Kwa hawa Madaktari huko mbeleni tutapata tabu

Kwa hawa Madaktari huko mbeleni tutapata tabu

Mimi naongea kwa experience, wewe unatumia uzoefu wa ubishi, ngoja nikuache

Na Mimi nakuambia Kwa uzoefu.

Ukiona moja Kati ya hao hawajui kingereza basi jua wanajua kihispania, kireno au kifaransa.

Zingatia; wengi wao sio wote
 
Materials za Taaluma ya Udaktari nyingi zipo Kwa lugha ya kingereza.

Na kutokana na mabadiliko ya magonjwa na madawa Udaktari kila siku unahitaji ku-update.

Huwezi kuwa Daktari mahiri bila kujua Lugha ya kingereza
Napingana na wewe.

Unaweza kabisa kuwa daktari mahiri na usijue Kiingereza.

Kuna madaktari wengi tu mahiri, dunia nzima ambao hawajui Kiingereza.
 
Suala la uwezo ni muhimu sana. Daktari asiyeimudu kazi yake hafai.

Lakini suala la uwezo na suala la kuongea Kiingereza ni vitu viwili tofauti kabisa.

Kuongea Kiingereza kizuri au kibaya, hakuna uhusiano wowote ule wa moja kwa moja na uwezo wa daktari katika kazi yake.

Huwezi kuwa Guru wa sheria Kama hujui kingereza.

Huwezi kuwa Daktari bingwa Kama kingereza kinakuchenga.

Sasa Kama kingereza kinakuzingua kutokana na uhaba WA msamiati utajifunza vipi vitu vipya maana wote tunajua vitu vingi havijaandikwa Kwa lugha ya Kiswahili.

Labda uwe Daktari wa level ya kawaida tuu
 
Hapa unazungumzia udaktari. Siyo uanasheria.

Mimi napingana na wewe.

Unaweza kabisa kuwa daktari bingwa hata kama Kiingereza hukijui vizuri.

Wewe una ‘defeatist attitude’. Mimi nina ‘ a can-do spirit’.

Kuna madaktari wengi tu hapa duniani ambao ni mabingwa na hawajui Kiingereza.

Futa ujinga. Panua wigo wako wa ufahamu.
 
Napingana na wewe.

Unaweza kabisa kuwa daktari mahiri na usijue Kiingereza.

Kuna madaktari wengi tu mahiri, dunia nzima ambao hawajui Kiingereza.

Hawajui kingereza lakini lazima wajue lugha moja Kati ya hizo.

Ki-spain
Kifaransa
Kirusi
Kireno
Kiarabu
Na kichina kidogo.

Kwa sababu material nyingi zimewekwa au kutafsriwa Kwa lugha hizo.

Hapa nchini uwezo wa kutafsri maandiko na vitabu vya kitaaluma Kwa Kiswahili ni kipengele.

Huko vyuoni kozi nyingi hufundishwa Kwa lugha ya kingereza, sasa Kama kingereza hujui utakuwaje mahiri??
Labda uwezo wa Kati tuu.

Sijui Kama umeelewa concept yangu.

Ni Kama vile Kozi ya sheria, unafikiri ingewekwa Kwa Kiswahili watu wangeiona ngumu?
 
Hapa unazungumzia udaktari. Siyo uanasheria.

Mimi napingana na wewe.

Unaweza kabisa kuwa daktari bingwa hata kama Kiingereza hukijui vizuri.

Wewe una ‘defeatist attitude’. Mimi nina ‘ a can-do spirit’.

Kuna madaktari wengi tu hapa duniani ambao ni mabingwa na hawajui Kiingereza.

Futa ujinga. Panua wigo wako wa ufahamu.

Nipo tayari kufuta ujinga wangu, Ila nawe unielewe kuwa, lugha ya Kiswahili kwenye mambo ya kitaaluma bado Sana.

Maandiko na vitabu vinhgi hayajaandikwa Kwa lugha ya Kiswahili.

Huwezi kuwa competent katika somo ambalo huijui lugha yake, labda ukariri tuu.

Kukariri sio utaalamu
 
Hawajui kingereza lakini lazima wajue lugha moja Kati ya hizo.

Ki-spain
Kifaransa
Kirusi
Kireno
Kiarabu
Na kichina kidogo.

Kwa sababu material nyingi zimewekwa au kutafsriwa Kwa lugha hizo.

Hapa nchini uwezo wa kutafsri maandiko na vitabu vya kitaaluma Kwa Kiswahili ni kipengele.

Huko vyuoni kozi nyingi hufundishwa Kwa lugha ya kingereza, sasa Kama kingereza hujui utakuwaje mahiri??
Labda uwezo wa Kati tuu.

Sijui Kama umeelewa concept yangu.

