pombe hainiharibii chochote
Juzi j2, Nilikaa na Mjomba wangu. Tulikuwa na Kakikao kidogo.
Ofcoz na Monde zinashuka mdogo mdogo.
Katika Maongezi akasema yeye Kaka yake anamchukia sana. Nikauliza kwa nini.
Akanihadithia story ya zaman wakat wako vijana.
Yeye Tumwite Uncle B. Na kaka wa Uncle B tumwite Uncle C.
Uncle C ameshastaafu na alikuwa Dokta Muhimbili.
Uncle B ni Prof na bado anafanya kazi na anakaribia kustaafu.
Prof Uncle B anasema miaka ya nyuma alijitahidi sana kumnasua Uncle C kwenye ulevi uliokithiri. Ni Dokta mzur ila Ulevi aliupa kipaumbele kiasi kwamba hakuna maendeleo amefanya zaid ya kujenga nyumba 2 na kusomesha . Kwa miaka yote akiwa Dokta pale Muhimbili.
Prof Uncle B ana maisha mazur zaid. Sasa Ugomvi wao wa sasa ni kuwa Uncle C anamuonea wivu maendeleo ya mdogo wake. Na amekuwa akipinga vitu ving mdogo wake akisema au kuamua kufanya.
kwahiyo akaniasa kuwa Kunywa Pombe ndio ila hakikisha na maendeleo unafanya. Isije ikafika kipind Huna nguvu tena ukajutia muda na hela ulizopoteza kwenye ulevi wakat ungewekeza.
Na usije ukafika Uzee ukaanza kuonea wivu maendeleo ya ndugu zako . Wakat na ww ungeweza kufanya ila ukaamua kuendekeza kwenye Pombe.
pombe hainiharibii chochote
Unaweza ukahisi Hivi. Kumbe Uhalisia Anauona Bi mkubwa. Kuwa pengine ungekuwa hunywi bas ungekuwa uko Juu zaid ya ulivyo sasa.
Msikilize Bi Mkubwa.
Mwenyewe nikifika 40 yrs natundika daruga 😊😊😊😊