Kwa documentary ya Pele hii iliyotoka nitakuwa mpuuzi kuendelea kumlinganisha na watoto wadogo kina Messi

Kwa documentary ya Pele hii iliyotoka nitakuwa mpuuzi kuendelea kumlinganisha na watoto wadogo kina Messi

Zamani walikua wanatumia kigezo cha Pele kufunga magoli 12 kwenye michuano yote ya world cup. Wakaja kukutana na akina Gerd Muller wenye magoli 14 akaja Ronald De lima akavunjavunja criteria. Sasa hivi hawasemi hii kitu.
 
Majority walimchagua maradona kamati zikaja na jina mfukoni huoni hiyo ni international robber ya izo kamati za kijinga?
Majority gani mkuu ile ya wapiga kura kutoka ulaya pekee..... Sahivi ningeelewa maana internet iko dunia nzima ssa enzi hizo ipo kwa wazungu tu tena votes 90% zimetoka ulaya unawezaje kupima ukweli wa mambo

Kingine wapiga kura wengi walikuwa hawajawahi kumuona pele hivyo haingekuwa fair kutumia washabiki wa dot com kuchagua wachezaji wa kabla ya uhuru wa tanganyika..... Kwa kuliona hilo ndio maana wakampa pele

Ni sawa na Man of the year ile ya forbes kma sikosei.... Magufuli aliongoza kura kwa mbali sana ila tuzo ikaenda sauzi..... Ni kma vyama vya siasa hapa TZ huwa kura za maoni zinachagua ila kamati kuu ndio inateua nani awe nani hivyo sio mara ya kwanza mfumo huo kutumika duniani

Ndio maana wachezaji wa zamani wote kwa sauti moja wakatoa tuzo ya mchezaji wa karne kwa pele
 
Zamani walikua wanatumia kigezo cha Pele kufunga magoli 12 kwenye michuano yote ya world cup. Wakaja kukutana na akina Gerd Muller wenye magoli 14 akaja Ronald De lima akavunjavunja criteria. Sasa hivi hawasemi hii kitu.
Mbona ya hat trick 92 inasemwa

Magoli 1000 inasemwa

Medali 3 za dhahabu worldcup inasemwa
 
Kuvunja mtu ndyo ubeki bora?


Pique na wenzake wanatumia akili wanacheza modern football sio hao wavunja miguu wako
Ndio nasema enzi hizo hakuna red card hivyo walikuwa wanacheza rafu sana nikimaanisha mastriker wa enzi hizo walipata shida sio sasa hivi mtu anaogopa kadi..... Sijui unaona tofauti
 
Kamati zako uchwara zina role gani kwenye football mbaka zimchague mtu aliyegaragazwa vibaya?
Zilijaa wataalam na makocha wa timu za taifa ambao walimshuhudia pele akicheza ila hao wapiga kura wa kizungu hakuna aliyewahi kumuona pele akicheza sasa nani kati yao anafaa kuaminika

Ni kama leo unaweza shindanisha nani rais bora wastaafu Tanzania kati ya nyerere au kikwete usishangae kikwete akashinda sababu 70% hawakuwepo enzi za nyerere hivyo watampigia kikwete waliyemuona

Hata mayweather vs ali atashinda mayweather kisa wengi hawakumuona ali
 
unfortunately, Uongo ukiongelewa sana unaonekana ni ukweli.

Kwanza. Nimeona huko juu wanaongelea sijui Unicef sijui UN.

UN ni nani katika soka, sikuhizi UN amekua expert wa Soka duniani?.
Kama sio , jiulize ni nani wako nyuma ya UN.
Jibu ni FiFa.
Fifa waliokataa kuistaafisha Jezi nambari kumi ya maradona.
Waliogoma kumweka Maradona kwenye video game zao.

FIFA 100 is a list made by Pelé so it's obviously useless here, not to mention the criteria is questionable.


Tungalie Tuzo binafsi kati ya Pelé 5 na 5 Maradona

FIFA Player of the Century (IFFHS): Pelé [4]

FIFA Player of the Century (popular vote): Maradona [6][emoji123]

World Team of the 20th Century: Pelé and Maradona [4] [6][emoji123]

Mastercard All-Star Team: Pelé (1958, 1970) and Maradona (1986, 1990) [7][emoji123]

FIFA Silver Boot: Pelé (1958) and Maradona (1986) [7][emoji123]
Kwa hiyo shirikisho la wachezaji wa zamani lilipompa pele walikuwa na wenyewe propaganda za fifa

Anyway kwa wewe unaona maradona anamzidi nini pele

Pele goli 1000 maradona 300+
Timu ya taifa pele 77 maradona chini ya 50
World cup pele 3 maradona 1
Ligi pele 6 maradona 2


Kwa ufupi hakuna ambalo maradona anamfikia pele sasa sijui mna base wapi kumpa maradona cheo asichostahili
 
Kumbe mpira wa pelle hakuwa na sheria 17?

