Kwa bajeti ya 10M - 12M naweza kupata gari gani used kutoka Japan?

Kwa bajeti ya 10M - 12M naweza kupata gari gani used kutoka Japan?

Kama lengo kubwa ni fuel consumption, achana na magari yenye zaidi ya 1500cc. Mbali ya CIF na TRA, gharama nyingine ni za bima na bandarini (hizi in most cases huwa hazizidi milioni 1).
Mkuu unataka kuniambia hii subaru inatumia chini ya Km 10 kwa lita? Nataka gari inayotumia lita 1 kuanzia Km 10 - 15. Bajeti yangu ya mafuta kwa mwezi ni 180,000/, hii ni hela nauli ninayotumia kwa mwezi. Nataka niibadiri iwe hela ya mafuta. Mizunguko yangu kwa siku ni Km 10, imegawanyika kwenye umbali wa Km mbili mbili. Mpaka sasa ni kati ya Subaru na Spacio ndiyo zipo kwenye mpango
 
Mkuu unataka kuniambia hii subaru inatumia chini ya Km 10 kwa lita? Nataka gari inayotumia lita 1 kuanzia Km 10 - 15. Bajeti yangu ya mafuta kwa mwezi ni 180,000/, hii ni hela nauli ninayotumia kwa mwezi. Nataka niibadiri iwe hela ya mafuta. Mizunguko yangu kwa siku ni Km 10, imegawanyika kwenye umbali wa Km mbili mbili. Mpaka sasa ni kati ya Subaru na Spacio ndiyo zipo kwenye mpango
Umepiga hesabu ya spea na matengenezo
 
Nimeendelea kufanya utafiti nimegundua zipo gari nyingi ambazo ni familly car na zina ukubwa wa engine (CC) wa kawaida tu kama vile HONDA STREAM, VOLKSWAGEN TOURAN, MAZIDA PREMACY, SUBARU EXIGA, TOYOTA SIENTA, n.k lakini upatikanaji wa spea ndiyo tatizo na zipo chini sana (ground clearance) maana matumizi yangu yanahusisha mchanganyiko wa njia za vumbi na lami. Mpaka sasa ninafikiria Spacio, Raum na Honda CR-V, bajeti zake naweza kuongezea kidogo nikapata.
Toyota sienta hapana mkuu...ni bora ununue wish
 
Kodi ni mara mbili yake, imezidi kidogo kwenye bajeti yangu
Chukua used kwa mtu anaedaiwa mkopo au aliyezidiwa madeni inakuwa bado imesimama.
Gari hazishikiki bado Wana mawazo ya kizamani eti gari ni anasa stupid kabisa mawazo ya Mwalimu kuwafanya wengi wawe masikini Ili awatale.
Sheria zetu ni msaafu huwa hazibadiliki.
 
Ushauri wangu ongeza hela upate chombo kizuri utaenda kwa wajanja watakushikisha kisa hela ndogo na unataka kitu kizuri. Au nunua mkononi zipo gari hadi za lakitisa😆😆😆
Za laki tisa? Aisee!
 
Niliongezea hela kidogo nikaagiza kutoka Japani gari aina ya Subaru Forester SG5, L.L Bean Edition, 1994 cc. ya mwaka 2003. Haina mwezi tangu imefika
Hongera mkuu, jumla imekuwa bei gani? type picha mkuu
 
Wakuu habari za asubuhi.

Ni matumaini yangu mmeamka salama siku hii ya pasaka.

Nina mpango wa kununua gari kwa bajeti ya Tshs 10M - 12M. Nipo mkoani na ni mara yangu ya kwanza kumiliki gari. Nina familia ya watu 6 yani wife watoto 3 na house girl.

Matumizi yangu ni kuendea kazini, kuwapeleka watoto shule, kwenda kanisani Jumapili na familia, kwenda mjini kununua mahitaji, na mara moja kwa mwaka kwenda kuwasalimia wazee kijijini.

Kutoka mahali ninapoishi hadi kazini kuna umbali wa 2Km rafu road, kwenda shuleni 3Km (1km rafu, 2Km rami), mjini 4Km (1Km rafu, 3Km rami), kanisani 2Km rafu road na kijijini kwa wazee ni 1150Km, takribani 70 rafu road baada kutoka mkoani.

Naomba ushauri kwa bajeti tajwa hapo juu naweza kupata gari gani inayoendana na matumizi yangu? Nikipata inayotumia mafuta kati ya 10Km - 15km/1Lt inaweza kunifaa.

Natanguliza shukrani za dhati.
Hata Mpwapwaa unapataa
 

Attachments

  • IMG-20230621-WA0001~2.jpg
    IMG-20230621-WA0001~2.jpg
    11.5 KB · Views: 6
  • IMG-20230621-WA0001~3.jpg
    IMG-20230621-WA0001~3.jpg
    10.8 KB · Views: 7
  • IMG-20230621-WA0003.jpg
    IMG-20230621-WA0003.jpg
    49.9 KB · Views: 7
  • IMG-20230621-WA0002.jpg
    IMG-20230621-WA0002.jpg
    63.5 KB · Views: 8
  • IMG-20230621-WA0001.jpg
    IMG-20230621-WA0001.jpg
    41.4 KB · Views: 8
Back
Top Bottom