MINOCYCLINE
JF-Expert Member
- Apr 2, 2015
- 8,018
- 16,802
Nampongeza sana Mshambuliaji Simon Msuva kwa Kufunga Goli zuri, tamu na la Viwango ambalo limetupa Alama Muhimu leo.
Nawapongeza mno Wachezaji wote wa Kikosi cha Taifa Stars kwa Mchezo mzuri walioucheza leo na hadi kutupa Ushindi na kuna Kitu nimegundua kuwa ukitaka Taifa Stars ishinde basi tishia kama Unaisusa Timu Kutoishangilia na Kuwachamba pia Wachezaji ( kama nilivyofanya Mightier hapa JamiiForums Jana ) na watakaza na kujitahidi hadi watashinda.
Nilipongeze pia Bench la Ufundi linaloongozwa na Kocha Paulsen ( anayewajua vilivyo Wachezaji wengi wa Tanzania kwani 75% ya wanaong'aa sasa aliwafundisha Timu za Vijana ) kwa Kupokea Ushauri na Kufanyia Kazi lawama zetu ambazo zimezaa Matunda na leo tumeshinda.
Mightier sitokuwa na Furaha kama leo nisipompa Pongezi zangu nyingi zaidi Kipa namba Moja Aishi Salum Manula kwa Kiwango Kikubwa alichokionyesha na jinsi ambavyo kila Siku anaimarika na Kutuumbua wale tunaomchukia na Kumlaumu kila Siku ( hasa Mashabiki wa Yanga SC )
Kweli Simon Msuva katufungia Goli Muhimu na katuweka patamu ( pazuri ) ila Kwangu Mimi Mightier ( na Sikulazimishi unikubalie ) Mchezaji Bora wa Mchezo ( Man of the Match ) ni Golikipa wa Taifa Stars na Simba Sports Club Aishi Salum Manula.
Hongereni Taifa Stars na Heko Manula.