Kwaiyo haukua tofauti na chandimu sio?

Kama ndyo hivyo basi ni haki yake kufikisha goal 1000 maana kuna jamaa chandimu kazi ile ya kila siku jioni mechi now ana goal 1500 hizi toka 2008 kwaiyo pelle mchumba tu japo wote wamecheza mpira usio na sheria
Mchumba ??? Wakati alicheza mechi ya portugal mguu unavuja damu na una ogo sababu hamna substitution Enzi hizo unafkiri hawa watoto kina neymar wanaweza

Kuna mechi alivunjwa mguu hadi akastaafu mpira ila jamaa hakupewa hata kadi ndio utalinganisha cku hizi messi kaskumwa kidogo tu red card na penalty..... Embu acheni utani
 
Na vipi kama hao akina Messi ndio wangezaliwa zama hizo, halafu akina Pele wakazaliwa leo? Heshimu kila mtu kwa kile alichokifanya kwa wakati wake.
 
Naomba majibu clear mkuu

1. Mbona kama unaji contradict mwenyewe kupamba mavi maua Mara unasema tuzo alipewa na UN sjui UNICEF huko ndiko kuna makocha na wachezaji walio muona?

2.Unaweza thibitisha statistically kuwa majority waliompigia kura maradona hawakumuona pelle?

3. Walipo amua kuwashindanisha kwa kura walikuwa hawana akili timamu hadi waje kubatilisha ushindi wa Diego?

4.(a)Umejuaje kuwa Jk nyerere na Jk kikwete kuwa kikwete atashinda wakishindanishwa nani kakuambia?

(b) huoni aibu kusema jk kikwete atashinda kwa opinions zako wewe bila kuonyesha fact kwa kuwashindanisha?
1. Hakuna contradictions zozote UNICEF ni branch ya umoja wa mataifa hivyo hata nikiishia kusema UN bado sijakosea maana ni UN ile ile kwahyo hakuna contradictions..... Na wao waliita wataalamu wa soka ndio wakafanya uchambuzi wamejifungia sehem wakatoka na jina la pele ndio akapewa tuzo ya mwanamichezo wa karne na akawa balozi wao tokea hapo

2. Statistically siwezi kuwa na data halisi ya umri wa wapiga kura ila kwa mahesabu ya haraka haraka waliokuwa na access ya kuangalia mechi pele uwanjani kutokea ulaya hawakuzidi 10% sababu by then hakuchezea ulaya kabisa na hakukuwa na live broadcast za mechi kma cku hizi kufikia 1970 pele alipostaafu soka world cup haikuwa na views hata million 300 ila by the time maradona anastaafu rekodi zinaonyesha world cup ya marekani ilivuka watazamaji billion 1 !!! Sasa hapo mkipiga kura nani atashinda more so 1994 wote hao billion 1 walimuona maradona akiwa active tofauti na pele wengi waliomuona miaka ya 50 walishakuwa wazee sana na hawakuwa wengi kufikia waliomuona maradona hivyo hitimisho ni kwamba kma kura zingepigwa mwaka 1980 hivi maradona asingeambulia hata kura 3 ila 1999 waliomuona pele hawakuzidi million 300 world cup 1970 ssa mkipiga kura nani atashinda hata 2050 wakipiga kura atashinda messi sababu wengi wao watakuwa hawajamuona maradona au pele

3. Nimeshasema kura zinatoa picha tu kma ambavyo ballon d'or ilivyo kura zinapigwa ila kamati ya waandishi wa habari ufaransa ndio huwa inaamua nani anachukua..... Hata forbes huwa mnapiga kura kuchagua kiongozi bora alafu wao wanaita wataalam wao wanaamua hata vyama vya siasa mnapiga kura za maoni alafu wataalam wa kamati kuu ndio wanamua nani mgombea hiyo ipo nchi zote kwamba washabiki wanaweza wasijue technicalities ndio maana hushangai hapa TZ unaweza shindanisha bongo star search alafu anaachwa leah muddy anapewa jumanne idd!!!! Ushabiki huwa hauleti uhalisia ila wataalam ndio wanajua nani yupo vzuri na nani hayuko vzuri hivyo ukitaka uhalisia tumia wataalam kama walivyofanya FIFA na zile taasisi 10 zingine

4. Kikwete sijawahi shindanisha ila historia inaniambia hivyo mfano walipopiga kura za best boxer of all time alishinda manny pacquaio na muhamad ali hakupata hata nusu ya kura za manny.... Sasa kwa ushabiki wa aina hiyo huoni hata ambao hawajawahi muona nyerere wanaweza mpigia kura kikwete na kumtosa nyerere kisa hawajawahi muona!!! Hivi hata ww nkikwambja mtu ambaye hujawahi kumuona kuwa ndio bora utamkubali alafu ukamuacha ambaye umeshamuona vya kutosha????

