Kwa Experience yangu ya muda mfupi kwenye "Betting" nimegundua mambo machache

Kwa Experience yangu ya muda mfupi kwenye "Betting" nimegundua mambo machache

Hiki ndio cha muhimu kabisa.
Watu wengi wanakuwa sana sana sana maana wanataka kutajirika kwa pesa ndogo sana yan MTU anaweka 10000/ ods 300 hapo probability ya kushinda ni ndogo sana sana.

Niwakumnushe kwa mfano match ya Yanga na Dodoma Jiji.
Yanga alipewa odd 1.41 lakini probability ya kushinda ilikuwa over 99% so ukiweka 1m unapata laki nne ndani ya DAKIKA 90 tu.

Au ukitaka probability ya 100% ungeipa Yanga apate walau goli mbili ambayo odd ilikuwa 1.3.
Ukiweka 10m unapata milioni 3 ndani ya dakika 90.

Watu tunaishi tunafamilia tunasomesha na kujenga kwa betting tu.
Bet responsibly.

Kubet ni kazi ya watu wenye akili kama huna akili nenda kijijini ukalime viazi mbatata huko.
Niweke mkeka wa milion 10 wakati huo ndani nimebakiza akiba ya shingapi?

Na hiyo milion 10 niliipataje? Si bora kutumia hiyo njia niliyotumia kupata hoyo 10M kuliko betting?

Anyway ila betting sometimes zina hamasa, kwenye zile jackpot watu wameshinda mpaka milion 100 huwa inachamgia sana kuwapa motivation vijana waingie mazima kwenye huu mchezo
 
Nidhamu tu. Betting rahisi sana. Odds 2.5 zinatosha kama utakuwa na nidhamu.
Dau anza na 25k. Unapata kama 48k baada ya kodi.
Opt nzuri inayotoa sana O 1.5 goals

Game nne tu za odds 1.25 unapata odds 2. Unakosaje hela hapo sasa?
Nenda Kule Uholanzi ligi kuu na second league. Bundesliga na bundesliga 2.
Scotland uingereza championship, ligi 1 na 2
 
Nidhamu tu. Betting rahisi sana. Odds 2.5 zinatosha kama utakuwa na nidhamu.
Dau anza na 25k. Unapata kama 48k baada ya kodi.
Opt nzuri inayotoa sana O 1.5 goals

Game nne tu za odds 1.25 unapata odds 2. Unakosaje hela hapo sasa?
Nenda Kule Uholanzi ligi kuu na second league. Bundesliga na bundesliga 2.
Scotland uingereza championship, ligi 1 na 2
Tuoneshe mikeka yako na transaction
 
Yaani bet inaka ibilisi fulani hivi yaani hata ukibet buku mbili lakini akili inakutuma ile pesa ya winning chance ndio yako. Yaani mkeka ukitoka vruu laki nane basi unajihisi ile laki nane ndio yako badala ya buku mbili uliyobetia.
Yaani ukikosa unaona umeloose laki nane lakini kiuhalisia umeloose buku mbili tu.
 
Nidhamu tu. Betting rahisi sana. Odds 2.5 zinatosha kama utakuwa na nidhamu.
Dau anza na 25k. Unapata kama 48k baada ya kodi.
Opt nzuri inayotoa sana O 1.5 goals

Game nne tu za odds 1.25 unapata odds 2. Unakosaje hela hapo sasa?
Nenda Kule Uholanzi ligi kuu na second league. Bundesliga na bundesliga 2.
Scotland uingereza championship, ligi 1 na 2
Upo sahihi,
Mimi nilishapigwa sana hadi nilipojifunza kwamba betting inatakiwa mtaji mkubwa na nidhamu ili kutoboa .
Mimi nacheza hata odd 1.4 ila naweka pesa nyingi kwa mfano unaweza kucheza mechi moja tu odd 1.4 then unaweka 1m ukapata laki tatu baada ya Kodi.
 
Jiulize kwanini Sport pesa wanatumia timu 13 kwenye jackpot yao? Hadi leo watu wanapigwa tu, buku 2 kila mkeka
Wala hujui mambo ya betting.
Ki UHALISIA hizo mechi 13 za jackpot kuna watu wanabet kwa 282000/ kwa double chance wengi TU na WANAKOSA .
 
