Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Sabato NJEMA!
Kuna madaktari waliotokea moja Kwa moja Kidato cha Sita kwenda kusoma MD, na wapo ambao wametokea Diploma(Clinical Officer, CO) kwenda kusomea MD.
Kiukweli nimeshtushwa mno baada ya kukutana na Baadhi ya Madaktari watarajiwa wasomao MD na wengine waliomaliza CO.
Mambo yaliyonishtua;
1. Hawajui Lugha ya kingereza.
Kuna kipindi nilifika Pale Mloganzila ambayo Kwa wasioijua ni sehemu ya Hospitali ya taifa ya Muhimbili ambayo kimsingi madaktari wake inatakiwa wawe vipanga na wenye uwezo Mkubwa.
Madaktari waliomafunzoni walinishtua Sana Kwa kingereza Chao kibovu kilichowafanya mara Kwa mara kucheka CHEKA Kwa aibu.
Sitaki kuzungumzia Ma-CO, ambao wengi wao nao kingereza kinawapiga chenga.
Kuna watu watasema, kingereza sio muhimu kwani ni lugha Kama lugha zingine.
Kumbuka materials nyingi za Taaluma ya Udaktari zipo katika Lugha ya kingereza, kutokujua kingereza kutamfanya Daktari kutokuwa mahiri.
2. Clinical officers wa Zama hizi wengi wao sio mahiri, hawako competent katika Taaluma Yao.
Nikikutana na wahitiu wa Diploma ya Clinical officer katika Stori nikiwasabahi nikawauliza mmoja mmoja aelezee concept ya Physiology, mwingine aelezee concept ya anatomy, na mwingine aelezee jinsi damu inavyozalishwa ndani ya Mwili WA mwanadamu.
Unajua hizo ni concept ndogo Sana ambazo hata mwanafunzi wa Kidato cha nne na sita wanaweza Kueleza.
Lakini wakaishia kubwabwaja.
Ukienda baadhi ya Hospitali, madaktari hawajui ku-take patient History, baadhi Yao wanakulazimishia vitu ambavyo havikuumi.
Na hapa nazungumzia madaktari Vijana. Unakuta kijana CV kubwa lakini uwezo unatia Shaka.
Hakuna kitu kinakera Kama uende Hospitalini alafu ukute Daktari anauwezo mdogo katika Fani yake, yaani ukimsikiliza unagundua kabisa hapa hamna kitu.
Ni Sawa na Mwanafunzi afundishwe na mwalimu kilaza, yaani inakera Sana.
Ushauri wangu, siku hizi ukienda Hospitalini kuwa Makini Sana, madaktari wa siku hizi sio wakuwaamini 💯 hasa hawa Vijana.
Serikali iangalie Kwa umakini hivi vyuo vya Kati ambavyo ongezeko lake limekuwa kubwa.
Kuna watu hawatanielewa.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Dar es salaam