Kwa Hali inayoendelea nashawika kusema 2025 CCM iondoke madarakani au utawala ubadilishwe!

Wamasai wa ngorongoro ni vita ya kijasusi ambayo ina itesa serikali. Wengi mwaweza msinielewe.
Mkuu TumainiEl tunaokuelewa tupo na tunakuheshimu na kukuzingatia sana!, hivyo keep it up, japo madogo humu ni wengi na hawakujui, wewe endeleza doing the good job you're doing humu na kwa taifa lako.
P
 
CCM ndio tatizo kwanini watanzania hatuelewi?!
 
Suppose ni kweli CCM iondoke, aje nani kwa mfano tuu, baada ya CCM kuondoshwa?.
P
Mkongwe aje yoyote bora CCM ipishe maana imemea mizizi haiheshimu tena misingi ya haki wala wananchi inaowaongoza inatumia ndivyo sivyo mihimili mingine (abuse) kwa manufaa yake na wanachama wake badala ya nchi kwao ni chama kwanza nchi baadae kwao wao ni chama dola kimeshajisahau matakwa ya wananchi sio kipaumbele tena kwao.
 
Siasa ni sayansi, ili CCM iweze kupisha, ni lazima kwanza pawepo mbadala wa kuireplace CCM!, it's very unfortunately Tanzania hatuna mbadala huyo, as a result ni CCM and CCM only, the one and only!.
Uchaguzi 2020 - Je, Tanzania tuna upinzani makini, upinzani wa kweli wa kuing'oa CCM madarakani au bado sana? Nilichoshuhudia leo uzinduzi CHADEMA, kiukweli...
-
P
 
Sawa mkongwe na kada mtiifu kwa maana hiyo tutaendelea kuwa nayo tutake tusitake mbona mnaipeleka nchi kusiko watu wakichoka hawatasikiliza tena sijui kisiwa cha amani mara uzalendo tena hiki kizazi cha sasa cha kuhoji kila kitu .
 
Sawa mkongwe na kada mtiifu lakini lazima nchi yetu ionewe huruma imetafunwa sana na bado inaendelea kwa hayo mambo ya rupia wengi wako kwenye lindi la umasikini licha ya uwepo wa kila aina ya malighafi katika ardhi yetu tena ardhi yenye rutuba ya hali ya juu, tazama mikataba ya KiMangungo tena hatuna budi kuomba radhi ukoo wa Mangungo maana zama zao elimu ilikuwa haijawafikia lakini tazama hawa walioelimika sasa bure kabisa wanauza nchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…