Kwa hali niliyoiona sitashawishika tena kupima UKIMWI

Hivi ni kipimo gani cha haraka zaidi na ni muda gani kinaweza kugundua virusi
 
Waliogopa kukupa majibu unaweza kufa kwa mshtuko.
 
Hawa wataalamu wa afya kwel sijui wapoje mwenyewe nilienda clinic kufika yule mama jaman katoa kipimo anapima utasena malaria af anaweka mbele yangu nione kinavyoenda ye anaendelea na story niliwaza apa hivi presha ikipanda si ninazikwa kabisa aliniboa sana yule mama
 
Hivi ni kipimo gani cha haraka zaidi na ni muda gani kinaweza kugundua virusi

Viral load(RNA PCR) test na combined antibody/antigen test ambapo kwa wenzetu window period ni 28days na sio miezi mitatu
 
Tena wengi wananyoaga siku ya ahadi ya game ili waonekane smart
 

Ilinikuta mkuu, na mfanyakazi mwenzangu tena alitoka mkoa mwingine akaja mkoani na wenzie wawili wakapanga chumba,......

Baada ya kazi kama mwezi tukapanga Party ya pamoja, tukatoka jioni tukachoma Mbuzi na Vinywaji baadae tukaenda Night Club, huku na huku ikawa mda mwingi nipo nae, mara vinywaji mara bolingo na vile aliumbika automaticaly tukajikuta room wawili asubui .......

Nawasha simu watsap nakutana na sms ya mwenzie, ikiambatana na Picha ya kopo la ARV Iikinihasa, niachane nae au nitumie kimba maana wanamjua kaasirika...iyo sms ilitakiwa iingie usiku vile simu yangu ilikua imezima na nilipiga kavu....

Nilipagawa mpaka akastuka ila nkamwambia mambo ya hm, nkamtoa nkaenda Hospital nkapima nkakutwa -ve, nkapewa PEP, mwezi mzima ziliniendasha vibaya nwezi mzima, nkaenda kupima tena mara 2 nkaambiwa sina.... .

Dah, nkajifunza na mbinu mbali mbali juu ya kuepuka na UKIMWI, Ata hivyo skumwambia, alibaki kua friend japo mara kwa mara alikua anataka tena nkawa nampiga kalend tu......

UKIMWI UPO UKITAKA KUAMINI NENDA AU ULIZA WATU WA CTC....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizi lugha ni moja ya chanzo cha watu kukataa kupima na hata wakikutwa + wakaja kusikia lugha kama hizi ndio mwanzo wa kufa moyo.

Tatizo sio kupima na wala tatizo sio huu ugonjwa , tatizo ni watu wanauchukuliaje huu ugonjwa!
Mkuu sijasema kwa ubaya nahisi umechukulia tofauti na mimi nilivyomaanisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahaa hawafai hawa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa usipopima utajuaje hali yako kijana?

Pima uishi kwa amani, maana kama utakuwa negative itakufanya uwe makini na uache kabisa kudinyana dinyana kusiko na mpango...
Mkuu heshima yako.

Sasa kama huyo mtu tumeambiwa toka alipopima tu na kujua kuwa anao; Amepoteza matumaini kabisa.

Ni amani gani nitaipata iwapo nikiambiwa niko HIV Positive?

Mapendo,
TANMO.
 
Hahaa hii komesha kwa wasiotaka kupima kwa hiari nikiwemo mimi. Nakumbuka huo mwaka 2006 nilijitolea damu wakarudi baada ya miezi kama miwili kutuletea majibu baada ya vipimo vya damu tuliyojitolea...nakumbuka niliulizwa kama niko tayari kupokea majibu ya vipimo vyote...nikawa ndo nimepima hapo nimekuja kupima mwaka huu tena kwa lazima

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahaa daah yaani wangejua hali anayokuwa nayo basi tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…