Kwa graduate tu....

Kwa graduate tu....

MTIRO

Senior Member
Joined
May 5, 2012
Posts
120
Reaction score
16
Napenda kuutumia muda huu kimshukuru mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha kimaliza masomo yangu katika chuo kikuu cha dar es salaam. Pia napenda kumshukuru mwenyezi mungu kwa kuendelea kunipa pumzi ya uhai na kunijalia nguvu kwa kipindi chote cha mwaka, sitosita kumuomba Mungu atuwezeshe kuumaliza mwaka salama.

Lengo kuu la makala hii kwa kueleza mtazamo wangu kwa sisi tuliohitimu masomo yetu ya chuo Kikuu, kama ilivyokawaida baada ya kuhitimu masomo yetu kilichobaki ni kutafuta kazi ya kufanya ili tuweze kupambana na maisha either kwa kujiajiri au kwa kuajiriwa. Binafsi toka nilipohitimu masomo yangu mnamo mwezi wa sita nilianza mchakato wa kutuma maombi ya kazi na namshukuru mungu kwa kuwa niliitwa kwenye interview tano ila sikubahatika kupata kazi hata moja.

Baadaya ya kukumbana na changamoto mbalimbali maswali mengi yalinisumbua kichwa changu kubwa ni hili la kuwa nitaomba kazi hadi lini? na je nisipopata hatima ya maisha yangu itakuwa ni ipi ? Haya ndiyo yananisukuma kuandika makala hii leo kwa kuwa ninaimani wapo wanaokumbana na maswali kama hayo.
Kutokana na kufikiri huko nimefikia hitimisho la kuona ni bora kuingia katika ulimwengu wa kujiajiri kuliko kungojea kuajiriwa, hivyo kutokana na hali halisi ya mazingira yetu mwanzo wa kuanza biashara huwa ni mgumu sana endapo utakuwa unafanya peke yako ila ina unafuu endapo tutafanya kama kikundi.
Hivyo basi naomba kama kuna graduate yeyote asiyependa kuajiriwa na ambaye kwa dhati ameamua kuweka vyeti pembeni na kuingia katika ulimwengu wa kujiajiri awasiliane nami ili tuunde kikundi ambacho tutaanzisha biashara na kila mtu atakuwa na share yake. Binafsi Mimi ni mchaga kwa kabila na nimefanya biashara kwa muda mrefu as a part time wakati nikiwa chuo hivyo ninauzoefu na hii kazi na nina imani endapo tukiwa group itakuwa ni rahisi kupata mkopo, kufanya marketing na kusupply na ninaimani we will make a lot of money only if we will be serious na tutasahau kutembea na bahasha kuomba kazi.

Nahitaji vijana watano tu ambao wapo serious na wenye lengo la dhati la kujiajiri wenyewe. Naomba kwa aliyetayari ani PM aweke na namba zake za simu ili tuweze kuwasiliana.

"KWA NINI USOME THEN UKAAJIRIWE NA SIO KUJIAJIRI?" we need to change our mindset.
 
Massawe.................wataka anzisha biashara gan mekuu
 
Aisee biashara zipo nyingi sana kinachohitajika ni vijana ambao wapo serious ili tuweze kuunda group itakayotuwezesha kupata mkopo baada ya kila mtu kutoa kiasi chake.
 
hiyo biashara haitakuwa na ukabila aaa? wataka wanaume/wanawake?
 
No ukabila ni mawazo ya kizamani sana ambayo sisi wasomi haturuhusiwi kuyatilia mkazo, kwenye suala la jinsia haijalishi cha muhimu ni awe serious and very committed.
 
Tatizo umeangalia zaidi elimu badala ya uwezo binafsi.kuna watu wapo tayari ila hawana hiyo elimu ya chuo kikuu.
 
nimehusisha elimu kutokana graduate wengi wanakumbana na hili tatizo ndio maana nikawazungumzia wao. Ila kwa ambaye anajua yuko serious ani PM usijali elimu uliyonayo.
 
Hapa ndo ninapoona umuhimu wa kusoma, nabaguliwa hata na wajasiriamali wenzangu?
Najipa moyo mkuu, SSB inasemekana alikuwa na elimu ya kawaida alipoanza ujasiriamali, nikimuorozesha mmoja kati ya wengi waliofanikisha ujasiriamali.
 
Tafadhali funguka zaidi kwa manufaa ya wengi bila shaka unajambo, huyo SSB ni nani ? je kwani wewe una elimu gani ? pia tambua kusoma ni wakati wowote na ni uamuzi hakika kwa dunia ya leo waweza toka std 7 hadi Phd within 10 yrs or less na ukiendelea na biashara yako kama kawaida huna sababu hata kidogo kuhofia hilo.
 
Aisee biashara zipo nyingi sana kinachohitajika ni vijana ambao wapo serious ili tuweze kuunda group itakayotuwezesha kupata mkopo baada ya kila mtu kutoa kiasi chake.

MTIRO Umesoma/umesomea nini hy degree yako ? What is ur profession ?
 
