Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Mbowe kwenye hotuba yake, akielezea kuwa hawezi kuwaachia watu wengine waongoze chama, baada ya yeye kuwa mwenyekiti kwa miaka 21, alisema kuwa Mtei aliachia umwenyekiti wa chama alipofikishia umri wa miaka 68. Halikadhalika, Bob Makani naye aliachia uongozi wa chama alipofikisha umri wa miaka 68.
Hivyo yeye kwa kuwa sasa ana umri wa miaka 63, hawezi kuachia uongozi kwa chama kwa watu wengine kwa sababu hajafikisha umri ambao watangulizi wake waliachia madaraka, ataachia akigikisha umri wa miaka 68. Aliyasema hayo, bila ya kujali aliowataja, wote waliongoza kwa kipindi cha miaka 5, kila mmoja.
Kama tungekuwa tunafuata falsafa hii ya Mbowe ya kufuata umri wa kiongozi wa mwanzo alioamua kuachia madaraka, ingebidi Marais wote wa Tanzania wasiwe na sifa ya kugombea Urais wakifikisha umri wa miaka 63, kwa sababu Mwalimu Nyerere, Rais wetu wa kwanza, na Baba wa Taifa, aliacha kuendelea kugombea Urais mwaka 1985, akiwa na umri wa miaka 63. Rais Samia kwa sasa ana umri wa miaka 64.
Na kwa tukifuata fikra hizi, yeye Mbowe kwa falsafa yake mwenyewe, hana sifa ya kugombea Urais maana amekwishaufikia umri ambao Mwalimu Nyerere aliondoka madarakani.
NB: Madaraka ya muda mrefu hulevya na kupofusha akili na weledi.