Nasikitika sana kuona vijana mnatumia mitandao (kama huu wa JF) kuonyesha umwamba wa chuo kipi bora na kipi sio bora, au taaluma gani bora na ipi sio bora. Hii ina sikitisha sana.
Kwa kifupi, mimi ni mmoja wa watu wakongwe hapa JF kuendesha mijadala hii ya upinzani wa vyuo, kwa kuwa mimi pia nilikuwa mmoja wa watu tuliosoma hivyo vyuo vinavyodhaniwa kuwa ni bora, kwa hiyo nilikuwa upande wa kudharau wale walio soma vyuo vilivyodhaniwa kuwa sio bora.
Upuuzi huu wa kudharau vyuo na taaluma za watu tuliufanya mpaka pale tulipo hitimu masomo na kuingia mtaani.
Mtaa ndio uliamua ni chuo gani bora na ni taaluma gani bora, ila kwa ufupi, wenzetu wengi walio soma IFM, CBE, IAA na TUMAINI walipata ajira kwa haraka, kuliko sisi wa UDSM, ARU, SUA na MZUMBE. Wale wa Muhimbili hawakupata madhara na sababu zinajulikana. Kikubwa kilicho wawezesha kupata kazi kwa haraka ilikuwa ni kufahamiana na waajiri wengi kwa sababu walifanya 'field' kwenye maeneo hayo, ukiachilia mambo kama undugu n.k
kwa muktadha huu, ubora wa chuo na taaluma unaonekana pale wahitimu wanapofyozwa na ajira, kama wahitimu wamezagaa tu mitaani na hakuna mwajiri anae watafuta, hapa ubora wa wahitimu hao upo wapi?
kwa kuhitimisha tu, kusoma chuo fulani na taaluma fulani hakuhitimishi kuwa utaifanyia kazi taaluma hiyo. kwa uchache wa ajira na urasimu wa kupeana kazi kwa kujuana, ni vyema kama wasomi mtumie majukwaa haya kujadili changamoto kama hizo na kuzipatia ufumbuzi badala ya kuendeleza mapambano ya vyuo na taaluma.
Natumaini hili litafanyiwa kazi na wanajukwaa.