nyingi za Tanzania alizeti inastawi vizuri sana. Kuanzia Singida na hata maeneo ya Handeni. Wakulima wadogo wanalima na wanavuna.

Hawa think tanks wetu hawajaangalia uwezekano wa kufanya uwekezaji mkubwa wa zao hili kiasi cha kutoa ajira nyingi kwa vijana na pia kutiweka kuwa wauzaji wa kuu wa alizeti kwa soko la Afrika?

Ukraine waliwekeza sana kwenye zao hili na mziki wake tunauona baada ya hii vita kuanza. Pamoja na ardhi tuliyonayo, hata sisi ni wateja wa mafuta ya alizeti kutoka huko.
Wanasema baba ndio kichwa cha familia, familia isiyokuwa na uwelekeo wakimaendeleo baba ndio tatizo.

Pascal Mayalla wana ccm nyie ndio baba wa taifa hili nini shida kwenye hili la kilimo
 
Kuna kitu kimoja watu wasikisahau wakaingia kichwa kichwa kwenye mkumbo wa hiki kinachotokea nchini.

Experiance ndogo kwenye kilimo biashara kwa nchi yetu .. Unaweza ukalima ndio .. na ukawekeza pesa ndefu kabisa ... na mazao yakakubali vizuri tuu .

ukishavuna.

Unakutana na kitu kinaitwa bei elekezi/au kanuni ya uuzwaji wa mazao ..Vyama vya AMCOS,,... Sometime unazuiwa kuuza mazao yako Nje ilhali Nchi jirani wao wanaingiza mazao Nchini kwenu ..

IN memorial to 2017 ... Tulifanikiwa kuteketeza mitaji yetu Rukwa kwenye kilimo cha mahindi... Soko la ndani likawa gumu .. mzee akabana mahindi hakuna kutoka .... Basi ikawa hivyoooo.

NB. mtu awaye yote na asiingie kwenye kilimo cha alizeti kichwa kichwa ... afanye utafiti wa kutosha ... ikibidi uwe na uwezo wa kustole product zako hata two years bila mtaji wako kuteteleka.
 
Kilimo chetu ni cha kujikimu i.e small scale farming; hicho hakiwezi kukidhi mahitaji. Tunahitaji kilimo cha kibiashara i.e mkulima anakuwa na heka kuanzia 10,000 na kuendelea, fully mechanized na wataalamu wa kutosha, wanaojua kuangalia ardhi, mbolea, hali ya hewa etc. Hiki kilimo cha kusubiri wingu ndio tuandae mashamba hatutoboi.

1648672056235.png
 
Haya ndiyo matatizo ya small scale farming, hata kiwango cha mazao hupati cha kutosheleza mahitaji ya manunuzi.

Wakulima wakubwa wanao uwezo wa kuzunguka dunia kutafuta masoko. Wana ma godown makubwa na wanahifadhi mazao kwa wingi.

Wanaweza kukutana na mnunuzi anaetaka tani 10,000 za maharage kila mwezi kwa miezi sita au kwa mwaka mzima na wanao uwezo wa kufanya hivyo.

Baada ya Uhuru kulikua na makampuni kama Gapex, haya yalinnunua mazao kutoka kwa wakulima wadogo na kuyakusanya na kusafirisha nje ya nchi. Lakini ukiritimba umeharibu mipango yote hiyo.
 
Kilimo chetu ni cha kujikimu i.e small scale farming; hicho hakiwezi kukidhi mahitaji. Tunahitaji kilimo cha kibiashara i.e mkulima anakuwa na heka kuanzia 10,000 na kuendelea, fully mechanized na wataalamu wa kutosha, wanaojua kuangalia ardhi, mbolea, hali ya hewa etc. Hiki kilimo cha kusubiri wingu ndio tuandae mashamba hatutoboi.

