Kwa hali niliyoiona sitashawishika tena kupima UKIMWI

Kwa hali niliyoiona sitashawishika tena kupima UKIMWI

Hivi ni kipimo gani cha haraka zaidi na ni muda gani kinaweza kugundua virusi
 
Baada ya condom kupasuka tukiwa tunagegedana nikamwambia tukapime akakubali alionyesha hofu lakn alijitahidi kuificha.

Tukaenda wote tulipopimwa tukatoka nje kusubiri majibu. Baada ya dakika 20 akaitwa na kuchukuliwa damu mara ya pili.

Muda wa kupewa majibu ukafika. Kweli bhana kumbe anaishi na maambukizi ya VVU.

Nikaeleza mbivu na mbichi nikapewa PEP. Nikazimeza kwa mwezi Mzima. Dawa zile ni kali mno, zinalevya mno na kuchosha. Ndoto za maruweruwe ya kutisha.

Nilipomaliza dawa nikaenda CTC pale Amana. Nikapima Nikaambiwa sina maambukizi. Nikakaa mwezi mmoja nikapima tena nikaambiwa sina.

Yule mwanamke huwezi kumdhania kabisa. Tena ni mnene na ana kalio la haja linaloweza kukudanganya. Kumbe ndani ameungua.
Waliogopa kukupa majibu unaweza kufa kwa mshtuko.
 
Siku hizi hamfanyi aisee zamani ilikuwa kabla ya kupima unapewa counselling ya maana na kabla ya kupewa majibu unafanyiwa counselling juzi nmeenda hospitali Dr kaniandikia tu kipimo cha HIV kama cha malaria vile simple bila hata kuniuliza kama niko tayari kupima

Sent using Jamii Forums mobile app
Hawa wataalamu wa afya kwel sijui wapoje mwenyewe nilienda clinic kufika yule mama jaman katoa kipimo anapima utasena malaria af anaweka mbele yangu nione kinavyoenda ye anaendelea na story niliwaza apa hivi presha ikipanda si ninazikwa kabisa aliniboa sana yule mama
 
Kuna sababu mbalimbali hupelekea pia mtu kuambukizwa ngoma hata kama unatumia kinga..mfano mtu umetoka ku shave sirini af unaenda kurukia,hujui kua yale maj maj yakirukia kwenye pale umeshave na umejikata uwezekano wa kuambukizwa upo,.pia vidonda vya mdomo,mtu una vidonda lakin unaenda chumvin au unapiga mate ya hatar,unategemea nin,..mtu umejikata vidolen,bado unapima oil.
Tena wengi wananyoaga siku ya ahadi ya game ili waonekane smart
 
Baada ya condom kupasuka tukiwa tunagegedana nikamwambia tukapime akakubali alionyesha hofu lakn alijitahidi kuificha.

Tukaenda wote tulipopimwa tukatoka nje kusubiri majibu. Baada ya dakika 20 akaitwa na kuchukuliwa damu mara ya pili.

Muda wa kupewa majibu ukafika. Kweli bhana kumbe anaishi na maambukizi ya VVU.

Nikaeleza mbivu na mbichi nikapewa PEP. Nikazimeza kwa mwezi Mzima. Dawa zile ni kali mno, zinalevya mno na kuchosha.

Ilinikuta mkuu, na mfanyakazi mwenzangu tena alitoka mkoa mwingine akaja mkoani na wenzie wawili wakapanga chumba,......

Baada ya kazi kama mwezi tukapanga Party ya pamoja, tukatoka jioni tukachoma Mbuzi na Vinywaji baadae tukaenda Night Club, huku na huku ikawa mda mwingi nipo nae, mara vinywaji mara bolingo na vile aliumbika automaticaly tukajikuta room wawili asubui .......

Nawasha simu watsap nakutana na sms ya mwenzie, ikiambatana na Picha ya kopo la ARV Iikinihasa, niachane nae au nitumie kimba maana wanamjua kaasirika...iyo sms ilitakiwa iingie usiku vile simu yangu ilikua imezima na nilipiga kavu....

Nilipagawa mpaka akastuka ila nkamwambia mambo ya hm, nkamtoa nkaenda Hospital nkapima nkakutwa -ve, nkapewa PEP, mwezi mzima ziliniendasha vibaya nwezi mzima, nkaenda kupima tena mara 2 nkaambiwa sina.... .

