Kwa elimu hii ya Tanzania tusahau kuhusu uvumbuzi

Kwa elimu hii ya Tanzania tusahau kuhusu uvumbuzi

Binafsi darasa la kwanza nilianza nikiwa na miaka 13. Hii ni kwasababu ya kimasingira na kimwamko.

University nimemaliza nikiwa na miaka 30 na ushehe kidogo, kwakuwa nilipomaliza six nikahangahikia ajira kwanza, uamuzi ambao mpaka kesho naufurahia.

Turudi kwenye mada.
Tanzania tunasoma kwa malengo 2 tu.

1. Tufaulu mitihani
Ushahidi uko wazi kabisa Darasa la 4 ,7, kidato cha 4 & 6 likizo zao hazijulikani. Ingekuwa tunasoma ili tuelimike, tugundue vitu kusingekuwa na haja ya madarasa haya 4 kuwa special. Hii kuanzia afisa elimu mkoa mpaka kata yanawanyima usingizi haya madarasa.

2. Tunasoma ili tuajiriwe
Hili kila mzazi anaweza kuwa shahidi. Wazazi wa kipato cha chini, kati mpaka cha juu katika nchi hii hutamani watoto wao waajiriwe. Utofauti ni kwamba mzazi maskini yeye anachojali mwanae aajiriwe tu hasa serikalini bila kujali kada ipi na ofisi ipi huku wazazi matajiri hutamani watoto wao waajiriwe kwenye mashirika ya umma yenye majina makubwa.

Idadi ya wasomi itaongezeka ila tusahau kuhusu uvumbuzi.

Tuendelee kukariri vya wenzetu, tafiti za ukubwani kama zile za SUA na panya magawa, mara wadudu maji moto hazina impact kubwa ulimwenguni.
Kwa nchi hii unafki ulivyo unaweza kuta hata mtoa mada naye huwa anamnunulia mtihani mwanaye kimagendo ili afaulu vizuri.

Suala hili ni complex lenye mgawanyo wa lawama kwa karibia kila muhusika.

NB: Mtu mweusi kamwe hawezi geuza mchanga/udongo kuwa mashine hata ase na PhD. Weupe peke yao ndio wanaweza.
 
B
Ni kweli mkuu,mfumo huu hautatufikisha popote.Ni Jambo la kusikitisha kwamba hata mfumo huu wa hovyo kabisa umeshachakachuliwa,na umepitwa na wakati sana.Infact ulikuwa designed na Wazungu kama source of "slave labour." Nia haikuwa kupata wavumbuzi from the onset.

Kuna haja ya ku-design system ya kwetu based on vitendo zaidi baada ya basics za I-VII,ingawa nasikia kuna mpango wa kufuta Std.VII,which is a very bad idea indeed kama ni kweli.Tunahitaji kuimarisha STD.I-VII sio kuondoa VII!
Hoja yako sio sahihi. Kuna weusi kibao wamesoma darasa moja na weupe huko ulaya katila levo mbalimbali kuanzia degree hadi PhD lakini mzungu atavumbua kitu wakati mswahili hawezi vumbua.
Mfumo huu huu ndio unaotumika duniani kote ( elimu zinasomana) ndio maana mtu akimiza form IV/Vi/ Bachelor au Master degrees hapa anaweza jiunga A Level/ university dunia nzima na akamudu masomo .katika ngazi za elimu zinazofuata.
 
Huwezi kua na uvumbuzi chini ya serikali ambayo haiona maana ya uvumbuzi

Kama uvumbuzi na teknolojia vitakua kipaumbele cha kwanza cha serikali, kutakua na uvumbuzi na teknolojia

Niamini, shuleni tumekutana na watu wenye vipaji (akili) ambao mpaka leo hatuchoki kuwafikiria, lakini uvumbuzi wowote ule mkubwa nyuma yake kuna mkono wa Serikali, kwanzia Internet mpaka Atomic Bomb

Hao kina Newton na Einstein walitokea kwenye nchi zinazoweka kipaumbele cha kwanza kwenye Elimu, Uvumbuzi na Teknolojia

Huku tuna serikalini inayoweka kipaumbele kwenye "kushinda" uchaguzi ujao, watoto zao kuwa madarakani na bila kusahau 10% kwenye kila mradi wa hovyo watakao kuja nao..... Huwezi kua na uvumbuzi

Tatizo sio Elimu, infact Elimu yetu ni ngumu kuliko, watoto wanasoma vingi kuliko vinavyohitajika.
Good
 
Ni kweli,hata mimi nimesema Ulaya na Wazungu,darasa moja,ila kuna kitu usichokijua.Ni hivii, hali iko hivi Ulaya.Zipo special schools,colleges na special Universities kwa vizazi vya wagunduzi.Unakumbuka hata Tanzania tulianzisha mtindo wa special schools,lakini ziliishia njiani.Infact kwetu haiku-make sense kwa kuwa hatukuwa na "special teachers" wa kuwafukarisha.

Ulaya na Marekani vizazi hivi special vya wagunduzi vina hata special IDs,ingawa ukiangalia kwa macho ID hizo zinaonekana sawa.Mkuu ninalosema ni nini,ndio Ulaya na Marekani wote Wazungu au Blacks,lakini wapo waliochaguliwa kupelekwa special Colleges and Universities kwa ajili ya special assignments zinazohitaji IQ kubwa.
 
Back
Top Bottom