Ni Kama vile Kozi ya sheria, unafikiri ingewekwa Kwa Kiswahili watu wangeiona ngumu?
Wajapan wanatumia lugha zipi kati ya hizo ulizoziorodhesha hapo?

Wajerumani nao wanatumia lugha zipi kati ya hizo?

Waitaliano je? Waturuki je?
 
Wajapan wanatumia lugha zipi kati ya hizo ulizoziorodhesha hapo?

Wajerumani nao wanatumia lugha zipi kati ya hizo?

Waitaliano je? Waturuki je?

Ishu hapo ni uwezo wao kutafsiri maandiko na vitabu vya kitaaluma katika Lugha zao.

Kutafsri nako usidhani ni kazi ndogo,

Nchi hizo na zingine zenye uwezo wa kutafsiri vitabu na majarida ya kitaaluma katika Lugha zao nyingi zipo vizuri Kama vile India.

Kwa muktadha wa Tanzania, machapisho, vitabu na majarida mengi Kam sio yote yapo Kwa lugha ya kingereza na ndio lugha ya kujifunzia, sasa mtu Kama hawezi kingereza unafikiri atakuwa mahiri wa Taaluma husika aliyofundishiwa Kwa lugha asiyoimudu?

Ni Sawa na Malenga wa ushairi wa Kiswahili asiyeimudu lugha ya kiswahili alafu awe mahiri katika Mashairi na Riwaya za Kiswahili.

Ndio maana washairi wengi WA lugha ya Kiswahili wametoka Pwani ya Afrika mashariki Kwa sababu wanamudu Lugha ya Kiswahili.

Huo ni mfano tuu.

Kama Udaktari ungekuwa unafundishwa Kwa lugha ya Kiswahili na vitabu vyake vingi vipo katika Lugha yetu basi ningeungana na wewe
 
Hakuna Daktari wa kichina na kiarabu asiyejua kingereza wadanganye hao hao wajinga.

Hao warusi ukiona hajui kingereza basi ujue anajua ki-spain au kireno.

Nenda Dubai, Qatar, kote huko
Wewe utakuwa hujatembea nchi zingine, ma Dr wengi tu wa china , india na nchi nyingi hawajui kingereza wanajua lugha ya kitabibu, kingereza hakitibu mgonjwa
 
Uko sahihi mkuu

Embu niambie wewe sio humudu vizuri Kiswahili labda Kwa vile umetokea Umasaini, au usukumani, hujui msamiati mwingi WA Kiswahili.

Embu niambie utakuwaje mahiri kwenye Fani ya ushairi kumshinda mtu aliyezaliwa Pwani Kama vile ZANZIBAR, Dsm, Tanga na Mombasa?

Utamshindaje Shaaban Robert?
 
Kwenye competency sawa, graduants wengi wako less competent. Ila kuhusu lugha taaluma ya udaktari inampitisha mwanafunzi kwenye lugha zaidi ya kiingereza. Yaani kuna Latin, Greece, Yunan na kadhalika.
 
Wewe utakuwa hujatembea nchi zingine, ma Dr wengi tu wa china , india na nchi nyingi hawajui kingereza wanajua lugha ya kitabibu, kingereza hakitibu mgonjwa

Kingereza hakitibu ndio Ila ndio lugha ya kujifunzia huo utabibu.
Sasa la huijui lugha inayokufanya uwe tabibu utakuwaje tabibu mahiri?

Hizo nchi za China na India wanajifunza utabibu Kwa kutumia kingereza? Au wanatumia lugha zao?
 
Sabato NJEMA!

Kuna madaktari waliotokea moja Kwa moja Kidato cha Sita kwenda kusoma MD, na wapo ambao wametokea Diploma(Clinical Officer, CO) kwenda kusomea MD.

Kiukweli nimeshtushwa mno baada ya kukutana na Baadhi ya Madaktari watarajiwa wasomao MD na wengine waliomaliza CO.

Mambo yaliyonishtua;

1. Hawajui Lugha ya kingereza.
Kuna kipindi nilifika Pale Mloganzila ambayo Kwa wasioijua ni sehemu ya Hospitali ya taifa ya Muhimbili ambayo kimsingi madaktari wake inatakiwa wawe vipanga na wenye uwezo Mkubwa.

Madaktari waliomafunzoni walinishtua Sana Kwa kingereza Chao kibovu kilichowafanya mara Kwa mara kucheka CHEKA Kwa aibu.

Sitaki kuzungumzia Ma-CO, ambao wengi wao nao kingereza kinawapiga chenga.

Kuna watu watasema, kingereza sio muhimu kwani ni lugha Kama lugha zingine.
Kumbuka materials nyingi za Taaluma ya Udaktari zipo katika Lugha ya kingereza, kutokujua kingereza kutamfanya Daktari kutokuwa mahiri.

