Kwa hatua iliofikia, nataka nigombane na mama mkwe live live

Kwa hatua iliofikia, nataka nigombane na mama mkwe live live

Hatuishi nyumba moja, ugonvi ulitokea mtoto akiwa kwao ndo mana nae akataka kunivaa achukue simu ya mtoto
mbona imekaa kifitina fitina hivi? Huyo mke wako ndio mgombanishi kwa nini amekwambia yote hayo. Angenyamaza tu lakini tena anakuja kukueleza wewe kwa faida gani?
 
Lianzishe Mkuu. Heshima irudi

Kugombana ni Jambo la kawaida sana kwenye Maisha ya binadamu.

Mkwe sio Mungu.
 
Mkuu
Huwa nahofia sana kufanya confrontation hasa na mtu wa karibu ila kwa hatua ilipofikia, nataka nimvae mama mkwe wazi wazi, yani nimpe majibu makavu.

Yeye anataka ku impose sheria zake na kumfundisha mtoto mambo ya ajabu, anakiburi sana na pia ananichukulia ananiweza.

Sababu kubwa ni kua sijawahi kumuonesha ubabe, muda wote nilikua nikimheshimu sana.

Mimi nimegombana na mwandani wangu, et kisha amemkuta analia, anampokonya simu na kumsema kua mimi namsumbua sana mwanae anataka anivae mimi, kwakua sikujiandaa kumchana, nimekata simu, pia bint alikataa kumpa simu.

sipendi tuishi kwa migogoro ila sasa haina jinsi, i have to face the reality, tutaelewana mbele kwa mbele akiwa ananiheshimu

Ni hayo tu, mama wakwe mtulie na ndoa zenu maiingilie mapenzi ya watoto wenu, muda weny ushapita
Busara inaelekeza hivi. Usimpigie simu mamamkwe wala usigombane nae kwa lolote. Maana bado ataendelea kuwa sehemu ya familia yako.

Akitaka kuliongelea hilo jambo letu mwambie naomba nawe ushirikishe upande wako pia. Pasipo kujibizana.

Kama jambo lenu mnaweza limaliza wewe na mkeo bila huyo mama yamalize kisha mtume mkeo aaongee na mama yake.

Kama akitaka kuongea na huku mmeshalimaliza mwambie mama hilo tulishalimaliza. Usimpe nafasi ya kukukera.

Mamamkwe ni mama yako na mama yako ni mamamkwe wa mkeo nae ni mama.

Usiwaruhusu hao watu wawe kero kwenu. Msiwe kero kwao na msiwape nafasi kwenye ndoa yenu.
 
Shemeji yangu nae alikuwa na tabia kama zako nilipiga makofi sana
 
Back
Top Bottom