Wewe msomi kuliko wasomi wote naomba unielimishe, je darasa la saba siyo graduate?
 
Wewe boya huyo SSB ni Bakhresa ambaye amepata elimu ya msingi tu, ndio maana unaonekana kituko hapa wakati hata Bill gates hakumaliza masomo yake Harvard, na kwa tangazo lako hili hata Bill Gates hana sifa ya kujiunga na wewe kwa sababu yeye siyo graduate.

Eti hawa ndio wasomi Tanzania!! My foot aliyeturoga kafa kwa kweli.
 
Una hasira duuu!!! Kaeleza kwa nini graduate hapo juu.Kama nimemuelewa kasema ndio wenye matatizo makubwa ya kutochangamkia biashara kwa sababu ya mindset zao zimekaa kuajiriwa na vile vile wote wanakaribishwa
 
Nawaombeni msiharibu hii thread, MTIRO ameleza vema kabisa pia hajabagua hata kidogo, pia ni vema kujua kuwa elimu sio darasani tu ! ! ! hata hy SSB anayo elimu ya juu sana yawezekana ni sawa kabisa na Masters ni vile tu haikupimwa kimadarasa..... anaweza pata elimu kwa kupitia watu anaowaajiri, wabia wake,, uzoefu,, n.k. maarifa yale yale yanayopatikana madarasani/ university. hakuna kipya utamwambia na degree yako.

Pili; huyo Bill Gate ile kuanza std 1 hadi second year University HUYO SIO MSOMI ? ? Ili mradi tu hakuchukua cheti ?
msidanganywe hakuna mafanikio yeyote kwa dunia ya leo bila elimu ! bila kujali hiyo elimu umeipataje darasani au mitaani au kazini.

Kama Bill Gate alikuwa na akili sana alifata nini University ? ?
 
Napenda kuutumia muda huu kimshukuru mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha kimaliza masomo yangu katika chuo kikuu cha dar es salaam. Pia napenda kumshukuru mwenyezi mungu kwa kuendelea kunipa pumzi ya uhai na kunijalia nguvu kwa kipindi chote cha mwaka, sitosita kumuomba Mungu atuwezeshe kuumaliza mwaka salama.

Lengo kuu la makala hii kwa kueleza mtazamo wangu kwa sisi tuliohitimu masomo yetu ya chuo Kikuu, kama ilivyokawaida baada ya kuhitimu masomo yetu kilichobaki ni kutafuta kazi ya kufanya ili tuweze kupambana na maisha either kwa kujiajiri au kwa kuajiriwa. Binafsi toka nilipohitimu masomo yangu mnamo mwezi wa sita nilianza mchakato wa kutuma maombi ya kazi na namshukuru mungu kwa kuwa niliitwa kwenye interview tano ila sikubahatika kupata kazi hata moja.

Baadaya ya kukumbana na changamoto mbalimbali maswali mengi yalinisumbua kichwa changu kubwa ni hili la kuwa nitaomba kazi hadi lini? na je nisipopata hatima ya maisha yangu itakuwa ni ipi ? Haya ndiyo yananisukuma kuandika makala hii leo kwa kuwa ninaimani wapo wanaokumbana na maswali kama hayo.
Kutokana na kufikiri huko nimefikia hitimisho la kuona ni bora kuingia katika ulimwengu wa kujiajiri kuliko kungojea kuajiriwa, hivyo kutokana na hali halisi ya mazingira yetu mwanzo wa kuanza biashara huwa ni mgumu sana endapo utakuwa unafanya peke yako ila ina unafuu endapo tutafanya kama kikundi.
Hivyo basi naomba kama kuna graduate yeyote asiyependa kuajiriwa na ambaye kwa dhati ameamua kuweka vyeti pembeni na kuingia katika ulimwengu wa kujiajiri awasiliane nami ili tuunde kikundi ambacho tutaanzisha biashara na kila mtu atakuwa na share yake. Binafsi Mimi ni mchaga kwa kabila na nimefanya biashara kwa muda mrefu as a part time wakati nikiwa chuo hivyo ninauzoefu na hii kazi na nina imani endapo tukiwa group itakuwa ni rahisi kupata mkopo, kufanya marketing na kusupply na ninaimani we will make a lot of money only if we will be serious na tutasahau kutembea na bahasha kuomba kazi.

Nahitaji vijana watano tu ambao wapo serious na wenye lengo la dhati la kujiajiri wenyewe. Naomba kwa aliyetayari ani PM aweke na namba zake za simu ili tuweze kuwasiliana.

"KWA NINI USOME THEN UKAAJIRIWE NA SIO KUJIAJIRI?" we need to change our mindset.

Hili wazo lako ni zuri, lakini ungekuwa na WAZO la biashara ingependeza sana! BTW, ipeleke kwenye jukwaa la Uchumi na Biashara huko watu watachangia kiuchumi zaidi, hapa limekaa kama tangazo labda unahitaji watumishi vile!
 
Back
Top Bottom