2. Clinical officers wa Zama hizi wengi wao sio mahiri, hawako competent katika Taaluma Yao.

Nikikutana na wahitiu wa Diploma ya Clinical officer katika Stori nikiwasabahi nikawauliza mmoja mmoja aelezee concept ya Physiology, mwingine aelezee concept ya anatomy, na mwingine aelezee jinsi damu inavyozalishwa ndani ya Mwili WA mwanadamu.
Unajua hizo ni concept ndogo Sana ambazo hata mwanafunzi wa Kidato cha nne na sita wanaweza Kueleza.

Lakini wakaishia kubwabwaja.

Ukienda baadhi ya Hospitali, madaktari hawajui ku-take patient History, baadhi Yao wanakulazimishia vitu ambavyo havikuumi.

Na hapa nazungumzia madaktari Vijana. Unakuta kijana CV kubwa lakini uwezo unatia Shaka.

Hakuna kitu kinakera Kama uende Hospitalini alafu ukute Daktari anauwezo mdogo katika Fani yake, yaani ukimsikiliza unagundua kabisa hapa hamna kitu.

Ni Sawa na Mwanafunzi afundishwe na mwalimu kilaza, yaani inakera Sana.

Ushauri wangu, siku hizi ukienda Hospitalini kuwa Makini Sana, madaktari wa siku hizi sio wakuwaamini 💯 hasa hawa Vijana.

Serikali iangalie Kwa umakini hivi vyuo vya Kati ambavyo ongezeko lake limekuwa kubwa.

Kuna watu hawatanielewa.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Dar es salaam

Hapa kuna mambo mengi yanawekwa pamoja:
1: Kusoma maneno ya kingereza na kuyaelewa.
2: Kuongea kingereza (generate sentensi mwenyewe)
3: Kujua basics za kazi yako, na kuwasilisha kwa lugha ya wagonjwa wako.

NB: Kama unaweza kusoma na kuelewa kingereza, basi utaweza kuwatibia watu wako bila shida kwani utawasiliana nao kwa lugha yao ya asili ambayo ni yako pia.

Na utakuwa na basic skills na knowledge, kwanu ulijuwa unasoma na kuelewa. Ila utashindwa kugenerate hayo mawazo kwa kiingereza ukiwa huru. Ndo maana tuna maprofesa wakiongea kingereza, wengi huwa wana hoji alifikaje huko?

Tatizo letu wengi liko kwenye kuwa na misamiati michache na kunapelekea, kufikiria kwa kiswahili ndo tunabadilisha kwenda kingereza. Badala ya kufikiria moja kwa moja kwa kingereza na kuongea.

Ingawa bado kuna wale ambao. 1 mpaka 3 ni tatizo na hii ni kwa fani zote. Hivyo, inategemea ulikutana na yupi kati ya hao. Hivi vitu vinategemeana, lakini si direct proportion/si moja kwa moja bali inategemea unaenda kuhudumia jamii ipi, ulipata basic skills za kutosha, unahitajibkutumia lugha ya kigeni kwenye kazi zako?
 
Kama wanasoma kiingereza kwa kiswahili unategemea waongee kiingereza kilichonyooka!!
 
Kuongea kingereza sio ttzo ila shida inakuja ni taaluma gan au ni sekta gan upo kwa Tz madaktari husoma na ufundishwa na vitabu vyao ving vimeandikwa kiingereza
Unaweza ukasema mbona China ,India Russia hawaongei kiingereza ila wanamadaktar na wanatibu ila tunasaha kua ayo ni mataifa makubwa na mfumo wao wa elimu wameuunda wao kulingana na mazingira yao ila kwa sisi Tanzania mfumo wetu wa elimu bado tumekopy West kwa wazungu

Nmesema tu ila mm sio daktar ni maoni tu
 
Kingereza hakitibu ndio Ila ndio lugha ya kujifunzia huo utabibu.
Sasa la huijui lugha inayokufanya uwe tabibu utakuwaje tabibu mahiri?

Hizo nchi za China na India wanajifunza utabibu Kwa kutumia kingereza? Au wanatumia lugha zao?
Na ndio maana nikakwambia wanajua lugha za kitabibu sio kingereza cha kuongea na hiyo ipo kwa wataalamu wengi too sio ma Dr. Peke yao hata engeneers na kada zingine

Tofautisha lugha ya mazungumzo na lugha ya kitaaluma ni vitu viwili tofauti kabisa
 
Materials za Taaluma ya Udaktari nyingi zipo Kwa lugha ya kingereza.

Na kutokana na mabadiliko ya magonjwa na madawa Udaktari kila siku unahitaji ku-update.

Huwezi kuwa Daktari mahiri bila kujua Lugha ya kingereza
English ya kusoma na kuelewa concept haijawahi kuwa tatizo kubwa kwa wanataaluma wengi kibongo..
 
Back
Top Bottom