Kwa Experience yangu ya muda mfupi kwenye "Betting" nimegundua mambo machache

Kwa Experience yangu ya muda mfupi kwenye "Betting" nimegundua mambo machache

VinJoe

Member
Joined
Dec 18, 2017
Posts
31
Reaction score
171
Jambo la kwanza na kubwa kabisa betting is addictive very addictive hutaamini itakavyo kukamata na kuingia kwenye mishipa ya damu yaani kuna wakati kukaa bila kua na ka mkeka unakokasubiria ka tick ✅ basi unahisi kama kuna kitu hakiko sawa hivi.

Jambo lingine ni kwamba utakua na matumizi yasio na mpangilio na hii itapelekea usione faida yake lakini mpaka ukija kugundua kua umekua na mfumo mbaya wa maisha na matumizi mabaya ya pesa tayari utakua ushakua addicted na betting

Betting zilizo nyingi hususani zile za casino hua zina kamfumo kakukufanya utamani kucheza zaidi na zaidi na nakuamini una bahati ila kama hutakua mjanja kua ukishapiga hela kubwa kwa siku hio uache na uende ukafanye kitu cha maana na ukija kubet tena iwe ni siku nyingine na ile ulioshinda hakikisha umeshaitumia kwenye mambo yako muhimu. Ukadanganyika baada ya kushinda ukaamini unaweza shinda kubwa zaidi ya hio amini unaweza ukaliwa yote na bado kwa mchanganyiko wa hasira na bado kuamini kua unaweza ukabahatika tena unaweza ukatoa na nyingine mfukoni uka deposit naukaendelea kucheza.

Siku hazifanani kuna siku niliweka buku tu kwenye sportpesa nikaweka mikeka 8 ya shilingia mia mia tu ila kina mingine ilikua ina odds mpaka 2500 kati ya mikeka nane nilishinda mikeka 7 hii ni kwenye e'soccer.
Nilipata hela nyingi sana mpka nikatamani niachane na mambo mengine niwe "professional Sports Bettor" iwe ndio my full time job.. ila siku iliofwata niliweka mikeka mingi sana tena nikiwa nimeweka hela kubwa ila nilishinda kamkeka kamoja na kale kalikokua na total odds ndogo😂 niliendelea kucheza na nikawa nashinda ila sio kama siku ile nilioshinda hela mingi na nikawachukua wanangu kimya kimya sikuwaambia nina beti tukaenda tukaweka heshima bar huku nikijiona mbarikiwa kinyama kumbe ilikua ni siku ile tu.

Kiukweli natamani sana kuacha kubet nishafuta mpaka applications za betting ila kuna mda nakua napata mchecheto mpaka nazi download tena.. ila bado hali yangu ni ile ile kiamaisha zaidi tu nimekua tofauti kidogo nakuamini katika bahati ambacho ni kitu sikua nakiamini hapo nyuma.

Kuhusiana na maswala ya imani na hizi issue za kubeti sitaki niziongelee japo najua kila mtu ana kitu anachokiamini na pia dini zetu zina mafunzo na makemeo mengi tu kuhusu kamari.

Ambao tunabet na hatuoni dalili za kuacha basi tuendelee tu maana kuna watu kadhaa walishawahi toboa kimaisha kisa hizi michezo😂

Na ambao hambeti kwa ushauri wangu msijaribu maana ninachojua hakuna kitu addictive ambacho hakina madhara.
 
Tafuta odds chache kama 2 mpk 3 weka mpunga wa kutosha
Hiki ndio cha muhimu kabisa.
Watu wengi wanakuwa sana sana sana maana wanataka kutajirika kwa pesa ndogo sana yan MTU anaweka 10000/ ods 300 hapo probability ya kushinda ni ndogo sana sana.

Niwakumnushe kwa mfano match ya Yanga na Dodoma Jiji.
Yanga alipewa odd 1.41 lakini probability ya kushinda ilikuwa over 99% so ukiweka 1m unapata laki nne ndani ya DAKIKA 90 tu.

Au ukitaka probability ya 100% ungeipa Yanga apate walau goli mbili ambayo odd ilikuwa 1.3.
Ukiweka 10m unapata milioni 3 ndani ya dakika 90.

Watu tunaishi tunafamilia tunasomesha na kujenga kwa betting tu.
Bet responsibly.

Kubet ni kazi ya watu wenye akili kama huna akili nenda kijijini ukalime viazi mbatata huko.
 
Usithubutu,[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Back
Top Bottom