Nyanjilinji
Senior Member
- Oct 23, 2016
- 150
- 141
Hakuna shida kabisa Mkuu...Kama mshahara unaingia kweni kunashida gani?
Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hakuna shida kabisa Mkuu...Kama mshahara unaingia kweni kunashida gani?
Lakini wote walianza kwa kutokujua kitu ndio wakajua kwa hiyo hakuna hoja hapo.Sabato NJEMA!
Kuna madaktari waliotokea moja Kwa moja Kidato cha Sita kwenda kusoma MD, na wapo ambao wametokea Diploma(Clinical Officer, CO) kwenda kusomea MD.
Kiukweli nimeshtushwa mno baada ya kukutana na Baadhi ya Madaktari watarajiwa wasomao MD na wengine waliomaliza CO.
Mambo yaliyonishtua;
1. Hawajui Lugha ya kingereza.
Kuna kipindi nilifika Pale Mloganzila ambayo Kwa wasioijua ni sehemu ya Hospitali ya taifa ya Muhimbili ambayo kimsingi madaktari wake inatakiwa wawe vipanga na wenye uwezo Mkubwa.
Madaktari waliomafunzoni walinishtua Sana Kwa kingereza Chao kibovu kilichowafanya mara Kwa mara kucheka CHEKA Kwa aibu.
Sitaki kuzungumzia Ma-CO, ambao wengi wao nao kingereza kinawapiga chenga.
Kuna watu watasema, kingereza sio muhimu kwani ni lugha Kama lugha zingine.
Kumbuka materials nyingi za Taaluma ya Udaktari zipo katika Lugha ya kingereza, kutokujua kingereza kutamfanya Daktari kutokuwa mahiri.
2. Clinical officers wa Zama hizi wengi wao sio mahiri, hawako competent katika Taaluma Yao.
Nikikutana na wahitiu wa Diploma ya Clinical officer katika Stori nikiwasabahi nikawauliza mmoja mmoja aelezee concept ya Physiology, mwingine aelezee concept ya anatomy, na mwingine aelezee jinsi damu inavyozalishwa ndani ya Mwili WA mwanadamu.
Unajua hizo ni concept ndogo Sana ambazo hata mwanafunzi wa Kidato cha nne na sita wanaweza Kueleza.
Lakini wakaishia kubwabwaja.
Ukienda baadhi ya Hospitali, madaktari hawajui ku-take patient History, baadhi Yao wanakulazimishia vitu ambavyo havikuumi.
Na hapa nazungumzia madaktari Vijana. Unakuta kijana CV kubwa lakini uwezo unatia Shaka.
Hakuna kitu kinakera Kama uende Hospitalini alafu ukute Daktari anauwezo mdogo katika Fani yake, yaani ukimsikiliza unagundua kabisa hapa hamna kitu.
Ni Sawa na Mwanafunzi afundishwe na mwalimu kilaza, yaani inakera Sana.
Ushauri wangu, siku hizi ukienda Hospitalini kuwa Makini Sana, madaktari wa siku hizi sio wakuwaamini 💯 hasa hawa Vijana.
Serikali iangalie Kwa umakini hivi vyuo vya Kati ambavyo ongezeko lake limekuwa kubwa.
Kuna watu hawatanielewa.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Dar es salaam
Huu uzi ni wa madaktar najua madaktar mtaingia humu kuusoma ebu naomba madaktar leo mnisaidie kitu
Unaweza kuta mtu anaumwa na ugojwa wake kulingana na kitua cha afya alipo hawez kutibika anatokea daktar anamshauri mgojwa akatibiwe kwa mganga wa kienyeji hii inatokea sana yan unakuta daktar au nesi anamuita mgojwa au ndg ya mgojwa af anamshauri kumtoa mgojwa hospital akatibiwe kienyeji
2) kuna ili suala la uzazi wa mpango unakuta daktar au nesi anamshauri mtumiaji wa dawa za uzazi wa mpango anamwambia sio nzuri zinazala wakiwa pembeni ila wakiwa ofsin daktar anakushauri utumie sasa km ni mbaya kwa nn madaktar hamjazikataa sku zimeletwa
Mbona kigeugeu Kama popobawa?, Mara kiingereza mara kireno mara kispain. Tuchukue lipi tuache lipi?. Acha kulimbukia lugha za watu, kwani kiingereza ndiyo kinatibu?. Basi usiende hospitali za Kitanzania katibiwe Uingereza, Ureno au Spain. Ushamba tu unakusumbua.Na Mimi nakuambia Kwa uzoefu.
Ukiona moja Kati ya hao hawajui kingereza basi jua wanajua kihispania, kireno au kifaransa.
Zingatia; wengi wao sio wote
Juzi nilikua hospital, hao vijana wameshindwa choma/ weka ile kanule mara 3, anakuja huyu mara yule. Nilijaa sumu kwa mgonjwa wangu
Unalo sema ni kweli ila linaanzia uko chini, mimi binafsi paka leo na shanga mtoto alie maliza f4 na kupata D4 anawezaje kusoma udakitari CO, kwanza vile vitabu vya medicine hawezi kutoa concept hailewi kabisa. Kiingereza hiki cha kawaida cha kuongea ni shida, àtaweza je kusoma na kuelewa vitabu vikumbwa kama atonomiology, kwa kweli mimi naona ni usani kwenye hivyo vyuo vya kati...........
Tuboreshe mfumo wetu wa elimu from the scratch ambapo tuandae vijana wenye uwezo wa kuelewa na siyo Kukariri.Tufanyaje sasa?