Kikwete atashinda sababu wengi waliopo sahvi wanamuona nyerere kwenye video clip tu
 
Huoni kuwa waliomchezea rafu walikuwa mashoga ivi uvunjwe na shawcros alafu uingie uwanjani mguu umegawanyika angeweza?

Hebu iweke hapa iyo clip anayocheza na hogo mkuu


Ona hapo amevunjwa ila bado anacheza na mguu umevunjika na alimaliza dakka 90 nani sahivi anaweza
 
1.utafiti wa kujifungia huoni kuwa ni wa kupikwa?

2.mbona umeshindwa kuleta data za ulichokuwa unakiongea ina, maana wewe ni muongo?
1. Utafiti si wataalam wanaangalia statistics ama ulitaka wazunguke barabarani kuhoji watu ilihali vigezo walishaweka

2. Takwimu nimeshasema viewers world cup 1970 ni million 300 dunia nzima ila 1994 world cup la mwisho kwa maradona ni billion 1 sasa nani ambaye ameangaliwa zaidi hapo??
 
Unaweza kutofautisha kuvunjwa na kuteguliwa?


Mfano angevunjwa kama macarth wa Everton angeendelea?
Pele alipata fracture kabisa na alifanyiwa operation ila sahvi vikiteguka kidogo tu vinatolewa nje
 
Jibu nilichoandika angevunjika kama macath angecheza?
Sasa ya mc carthy ni special case ila kudislocate ile kawaida tu wachezaji wengi hawawezi cku hzi ila pele beckanbauer na gunter metzer walicheza na dislocation
 
Huoni kuwa ni kukataa wengi kwa maslahi ya wahuni wachache wanaijiita wataalam?
Wengi wasio na utaalamu ina faida gani?? 90% walikuwa washabiki tu ila hawajui vigezo ni sawa na leo wanapiga kura ndio maana kila mwaka messi na christiano ila enzi hizo wasingeshinda mwaka 10 mfululizo hakuna kitu kma hicho ila cku hizi wataalam hawatumiki eti wanapiga kura ila wataalm wangetumika kuamua mpaka ssa xavi iniesta forlan sneijder milito etoo drogba riquelme ribery wangekuwa wameondoka na FIFA player of the year award
 
Wengi wasio na utaalamu ina faida gani?? 90% walikuwa washabiki tu ila hawajui vigezo ni sawa na leo wanapiga kura ndio maana kila mwaka messi na christiano ila enzi hizo wasingeshinda mwaka 10 mfululizo hakuna kitu kma hicho ila cku hizi wataalam hawatumiki eti wanapiga kura ila wataalm wangetumika kuamua mpaka ssa xavi iniesta forlan sneijder milito etoo drogba riquelme ribery wangekuwa wameondoka na FIFA player of the year award

Kuna Ile ya mwaka 2010 Ilikuwa iwe ya Iniesta wakampa Messi,
Iniesta alikuwa na kila kitu akichokuwa nacho Messi , na akamzidi kombe la Dunia na Euro kombe la mabara wakati Messi na alijentina yake walichemka Copa America, Lakin wasiojua vigezo wakampa Messi,
Kisa ana Uefa hahaha dah, wakati na Iniesta anayo, na ndo aliibeba spain kubeba ubingwa Goli lake la 86"

Ya mwaka 2012 wakampa Messi Badala ya Xavi

Xavi alikuwa na Euro , Eufa, La Liga, TOP assits, kiungo mwenye magoli na assists kuzidi wenzake, Lakin walikalili jina messi, ambaye hakuwa na sifa za Xavi,

2013 wakampa Ronaldo Badala ya Ribery
alikuwa na kila sifa ya Kupata hii tuzo
2014 wakampa Ronaldo Badala ya Neur Emanuel
Mwenye
Uefa , World cup, Bundesliga, Ame conceed magoli machache kuliko kipa yeyote, na amekuwa man of match 80% ya mechi alizocheza, duh aisee wanaokalili ushindani wa Ronaldo na Messi wakaidondosha Kwa Ronaldo,


Lakin wanaoelewa watakataa mi ni shabiki wa Messi na Barcelona tangu tuko na Henrik Larson, Kina Kruivert, Romario, Ronaldo de lima (Original)

Lakin ukweli usemwe,

Na sasa Natabili Coutinho anaweza Tisha,
 
Back
Top Bottom