Kwa ardhi tuliyonayo tunashindwa nini kuzalisha alizeti tukawa wauzaji wa mafuta kwa Afrika

Tukipata Watu watano, wakawa tayari kutoa 5m Kila Mtu na tukajiunga na ku-process loan bank tunaweza kukusanya 50m Hadi 100m, hii tunaweza kuweka kwenye Alizeti tukafanya wonders. Tukipata 1b tunafanya kilimo Cha umwagiliaji bila kumtegemea Mvua, meaning kuwa Kunakua na stable and quaranteed supply ya Alizeti.

Nimefika Kondoa, Kuna kiwanda Cha Mafuta ya Alizeti, ameshapumzika kwa Amani yule Mzee ila ni uwekezaji mkubwa japo hakifanyi kazi Tena Kwa sasa.

Water table Iko juu sana ukanda wote wa Dodoma, Singida hata baadhi ya maeneo ya Tabora na Shinyanga kwahio irrigation system ni Rahisi sana na pump unafunga za solar.

Sunflower husks ni raw materials ghali sana sana na most of the time zinakua exported. Kwahio huuzi Mafuta tu unauza Hadi hayo mashudu kwa Ajili ya break pads na chakula Cha mifugo....nani Yuko Tayari?
Mimi Niko tyr
 
Mbona kuna mafuta mengi ya alizeti mabarabarani? Ukipita barabarani Singida, Wang'ing'ombe(Njombe), kuna mafuta kibao ya alizeti barabarani. Wauzaji hutung'ang'aniza kununua tukiwa kwenye vyombo vyetu vya usafiri. Uhaba huo uko wapi?
Mbona mashelf madukani yana mafuta ya kula kibao?
Huo uhaba unaosemwa uko wapi?
Kwa mafuta ya kula nadhani kupanda kwake kwa bei, sio issue ya demand and supply forces. Nadhani ni issue ya kupanda kwa gharama za uzalishaji. Sasa hata uzalishe alizeti hadi ya kubaki, bado bei ya mafuta itabaki pale pale.
 
Kwa hali ya sasa nchini Tanzania kuna upungufu mkubwa sana wa mvua. Hata sehemu zilizokuwa zinapata mvua nyingi sasa zinapata mvua chache na zao la alizeti hustawi vizuri kwenye sehemu yenye mvua chache. Nimezunguka Maeneo ya Tarime, sengerema na visiwa vyake karibia vyoote zao la alizeti limepata kulimwa na kustawi vizuri japo sio kwa kiasi kukubwa linalimwa.
Kingine tija ya zao alizeti litaonekana kama nishati ya kukamulia mafuta itakuwa inapatikana kwa bei nafuu. Kama umeme utakuwa nafuu basi mafuta ya alizeti yatakuwa nafuu pia. Ukitizama bei ya lita 5 ya korie toka malyasia, indonesia na sehemu za mbali kama izo ni nafuu kuliko lita 5 ya alizeti toka singida. Kumbe kama umeme utapatikana kwa bei nzuri alizeti itakuwa bei nzuri vinginevyo tutengeneze mashudu tulishe nguruwe tuu.
 
Heka moja ya mawese inatoa mafuta mengi kuliko heka moja ya alizeti. Kumbuka maweze mti wake hudumu miaka na mikaka.
BTW alizeti mafuta yake yanapendekezwa na wataalum wa afya kutumika kuliko mafuta ya mawese.
Zote kwa pamoja alizeti na mawese hutoa malighafi nyingi mbali na mafuta ya kupikia tuu.
 
Mawese yanatoa malighafi gani nyingine zaidi ya mafuta
 
Heka moja ya mawese inatoa mafuta mengi kuliko heka moja ya alizeti. Kumbuka maweze mti wake hudumu miaka na mikaka.
BTW alizeti mafuta yake yanapendekezwa na wataalum wa afya kutumika kuliko mafuta ya mawese.
Zote kwa pamoja alizeti na mawese hutoa malighafi nyingi mbali na mafuta ya kupikia tuu.
Huo muda wa kusubiri mti wa mawese ukue na kuanza kutoa matunda kwa ajili ya mafuta.
Ninaweza kuvuna eneo hilohilo alizeti kwa misimu--sio chini ya mitano.
Nina uwezo wa kubadilisha mbegu kwa haraka zaidi.
Nina uwezo wa kupanda pamoja na mazao mengine pia.
 
