Kwa first year na wanachuo wote

Kwa first year na wanachuo wote

HAMY-D

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2011
Posts
7,149
Reaction score
3,825
Nasikitika sana kuona vijana mnatumia mitandao (kama huu wa JF) kuonyesha umwamba wa chuo kipi bora na kipi sio bora, au taaluma gani bora na ipi sio bora. Hii ina sikitisha sana.

Kwa kifupi, mimi ni mmoja wa watu wakongwe hapa JF kuendesha mijadala hii ya upinzani wa vyuo, kwa kuwa mimi pia nilikuwa mmoja wa watu tuliosoma hivyo vyuo vinavyodhaniwa kuwa ni bora, kwa hiyo nilikuwa upande wa kudharau wale walio soma vyuo vilivyodhaniwa kuwa sio bora.

Upuuzi huu wa kudharau vyuo na taaluma za watu tuliufanya mpaka pale tulipo hitimu masomo na kuingia mtaani.

Mtaa ndio uliamua ni chuo gani bora na ni taaluma gani bora, ila kwa ufupi, wenzetu wengi walio soma IFM, CBE, IAA na TUMAINI walipata ajira kwa haraka, kuliko sisi wa UDSM, ARU, SUA na MZUMBE. Wale wa Muhimbili hawakupata madhara na sababu zinajulikana. Kikubwa kilicho wawezesha kupata kazi kwa haraka ilikuwa ni kufahamiana na waajiri wengi kwa sababu walifanya 'field' kwenye maeneo hayo, ukiachilia mambo kama undugu n.k

kwa muktadha huu, ubora wa chuo na taaluma unaonekana pale wahitimu wanapofyozwa na ajira, kama wahitimu wamezagaa tu mitaani na hakuna mwajiri anae watafuta, hapa ubora wa wahitimu hao upo wapi?

kwa kuhitimisha tu, kusoma chuo fulani na taaluma fulani hakuhitimishi kuwa utaifanyia kazi taaluma hiyo. kwa uchache wa ajira na urasimu wa kupeana kazi kwa kujuana, ni vyema kama wasomi mtumie majukwaa haya kujadili changamoto kama hizo na kuzipatia ufumbuzi badala ya kuendeleza mapambano ya vyuo na taaluma.

Natumaini hili litafanyiwa kazi na wanajukwaa.
 
Ahsante sana mkuu kwa kuonyesha ukongwe juu ya hili suala. Mimi sina hii tabia ila inanikera sana
 
Sijawahi kukukubali hata kwa thread yakp moja kwa zote zilizopita. Ila hii nimekukubali sana kwa kuwa umeonesha kuwa una kiwango cha juu cha kufikiri.
 
Smtymz chuo ulichosoma akimatter in lyf kua na maisha mazuri ni juhud binafsi za mtu na kumuomba Mungu
 
HAMY-D

Mkuu,

Ungeama jukwaa la siasa na kuja kushirikiana nasi hapa penye KITOVU cha MEMA na MABAYA, vijana wananyukana kwa hoja mfu.

Weka kambi hapa angalau kwa week mbili usaidie kundi hili la wasomi wajao wa taifa letu........Labda waweza kumbukwa na Kizazi hiki siku za usoni lakini siyo kule jamvi la si-ha-sa.
Wasalaam.
 
Last edited by a moderator:
Kwa geomatics,architecture,environmentalengineering hakuna anaemaliza chuo na kusota mitaani hawana kazi..sema labda wawe hawajapata wanayoitaka lakini kazi za kufanya na kupata hela ya mahitaji wanafanya..nina reference ndio maana nimekwambia..

Kwani kuuza nyanya na vitunguu sio kazi?, au unadhani wanaofanya hizo kazi wanapenda?, ila all in all wanapata pesa. Changamoto ya ajira ipo kwa wote, hakuna cha Ardhi, UD wala Muccobs.
 
kweli ukubwa dawa,kwa mwenye akili ataelewa ila kumbuka kaka nabii hakubaliki kwao,namaanisha kwamba kuna baadhi ya watu ni lazima watakupinga but all in all hili ni somo lisilohitaji hata tuition.....
 
mtaa unatreat wote equaly! hakuna cha TEKU WALA UDSM! watu wanasota huku ktaa
 
Ardhi University wanatafutwa?

Kuna shahada kama BE, CM, LMV, ARCHTECTURE, INTERIOR DESIGN, REFI, EE, GM, ISM, BAF just to mention few. Hawa wote wapo mitaani na tulikuwa pamoja katika kudharau watu waliosoma IFM, CBE na IAA...

Sikiliza kijana, wewe bado upo chuo, nenda kaulize hao wanafunzi wa Ardhi wanasemaje kuhusu field tu. Kama field tu inawapa shida, hiyo ajira unaisemaje?

Sasa wewe unataka kupotosha watu kuwa waajiri wanawatafuta wanafunzi kutoka Ardhi ili iweje?, Ardhi sio isolated island kijana, tuna wadogo zetu tunasomesha hapo, hata huyo Idrisa Mshoro anajua vizuri hali ya ajira, halafu wewe unataka kujidanganya kuwa hali ni nzuri eti kisa taaluma za hapo ni za kipekee!

Hamy- d umenena kweli.
ninawafahamu graduate wa ardhi wapo mtaani mwaka wa tatu sasa hawajaajiriwa na taasisi yoyote siyo ya serikali au binafsi.
last time nilimpa kazi ya kufanya asset coding.
hakuna chuo wala kozi bira zaidi ya nyingine.
Injinia akidharau mfano BA education watoto wako unataka wafundishwe na nani?
Hesabu zako atazikagua nani? mkopo wako benki atapitisha nani?
mbwa wako nyumbani anaumwa n dokta gani atakuja kumdunga sindano?
Ni utoto na ulimbukeni.
 
kwa ardhi hamy d kidogo sikubaliani na wewe, pale karibia koz nyingi huwezi kukaa mtaan bila kitu cha kufanya ni kama pale wanaosoma COET
 
Tukomeshe ulimbukeni...tukiona thread yakukandamiza chuo..don't support..tuiache izagage..

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
bro unaakiri sana vijana wasikuhizi hawafikirii mbali wanapenda ushabiki ambao hauta wasaidia
 
Back
Top Bottom