View attachment 2169817
Wale Makaburu wa Afrika Kusini waliajiri watu wengi sana kwasababu Afrika bado kuna cheap Labour. Walipo pull out walisababisha ujambazi kuongezeka kwasababu ghafla tu watu wengi walipoteza kazi na wengine hata nyumba za kuishi.

Hii large scale farming wanawekeza kwasababu ni mali ya familia, watoto na watoto wao wanaendeleza. Familia nyingine zinafuga ng’ombe kwa miaka 100 au zaidi.
 
Wanasema baba ndio kichwa cha familia, familia isiyokuwa na uwelekeo wakimaendeleo baba ndio tatizo.

Pascal Mayalla wana ccm nyie ndio baba wa taifa hili nini shida kwenye hili la kilimo
Msema kweli ni Mpenzi wa Mungu, ni kweli pale mwanzo Baba alikuwa tatizo, na baadhi ya akina sisi watoto, hilo tuliliona, hatuku kaa kimya kwa kunyamaza, tulipaaza sauti zetu kulisema

Huyu Baba wa sasa aliyepo, (japo kijinsia ni mwanamke), ili asifanye makosa kama ya Baba aliyemtangulia anahitaji kusaidiwa kuonyeshwa tatizo ni sisi Watanzania wenyewe kwenye Upangaji wa Vipaumbele Vyetu, baadhi ya sisi Watanzania wazalendo tumeisha libaini hili na tumejitolea kujitokeza kumsaidia kupitia sauti zetu (TV Program ya "Kwa Maslahi ya Taifa" ), au kupitia makala za magazetini "Kwa Maslahi ya Taifa" na huku kwenye mitandao ya Jamii ikiwemo JF, na mfano mzuri ni Makala yangu hii

Tanzania bado tuna tatizo la upangaji vipaumbele vyetu, baada ya Elimu, Afya na kilimo, ilipaswa ije nishati!. Ni aibu na hatari kupikia kuni na mkaa!

Makala hiyo iliandamana na kipindi cha TV kwenye ITV na TBC. Sasa kama Mzee Baba (Mama Babaa) na lile jicho lake (japo limeregea lakini linaona sana), litakuwa limeona, hata kama sio yeye mwenyewe in person, lakini lile jicho lake jingine by proxy linaloona kila mahali , kila kona hadi uvunguni, litakuwa limeona, hivyo Mimi kama raia mwema wa taifa langu, nitakuwa nimetimiza wajibu wangu kwa nchi yangu.

P.
 
Ni swala la muda sisi tunasubiri tuone usemayo kama yatafanyika na tuyatakie heri mipango hiyo..
 
Shida siyo mitaji, ila bei kupangwa na serikali ndio inasababisha wakulima wengi kukimbia kilimo. Hebu imagine kwa sasa bei ya diesel ilivyo juu alaf nimelima tu alizeti kangu alaf mtu aje akupangie bei ya kuuza.
Na hii ndio sababu moja wapo kubwa kwann sikipendi kilimo,na sitokaa nikipende kwasababu hiii

siwezi lima kisasa,kwa gharama,nimefanya research zangu,nmetafuta wataalamu,nmechukua udongo

nimepeleka maabara umepimwa nimepata uhakika kabisa kwa udongo huu zao flan na flan linatoka

halafu baada ya mahangaiko yote hayo,mazao yangu yamekubali kwa 95% anatokea mjinga mmoja (serikali)

ananiambia bei ya hayo maharage yako kilo 1 n sh 1000,hutakiwi uza zaidi ya 1000,Ananipangia bei yeye kama nani? gharama nilizotumia hadi navuna mazao yangu anazijua?

au anahisi nilichimba tu mashmo nikafukia mbegu zikaja zikajiotea zenyewe? ki ufupi serikali isipo ondoka

kwenye kilimo ikaacha watu walime wenyewe na wauze wenyewe Kilimo ndio kitakua dili,ila kwasasa hivi huwezi kuwa mkulima wa Heka 5 10 15 ukaona mafanikio ya kueleweka,ni kudanganyana tu.

ila naweza kaanga Kuku wangu nikawaunga nikawatia mbwembwe nikatoa mshkaki wa kuku nikauza mshkaki m1 20,000, tena nimeweka finyango 3 na karoti zimejipangaaa na vikachumbari umbea,Nauza 20k mshakika wa Kuku 1.