Sehemu nyingi za Tanzania alizeti inastawi vizuri sana. Kuanzia Singida na hata maeneo ya Handeni. Wakulima wadogo wanalima na wanavuna.

Hawa think tanks wetu hawajaangalia uwezekano wa kufanya uwekezaji mkubwa wa zao hili kiasi cha kutoa ajira nyingi kwa vijana na pia kutiweka kuwa wauzaji wa kuu wa alizeti kwa soko la Afrika?

Ukraine waliwekeza sana kwenye zao hili na mziki wake tunauona baada ya hii vita kuanza. Pamoja na ardhi tuliyonayo, hata sisi ni wateja wa mafuta ya alizeti kutoka huko.
Sisi ni inchi tajiri, na matajiri hawaangaiki na vilimo, waking’atwa na nyoka je! Au nasema uongo ndugu zanguuu..?
 
Tukipata Watu watano, wakawa tayari kutoa 5m Kila Mtu na tukajiunga na ku-process loan bank tunaweza kukusanya 50m Hadi 100m, hii tunaweza kuweka kwenye Alizeti tukafanya wonders. Tukipata 1b tunafanya kilimo Cha umwagiliaji bila kumtegemea Mvua, meaning kuwa Kunakua na stable and quaranteed supply ya Alizeti.

Nimefika Kondoa, Kuna kiwanda Cha Mafuta ya Alizeti, ameshapumzika kwa Amani yule Mzee ila ni uwekezaji mkubwa japo hakifanyi kazi Tena Kwa sasa.

Water table Iko juu sana ukanda wote wa Dodoma, Singida hata baadhi ya maeneo ya Tabora na Shinyanga kwahio irrigation system ni Rahisi sana na pump unafunga za solar.

Sunflower husks ni raw materials ghali sana sana na most of the time zinakua exported. Kwahio huuzi Mafuta tu unauza Hadi hayo mashudu kwa Ajili ya break pads na chakula Cha mifugo....nani Yuko Tayari?
Mimi niko tiari kwa huu mpango niko Singida
 
Sehemu nyingi za Tanzania alizeti inastawi vizuri sana. Kuanzia Singida na hata maeneo ya Handeni. Wakulima wadogo wanalima na wanavuna.

Hawa think tanks wetu hawajaangalia uwezekano wa kufanya uwekezaji mkubwa wa zao hili kiasi cha kutoa ajira nyingi kwa vijana na pia kutiweka kuwa wauzaji wa kuu wa alizeti kwa soko la Afrika?

Ukraine waliwekeza sana kwenye zao hili na mziki wake tunauona baada ya hii vita kuanza. Pamoja na ardhi tuliyonayo, hata sisi ni wateja wa mafuta ya alizeti kutoka huko.
Kila jambo linaanza na wazo kisha kulifanyia kazi, alizeti uwekezaji wake bado mdogo sana Tanzania na tunaweza tukiamua. Wakulima wanaolima alizeti in bulk quantity ni wachache sana kuweza kukidhi soko letu la ndani na nje ya Tanzania.
 
Serikali inayoendeshwa na wazee wa mjini wanaokula% kutoka Kwa waagizaji wa mafuta usitegemee hoja za kilimo zipite kiurahisi
 
Kila jambo linaanza na wazo kisha kulifanyia kazi, alizeti uwekezaji wake bado mdogo sana Tanzania na tunaweza tukiamua. Wakulima wanaolima alizeti in bulk quantity ni wachache sana kuweza kukidhi soko letu la ndani na nje ya Tanzania.
Miaka ile ya Chama kushika hatamu kulikua na kiwanda cha kuchakata alizeti kuwa mafuta, mafuta ya alizeti yaliuzwa kwenye magaloni ya ujazo wa litre tatu na tano. Hivi viwanda vikiwezeshwa tunaweza kukaba soko la East Africa kwa kuanzia.
 
Tatizo kubwa la Tanzania mrundikano wa kodi unakuta mafuta unayozalisha Tanzania gharama yake ni kubwa kuliko yanayotoka nje lazima ushindwe sokoni
 
Balozi , mwenyekiti .. tfda,tbs, mamlaka ya mawasiliano, trc atcl... Halmashauri .. Taifa ..vat .. pgo .. cdf mabeyo.. ffu ..
 
Tuwe na nishati ya uhakika kwanza na ya bei nafuu alafu Tuje hapa tuzungumze.
 
Back
Top Bottom