Wanaojua mbinu nzuri za kubet waeleze hapa ili tufahamu
 
Betting, kubashiri au wengine wanaita mchezo wa kubahatisha ni aina mojawapo ya KAMARI. Kama hujashiriki kwenye betting au aina yoyote ya kamari usiingie na KIMBIA NA KAA NAYO MBALI SANA, na kama unashiriki ukiwa na matumaini kwamba siku moja utatoboa kwa betting, TOKA HARAKA SANA NA KAA MBALI NAYO SANA, betting (Kamari) ni mbaya, haifai ni uraibu ambao ukikupata umekwisha, athari za kamari sio tu katika kupoteza pesa, bali pia inalemaza akili. Najua tunaaminishwa kwamba kuna wachache walipata 'fedha nyingi' kwenye betting (Inategemea tafsiri ya 'fedha nyingi' ina maana gani kwako), lakini hebu jiulize ni asilimia ngapi hao waliopata? je ni kweli wametoboa? Lazima ufahamu kwamba kuna tofauti kati ya kushinda betting na kutoboa kimaisha. Betting inaathiri ubunifu wako wa asili na inalemaza akili na inaathiri hata watu wako wa karibu, hasa kama una familia na marafiki. Mojawapo ya athari kwa wanao bet ni kufikiri kwamba betting au kamari ni njia ya mkato katika kufanikiwa maishani. Hakuna short cut maishani, hakuna, hakuna, hakuna.

Betting inaweza kukusababishia kukata tamaa, kuwa na mawazo mengi, kuamini na kutegemea bahati nasibu kuwa ndiyo njia pekee ya mafanikio kwenye maisha. Betting inawafanya wachezaji kuondoa matumaini kwenye juhudi na maarifa katika kufanya kazi halali. Huwachochea watu wapende fedha nyingi kwa njia ya mkato

KUFANYA KAZI, KUFANYA BIASHARA KUFANYA UJASIRIAMALI (KWA BIDII, KWA NIDHAMU NA UBUNIFU) UKIWA NA MALENGO YA MUDA MREFU NDIO NJIA PEKEE YA WEWE KUPIGA HATUA NA KUPATA MAENDELEO TARATIBU NA HATIMAYE KUFANIKIWA MAISHANI MWAKO - SI KWA NJIA YA BETTING AU KAMARI.
 
Bet ni talata kutoka kwa mola ndio watu wamezaliwa nazo,bet ni kipaji kama kipaji kingine mfano kama.wachezaji,wasani,wanariadha,wanasiasa,marubani,madalali,wanajeshi nakadhalika, so ukitaka kufanya kazi angalia je hii kazi ni kipaji changu?

Ndio maana tumedumaa kimaisha/kiuchumi sababu tunalazimika kufanya kazi ambazo si kipaji chetu.

so beting inawenyewe made, usifanye kwa ajili ya Tama ya pesa
 
Hebu screenshot hizo odds chache na huo mpunga wa kutosha ambao uliwahi kuweka
Mpunga wa kawaida tuu

F3F5D24F-B9E8-418B-A023-3D0D27A3FD20.jpeg


041B7F2E-C76B-46FB-A8FB-572385C57AC0.jpeg
 
Mimi huwa nabet Mara moja moja Sana nimeepuka kuwa addiction nayo..toka nianze kubet Nina miezi Kama 4 lakini nimetumia pesa si zaidi ya laki nanusu na nimekula zaidi ya laki 4. Ukitulia vizuri kinaweza kuwa chanzo Kingine Cha mapato. Muhimu Ni nidhamu na kujifunza zaidi na zaidi.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Betting inahitaji kufanya kazi kwa bidii, coz huwezi kufanya betting kama huna mzunguko wa pesa angalau kuwa na uhakika wa buku 3 na kuendelea kwa siku itakuwa ngumu kuachive.
ukitaka kubeti vizuri hutakiwi kuweka stress kwenye mkeka na stake uliyoweka.

Betting inahitaji records na ufuatiliaji mzuri wa ratiba pamoja na uchambuzi wa kina.
ni vema ukawa na smartphone au kompyuta ili kubet kwa ufanisi.
 
Soon nitaingia chimbo kuandaa kitabu cha betting, nahitaji maoni yenu na sapoti yenu katika hili.
 
Back
Top Bottom