Kuku m1 ananipa mishkaki mpk mi 4,yani napga 80k kwa kuku nliemnunua 7000, Unafkiri ingekuwaje kama serikali ingeniambia mshkaki wa kuku siruhusiwi kuuza zaidi ya 1000,unadhani ningetoboa?

Mahali popote penye kiherehere (serikali) huwezi ona Faida otherwise uwe na capital iliyoshiba na wengi wetu tunasema tukpata capital tutalima ila leo unipe 1B uniambie nilime aw weeee silimi ng'ooo biashara kibaooo nijipeleke kilimoni,siweziiii.

So imekaa hivyo,kilimo ni uti wa mgongo wa maskini sio Tajiri...Tajiri akilima n anaongeza tu income ila tayari ana channel zake hukoooo tusizozijua.

Kilimo Tanzania ni Utumwa.Full Stop.
 
Hatupo serious kwenye mambo yote ya msingi, narudia; mambo yote ya msingi hatupo serious nayo, tunafikiria kuongeza idadi ya mikoa, wilaya, tarafa nk, yaani vichwani mwetu kila kukicha tunawaza namna ya kutumia pesa na sio namna ya kuongeza kipato; fikiria jinsi gani mkulima anavyo bebeshwa mizigo ya TOZO, juzi waziri mkuu na waziri wa kilimo wameondoa baadhi ya TOZO kwa zao la Kahawa; hatufikiri kumuwezesha mkulima instead tunafikiria namna ya kumkamua mkulima. Hali ya hewa ya Njombe, Mufindi, Makete, Babati, Kateshi, Hydom inafanana kabisa na huko wanako lima Ngano and of course hayo maeneo hadi sasa yanalima Ngano, tungekua sisi ni watu makini, tungewekeza nguvu kubwa kwenye kilomo hicho hata ikibidi kwa kumwagilia kabisa ili kina Bakhresa, MO wasikwame kwenye uzalishaji wao wa Ngano processed one; yaani tunasikia RAHA hao jamaa kua wanaleta mimeli mikubwa mikubwa ya ngano kutoka huko duniani. Akitokea mkulima mmoja atakae wekeza huko, utasikia utitiri wa KODI atakao pelekewa. Sijui shuleni huaga tunakwenda kutoa UJINGA au kutafuta vyeti. Long leave RC Mtaka
 
Malaysia wameteka soko la tui la nazi za makopo katika dunia yote ya Magharibi, na mapishi ya kutumia nazi yanaongezeka kutokana na globalisation. Kwakutumia ardhi yetu hata sisi tungeweza kusambaza tui la nazi hata East Africa tu.
Mimi nilishiiwa nguvu baada ya kujua kua hili tui la nazi wanalouza azam na kina simba nazi kua wanaagiza toka Malaysia na sio kutengeneza wenyewe ilihali minazi imejaq
 
Mimi nilishiiwa nguvu baada ya kujua kua hili tui la nazi wanalouza azam na kina simba nazi kua wanaagiza toka Malaysia na sio kutengeneza wenyewe ilihali minazi imejaq
Minazi inapungua kwa kasi sana, mingi iliyopandwa enzi za kale imefikia uzee, kutokana na ugumu wa maisha wengi wanauza minazi ipasuliwe mbao.
 
1649669470008.png

Tanzania tumewahi kuwa namba 3 Duniani kwa uzalishaji wa alizeti mwaka 2014.
Sijui ni nini kilitokea mpaka tukateremka hadi namba 16 mwaka huu.
Source:
 
Back
Top Bottom