Mwamuzi wa Tanzania
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 15,486
- 45,256
Binafsi darasa la kwanza nilianza nikiwa na miaka 13. Hii ni kwasababu ya kimasingira na kimwamko.
University nimemaliza nikiwa na miaka 30 na ushehe kidogo, kwakuwa nilipomaliza six nikahangahikia ajira kwanza, uamuzi ambao mpaka kesho naufurahia.
Turudi kwenye mada.
Tanzania tunasoma kwa malengo 2 tu.
1. Tufaulu mitihani
Ushahidi uko wazi kabisa Darasa la 4 ,7, kidato cha 4 & 6 likizo zao hazijulikani. Ingekuwa tunasoma ili tuelimike, tugundue vitu kusingekuwa na haja ya madarasa haya 4 kuwa special. Hii kuanzia afisa elimu mkoa mpaka kata yanawanyima usingizi haya madarasa.
2. Tunasoma ili tuajiriwe
Hili kila mzazi anaweza kuwa shahidi. Wazazi wa kipato cha chini, kati mpaka cha juu katika nchi hii hutamani watoto wao waajiriwe. Utofauti ni kwamba mzazi maskini yeye anachojali mwanae aajiriwe tu hasa serikalini bila kujali kada ipi na ofisi ipi huku wazazi matajiri hutamani watoto wao waajiriwe kwenye mashirika ya umma yenye majina makubwa.
Idadi ya wasomi itaongezeka ila tusahau kuhusu uvumbuzi.
Tuendelee kukariri vya wenzetu, tafiti za ukubwani kama zile za SUA na panya magawa, mara wadudu maji moto hazina impact kubwa ulimwenguni.