Kwa faida ya watoto waliozaliwa miaka ya themanini na tisini na kuendelea: Nyerere alijenga uchumi wenye nguvu sana chini ya ujamaa na Kujitegemea!

Uchumi imara huo wa kupanga foleni kununua sukari? Kula unga wa mahindi wanayolishwa wanyama tuliyopewa msaada? Ungejua jinsi Nyerere watu walivyokuwa wamemchoka baada ya uchumi kumshinda wala usingesema haya. Jiulize kwa nini uhaini wa kutaka kupindua nchi ulifanyika mara nyingi wakati wa Nyerere?
 
Uchumi wenye nguvu ndio huo ambao mlikuwa mnavaa viraka? 😄😄

Uchumi wenye nguvu ndio huo mlishindwa kujenga hata shule mkaishia kutegemea za wakoloni kiasi kwamba watu wachache sana walipata elimu,Wilaya nzima ina shule moja au hakuna kabisa..

Uchumi wenye nguvu ndio huo mlikuwa mnapanga foleni kununua sabuni kila baada ya miezi 3?

Uchumi wenye nguvu ndio huo mlikuwa mnaishi nyumba za tembe?

Wewe mtoa mada kawadanganye wake zako sio mtu anaeweza kunteason..

Baba yenu wa Taifa ndio amechangia hii Nchi kuwa na watu wenye mdomo sana ,maneno mengi,kulaumu serikali na wenye pesa nk badala ya kufanya Kazi na kutafuta fursa..

Harafu wewe Mzee usiye na akili nani kakuambia kwamba currency exchange rate/value against $ ndio kipimo cha Uchumi imara nani?

Mimi naeongea hapa ni WA miaka ya 80's na mimeonja kidogo ugumu wa maisha..
 
China na Japan hushusha Thamani ya pesa zao kwa lengo la kuboost exports,nyerere alikua anadictate Thamani ya shilingi hakuacha nguvu za soko zifanye kazi(centralized economy)
 
Mwinyi mswahili huwa anadhihaki akikutukuza..akisema aliikuta nchi kwenye foleni ya unga,uchumi imara watu wanakosa mahitaji muhimu!?..chakula,mavazi hata sabuni za kuogea!!?..na inflation kubwa zaidi ilikua kipindi Cha nyerere
 
1 USD = 134 Japanese Yen
1 USD = 117 Kenyan Shillings
1 USD = 11 Botswana Pula

Kwa akili za Wajamaa watakwambia uchumi wa Kenya na Botswana una nguvu kuliko wa Japan.
Okay, vipi kuhusu china? Yuan?
 
Kuna watu wanafikiri serikali kumiliki mashirika ya umma ni ujamaa, UK ndii anaongoza kumiliki mashirika ya umma pamoja na kwamba sio nchi ya kijamaa
 
Upuuzi tu Ujamaa Ndo chanzo cha Umasikini kwa Watanzania
 
Uko Sahihi Kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…