Dah, nkajifunza na mbinu mbali mbali juu ya kuepuka na UKIMWI, Ata hivyo skumwambia, alibaki kua friend japo mara kwa mara alikua anataka tena nkawa nampiga kalend tu......

UKIMWI UPO UKITAKA KUAMINI NENDA AU ULIZA WATU WA CTC....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizi lugha ni moja ya chanzo cha watu kukataa kupima na hata wakikutwa + wakaja kusikia lugha kama hizi ndio mwanzo wa kufa moyo.

Tatizo sio kupima na wala tatizo sio huu ugonjwa , tatizo ni watu wanauchukuliaje huu ugonjwa!
Mkuu sijasema kwa ubaya nahisi umechukulia tofauti na mimi nilivyomaanisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
unachoongea ni sahihi mkuu...kama miez miwili hvi nlkua muhimbili pale jakaya kikwete nachek afya..sasa nikawa nimeshafanyiwa vipimo vyote nlivyoambiwa na daktari ila nikaambiwa baada ya kutoka kwa daktari nipitie kwnye chumba kingine kipo kwnye kona flan hvi...Si nikafika pale nikakaribishwa vzuri kweli nikaelekezwa nikae kwnye kiti..

Asalaleee nashangaa naambiwa bwana humu umekuja tutakufanyia kipimo cha HIV, nikashangaa kwnza nikauliza tena kama kipomo hcho nimeandikiwa / vipi. madaktar wakanambia pale kua hii ni lazima ata ue hujaandikiwa..bas nikaanza kuulizwa maswal mengi pale uku mwngine ananichukua damu tayar kwa kunipima

yan in short skutakiwa kua na hoja nyingine yoyote zaid ya kukubali kupimwa, ila nsshkuru majibu yalikua fresh

Ila skuiz mtu unaeza kupimwa ukimwi hospitali bila ata kuambiwa, unashangaa tu umewekwa kati unafanyiwa kipimo kikubwa
[emoji16]

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahaa hawafai hawa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa usipopima utajuaje hali yako kijana?

Pima uishi kwa amani, maana kama utakuwa negative itakufanya uwe makini na uache kabisa kudinyana dinyana kusiko na mpango...
Mkuu heshima yako.

Sasa kama huyo mtu tumeambiwa toka alipopima tu na kujua kuwa anao; Amepoteza matumaini kabisa.

Ni amani gani nitaipata iwapo nikiambiwa niko HIV Positive?

Mapendo,
TANMO.
 
Kweli kabisa hata mimi nilienda kupima mwezi uliopita yaani unaandkiwa kama vile unapima ugonjwa mafya tu na majibu yanakuja unapewa kama vile taarifa ya mapato na matumizi.

Ila kipindi cha miaka ya 2006/2007 ilikuwa unapewa ushauri wa kutosha na unaulizwa kulingana na maelezo uliyopewa unahisi una asilimia ngapi za kuwa +ve au -ve . Kwa sababu unapewa na elimu jinsi VVU vinayoambukiza kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwengine.

Sasa hivi tena wanakutoboa tu kama kipimo cha malaria ndani dakika tano unapewa jibu so ukikutwa umeambikizwa na haukuwa tayari kupokea taarifa ya hivyo unaweza kuzimika kwa pressure.
Hahaa hii komesha kwa wasiotaka kupima kwa hiari nikiwemo mimi. Nakumbuka huo mwaka 2006 nilijitolea damu wakarudi baada ya miezi kama miwili kutuletea majibu baada ya vipimo vya damu tuliyojitolea...nakumbuka niliulizwa kama niko tayari kupokea majibu ya vipimo vyote...nikawa ndo nimepima hapo nimekuja kupima mwaka huu tena kwa lazima

Sent using Jamii Forums mobile app
 
nilienda sinza palestina..daktari akaniandikia vipimo viwili...kimoja cha maralia kingine ukimwi vyote navijua ila yeye akadhani mi sijui...nimeenda kuchukua majibu ananiambia maralia huna...nikamuuliza na ukimwi je si umeniandikia nipimwe akasema(huku akipepesa macho)..huna ukimwi...sijui kwanini hawasemagi aisee...najaribu kuvuta picha ningekutwa nao..
Hahaa daah yaani wangejua hali anayokuwa nayo basi tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom