Kwa hawa Madaktari huko mbeleni tutapata tabu

Concept yako ni nini?
Ni daktari kujua kingereza au kuwa multilingual?
Inasaidia nini kwenye taaluma yake?

Daktari ili awe mahiri anapaswa kujua, na kuimudu lugha ya kujifunzia Udaktari wakez Kwa hapa nchini lugha ya kujifunzia ni Kingereza.

Wapi hujaelewa ndugu.

Utabibu Kwa Zama zetu huja Kwa kusoma, kusoma lazima lugha ihusike.
Kwa bahati mbaya lugha inayotumika ni kingereza hapa NCHINI, na materials nyingi za kujifunzia zipo katika Lugha ya kingereza,

Bado hatujazitafsiri Kwa lugha zetu, na kutafsiri pia usidhani ni KAZI rahisi, inahitaji Wataalamu na Fedha ya kutosha.

Kama huimudu lugha ya kujifunzia huwezi kuwa mahiri kwenye somo husika, utakuwa wakawaida Sana na mtu wa kukariri kariri tuu.

Mataifa uliyoyataja lazima ujue aidha yametafsiri materials za kujifunzia Kwa lugha zao wenyewe hivyo wanazifanya zieleweke Kwa urahisi na Kama hawajatafsiri basi lazima wajifunze lugha zingine ambazo materials ya kujifunzia zimeandikwa kwazo
 
Sabato NJEMA!

Kuna madaktari waliotokea moja Kwa moja Kidato cha Sita kwenda kusoma MD, na wapo ambao wametokea Diploma(Clinical Officer, CO) kwenda kusomea MD.

Kiukweli nimeshtushwa mno baada ya kukutana na Baadhi ya Madaktari watarajiwa wasomao MD na wengine waliomaliza CO.

Mambo yaliyonishtua;

1. Hawajui Lugha ya kingereza.
Kuna kipindi nilifika Pale Mloganzila ambayo Kwa wasioijua ni sehemu ya Hospitali ya taifa ya Muhimbili ambayo kimsingi madaktari wake inatakiwa wawe vipanga na wenye uwezo Mkubwa.

Madaktari waliomafunzoni walinishtua Sana Kwa kingereza Chao kibovu kilichowafanya mara Kwa mara kucheka CHEKA Kwa aibu.

Sitaki kuzungumzia Ma-CO, ambao wengi wao nao kingereza kinawapiga chenga.

Kuna watu watasema, kingereza sio muhimu kwani ni lugha Kama lugha zingine.
Kumbuka materials nyingi za Taaluma ya Udaktari zipo katika Lugha ya kingereza, kutokujua kingereza kutamfanya Daktari kutokuwa mahiri.

2. Clinical officers wa Zama hizi wengi wao sio mahiri, hawako competent katika Taaluma Yao.

Nikikutana na wahitiu wa Diploma ya Clinical officer katika Stori nikiwasabahi nikawauliza mmoja mmoja aelezee concept ya Physiology, mwingine aelezee concept ya anatomy, na mwingine aelezee jinsi damu inavyozalishwa ndani ya Mwili WA mwanadamu.
Unajua hizo ni concept ndogo Sana ambazo hata mwanafunzi wa Kidato cha nne na sita wanaweza Kueleza.

Lakini wakaishia kubwabwaja.

Ukienda baadhi ya Hospitali, madaktari hawajui ku-take patient History, baadhi Yao wanakulazimishia vitu ambavyo havikuumi.

Na hapa nazungumzia madaktari Vijana. Unakuta kijana CV kubwa lakini uwezo unatia Shaka.

Hakuna kitu kinakera Kama uende Hospitalini alafu ukute Daktari anauwezo mdogo katika Fani yake, yaani ukimsikiliza unagundua kabisa hapa hamna kitu.

Ni Sawa na Mwanafunzi afundishwe na mwalimu kilaza, yaani inakera Sana.

Ushauri wangu, siku hizi ukienda Hospitalini kuwa Makini Sana, madaktari wa siku hizi sio wakuwaamini 💯 hasa hawa Vijana.

Serikali iangalie Kwa umakini hivi vyuo vya Kati ambavyo ongezeko lake limekuwa kubwa.

Kuna watu hawatanielewa.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Dar es salaam
Utabibu mzuri haupatikani kwa KUJUA KIINGEREZA, KUWA KIPANGA FORM SIX Wala KUKAA SANA DARASANI.

Utabibu mzuri unatokana na UZOEFU Kazini.

- Patient cases ngapi umekutana nazo na kufanya clerking.

- Juhudi binafsi za mtu husika kujifunza ( Mambo yanabadilika Kila siku). Dawa zinabadilika na hata magonjwa Kila wakati yanaibuka mapya.

Unaweza ukawa MD lakini ukikutana na ACO unakaa chini.

Kwakuwa haupo sekta ya afya huwezi kujua.

Kuna kituo kimoja Kuna MD hata kutahiri hawezi na ndio in charge. Akija mtu, Kuna nurse ndio anafanya.

Na Mara nyingi kuhusu matibabu Ni Mungu tu huwa anasaidia.
 
Daktari ili awe mahiri anapaswa kujua, na kuimudu lugha ya kujifunzia Udaktari wakez Kwa hapa nchini lugha ya kujifunzia ni Kingereza.

Wapi hujaelewa ndugu.

Utabibu Kwa Zama zetu huja Kwa kusoma, kusoma lazima lugha ihusike.
Kwa bahati mbaya lugha inayotumika ni kingereza hapa NCHINI, na materials nyingi za kujifunzia zipo katika Lugha ya kingereza,

Bado hatujazitafsiri Kwa lugha zetu, na kutafsiri pia usidhani ni KAZI rahisi, inahitaji Wataalamu na Fedha ya kutosha.

Kama huimudu lugha ya kujifunzia huwezi kuwa mahiri kwenye somo husika, utakuwa wakawaida Sana na mtu wa kukariri kariri tuu.

Mataifa uliyoyataja lazima ujue aidha yametafsiri materials za kujifunzia Kwa lugha zao wenyewe hivyo wanazifanya zieleweke Kwa urahisi na Kama hawajatafsiri basi lazima wajifunze lugha zingine ambazo materials ya kujifunzia zimeandikwa kwazo
Naomba upate nafasi idhurie kipindi cha hao ma CO wakiwa wanafundishwa, ni majanga tu, mualimu nikama anaufundisha historia ya udakitari tena kwa lugha kiswahili, yani waalimu wenyewe are not competent......mimi nikipata pesa elimu ya hapa kwetu hapana
 
Sabato NJEMA!

Kuna madaktari waliotokea moja Kwa moja Kidato cha Sita kwenda kusoma MD, na wapo ambao wametokea Diploma(Clinical Officer, CO) kwenda kusomea MD.

Kiukweli nimeshtushwa mno baada ya kukutana na Baadhi ya Madaktari watarajiwa wasomao MD na wengine waliomaliza CO.

Mambo yaliyonishtua;

1. Hawajui Lugha ya kingereza.
Kuna kipindi nilifika Pale Mloganzila ambayo Kwa wasioijua ni sehemu ya Hospitali ya taifa ya Muhimbili ambayo kimsingi madaktari wake inatakiwa wawe vipanga na wenye uwezo Mkubwa.

Madaktari waliomafunzoni walinishtua Sana Kwa kingereza Chao kibovu kilichowafanya mara Kwa mara kucheka CHEKA Kwa aibu.

Sitaki kuzungumzia Ma-CO, ambao wengi wao nao kingereza kinawapiga chenga.

Kuna watu watasema, kingereza sio muhimu kwani ni lugha Kama lugha zingine.
Kumbuka materials nyingi za Taaluma ya Udaktari zipo katika Lugha ya kingereza, kutokujua kingereza kutamfanya Daktari kutokuwa mahiri.

2. Clinical officers wa Zama hizi wengi wao sio mahiri, hawako competent katika Taaluma Yao.

Nikikutana na wahitiu wa Diploma ya Clinical officer katika Stori nikiwasabahi nikawauliza mmoja mmoja aelezee concept ya Physiology, mwingine aelezee concept ya anatomy, na mwingine aelezee jinsi damu inavyozalishwa ndani ya Mwili WA mwanadamu.
Unajua hizo ni concept ndogo Sana ambazo hata mwanafunzi wa Kidato cha nne na sita wanaweza Kueleza.

Lakini wakaishia kubwabwaja.

Ukienda baadhi ya Hospitali, madaktari hawajui ku-take patient History, baadhi Yao wanakulazimishia vitu ambavyo havikuumi.

Na hapa nazungumzia madaktari Vijana. Unakuta kijana CV kubwa lakini uwezo unatia Shaka.

Hakuna kitu kinakera Kama uende Hospitalini alafu ukute Daktari anauwezo mdogo katika Fani yake, yaani ukimsikiliza unagundua kabisa hapa hamna kitu.

Ni Sawa na Mwanafunzi afundishwe na mwalimu kilaza, yaani inakera Sana.

Ushauri wangu, siku hizi ukienda Hospitalini kuwa Makini Sana, madaktari wa siku hizi sio wakuwaamini [emoji817] hasa hawa Vijana.

Serikali iangalie Kwa umakini hivi vyuo vya Kati ambavyo ongezeko lake limekuwa kubwa.

Kuna watu hawatanielewa.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Dar es salaam
Kwani si wanafanya mitihani mpk kupita? Lbd kama wengine wanapita kimangumashi, fikiria mitihani ya ma Co mwaka Jana imevuja hatujasikia ni hatua gani inechukuliwa Kwa walivujisha na ni Wakina nani walihusika, matokeo ni watoto wamepata adhabu ya kurudia mitihani, je Kwa mambo haya huoni tunatengeneza matokeo mabaya?? Nafikiria Kila 1 akitimiza muda wake hasa Walimu wakaingia darasani Kwa wakati na mitihani ikasimamiwa vzr na kazi zao za vitendo wodini zikasimamiwa Kwa uhodari ,hapo tutatoa madaktari wazuri sana.
 
Sio madaktari tu usiwaonee! Ni almost fani zote. Nchi hii kiingereza ni tatizo. Prof. Mkenda fanya kitu ila sina hakika kama ilani unayoitumikia inakuruhusu.
Kweli kbs wasiwaonee madaktari tu, hata Walimu na wengine kingereza ni tatizo.
 
Kama daktari anaweza kuokoa maisha kingereza kinasaidia nini?, Nenda China, urusi, Spain, uarabuni, uone Kama kuna mtu anahusudu kingereza.
Hivi hii dhana huwa mnaitoa wapi nyie akili fupi wa ccm? Huko China madaktari wanafundishwa kwa kiingereza? Urusi madaktari wanasoma kwa kiingereza au Kirusi? Vitabu vya udaktari Ufaransa ni vya kiingereza au kifaransa?
Tanzania kila kitu kuhusu udaktari ni English na Latin, wewe unaona siyo lazima mtu kuwa fluent kwenye lugha anayojifunzia wakati hakuna mitaala ya Kisukuma?
 
Kwani si wanafanya mitihani mpk kupita? Lbd kama wengine wanapita kimangumashi, fikiria mitihani ya ma Co mwaka Jana imevuja hatujasikia ni hatua gani inechukuliwa Kwa walivujisha na ni Wakina nani walihusika, matokeo ni watoto wamepata adhabu ya kurudia mitihani, je Kwa mambo haya huoni tunatengeneza matokeo mabaya?? Nafikiria Kila 1 akitimiza muda wake hasa Walimu wakaingia darasani Kwa wakati na mitihani ikasimamiwa vzr na kazi zao za vitendo wodini zikasimamiwa Kwa uhodari ,hapo tutatoa madaktari wazuri sana.
Ule mtihani ni majanga tu kwa mfano kati ya wana funzi 200 wanaweza kufaulu 25 tu, wengine hurudia na wizara na pamoja kupiga pesa tena ya mtihani yaani ni kama mradi fulani.... .uwezo wa mtoto wa form mwenye D4 kusomea udakitari, sio huyu mtoto hawezi kujisomea na kuelewa vitabu vya medicines
 
Hivi hii dhana huwa mnaitoa wapi nyie akili fupi wa ccm? Huko China madaktari wanafundishwa kwa kiingereza? Urusi madaktari wanasoma kwa kiingereza au Kirusi? Vitabu vya udaktari Ufaransa ni vya kiingereza au kifaransa?
Tanzania kila kitu kuhusu udaktari ni English na Latin, wewe unaona siyo lazima mtu kuwa fluent kwenye lugha anayojifunzia wakati hakuna mitaala ya Kisukuma?
Mitaala ni ya kingereza Kaka, hakuna kitabu cha medicine kimeandikwa kichina au kifaransa, vitabu vya medicine ni international. Kama unavijua leta ushahidi. Au tumia Google kusearch kitabu chochote cha medicine kilichoandikwa kiarabu
 
Inasikitisha sana...

Cha kusikitisha daktari kipanga hua very humble, ila daktari kilaza hua wakali sana bila sababu...
 
Na ndio maana nikakwambia wanajua lugha za kitabibu sio kingereza cha kuongea na hiyo ipo kwa wataalamu wengi too sio ma Dr. Peke yao hata engeneers na kada zingine

Tofautisha lugha ya mazungumzo na lugha ya kitaaluma ni vitu viwili tofauti kabisa
Kiingereza siyo medical terminology japo kwenye suala la lugha ya kufundishia ni kweli kuna tatzo na hii ni kuanzia huku chini kabisa suala la ubora wa wataalamu wa afya kuwa na uwezo mkubwa siyo kwamba nikusoma tu inatakiwa kuwepo na mazoezi ya vitendo ya kutosha, na semina za mara kwa mara ili kuwafanya kuwa na uwezo mkubwa
 
Hilo suala la kiingereza cha kuongea ni tatizo la mtu binafsi. Mtu anajisomea kujua ugonjwa wa mtu mpaka matibabu kwa lugha ya kiingereza lakini delivery kwa lugha ya kiingereza ikawa ngumu(kuongea).

Kutokujua lugha ya kuongea haimaanishi kuwa hautakuwa Mahiri.

Labda mtoa mada nkuulize ushawahi shuhudia wanafunzi wa udaktari wanavyokaziwa pindi wana"present case" kwa machief wao?
 
Mimi nasema bora hata hao watu wa afya ,kuna na tour guides wengi sana wanaongea broken hadi aibu
 
Shida wabongo mnajikuta wajuaji wa kila kitu kama hutaki kutibiwa na madaktari wasiojua kingereza baki nyumbani kwako ujitibie/utibie familia yako kwa kingereza.
Sasa hivi mna afya nzuri mnaongea upumbavu siku afya zenu zikiwabadilikia mnarudi kuwanyenyekea madaktari wasiojua kingereza
 
Back
Top Bottom