Hii fani imevamiwa na makanjanja mkuu....hulifahamu hilo watakucheka watu😂😂😂
Mbona kigeugeu Kama popobawa?, Mara kiingereza mara kireno mara kispain. Tuchukue lipi tuache lipi?. Acha kulimbukia lugha za watu, kwani kiingereza ndiyo kinatibu?. Basi usiende hospitali za Kitanzania katibiwe Uingereza, Ureno au Spain. Ushamba tu unakusumbua.
Ishu hapo ni uwezo wao kutafsiri maandiko na vitabu vya kitaaluma katika Lugha zao.
Kutafsri nako usidhani ni kazi ndogo,
Nchi hizo na zingine zenye uwezo wa kutafsiri vitabu na majarida ya kitaaluma katika Lugha zao nyingi zipo vizuri Kama vile India.
Kwa muktadha wa Tanzania, machapisho, vitabu na majarida mengi Kam sio yote yapo Kwa lugha ya kingereza na ndio lugha ya kujifunzia, sasa mtu Kama hawezi kingereza unafikiri atakuwa mahiri wa Taaluma husika aliyofundishiwa Kwa lugha asiyoimudu?
Ni Sawa na Malenga wa ushairi wa Kiswahili asiyeimudu lugha ya kiswahili alafu awe mahiri katika Mashairi na Riwaya za Kiswahili.
Ndio maana washairi wengi WA lugha ya Kiswahili wametoka Pwani ya Afrika mashariki Kwa sababu wanamudu Lugha ya Kiswahili.
Huo ni mfano tuu.
Kama Udaktari ungekuwa unafundishwa Kwa lugha ya Kiswahili na vitabu vyake vingi vipo katika Lugha yetu basi ningeungana na wewe
Kama mtu ni PhD holder anasema taki fosi( task force) unadhani hao form 6 mkuu watakuwaje?Sabato NJEMA!
Kuna madaktari waliotokea moja Kwa moja Kidato cha Sita kwenda kusoma MD, na wapo ambao wametokea Diploma(Clinical Officer, CO) kwenda kusomea MD.
Kiukweli nimeshtushwa mno baada ya kukutana na Baadhi ya Madaktari watarajiwa wasomao MD na wengine waliomaliza CO.
Mambo yaliyonishtua;
1. Hawajui Lugha ya kingereza.
Kuna kipindi nilifika Pale Mloganzila ambayo Kwa wasioijua ni sehemu ya Hospitali ya taifa ya Muhimbili ambayo kimsingi madaktari wake inatakiwa wawe vipanga na wenye uwezo Mkubwa.
Madaktari waliomafunzoni walinishtua Sana Kwa kingereza Chao kibovu kilichowafanya mara Kwa mara kucheka CHEKA Kwa aibu.
Sitaki kuzungumzia Ma-CO, ambao wengi wao nao kingereza kinawapiga chenga.
Kuna watu watasema, kingereza sio muhimu kwani ni lugha Kama lugha zingine.
Kumbuka materials nyingi za Taaluma ya Udaktari zipo katika Lugha ya kingereza, kutokujua kingereza kutamfanya Daktari kutokuwa mahiri.
2. Clinical officers wa Zama hizi wengi wao sio mahiri, hawako competent katika Taaluma Yao.
Nikikutana na wahitiu wa Diploma ya Clinical officer katika Stori nikiwasabahi nikawauliza mmoja mmoja aelezee concept ya Physiology, mwingine aelezee concept ya anatomy, na mwingine aelezee jinsi damu inavyozalishwa ndani ya Mwili WA mwanadamu.
Unajua hizo ni concept ndogo Sana ambazo hata mwanafunzi wa Kidato cha nne na sita wanaweza Kueleza.
Lakini wakaishia kubwabwaja.
Ukienda baadhi ya Hospitali, madaktari hawajui ku-take patient History, baadhi Yao wanakulazimishia vitu ambavyo havikuumi.
Na hapa nazungumzia madaktari Vijana. Unakuta kijana CV kubwa lakini uwezo unatia Shaka.
Hakuna kitu kinakera Kama uende Hospitalini alafu ukute Daktari anauwezo mdogo katika Fani yake, yaani ukimsikiliza unagundua kabisa hapa hamna kitu.
Ni Sawa na Mwanafunzi afundishwe na mwalimu kilaza, yaani inakera Sana.
Ushauri wangu, siku hizi ukienda Hospitalini kuwa Makini Sana, madaktari wa siku hizi sio wakuwaamini 💯 hasa hawa Vijana.
Serikali iangalie Kwa umakini hivi vyuo vya Kati ambavyo ongezeko lake limekuwa kubwa.
Kuna watu hawatanielewa.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Dar es salaam
Hao madaktari hawajui Kuandika Kiingereza,Kusoma Kiingereza au Kuzungumza Kiingereza?. Kuwa specific tafadhali. Lipi hapo?Materials za Taaluma ya Udaktari nyingi zipo Kwa lugha ya kingereza.
Na kutokana na mabadiliko ya magonjwa na madawa Udaktari kila siku unahitaji ku-update.
Huwezi kuwa Daktari mahiri bila kujua Lugha ya kingereza
Hata jiwe kwake kilikuwa kigumu kukielewa japo cha kibongo bongo kipooooooooooo!!!!!!!!Kuhusu Kiingereza, hilo ni janga la kitaifa [endapo kama unaithamini lugha hiyo].
Kiingereza hicho kibovu unachodai, kinaakisi uwezo wa Watanzania walio wengi.
Watanzania walio wengi lugha hiyo inawapiga chenga.
Hivyo hamna cha ajabu hapo. Watanzania kuongea Kiingereza kibovu ni jambo la kawaida sana.
Si ajabu hata wewe mwenyewe huongei Kiingereza kizuri kilichonyooka.
Just sayin’.
Ushaambiwa material zetu za udaktari zimeandikwa kwa kiingereza, hao unaowataja wanavitabu vyao vilivyoandikwa kwa lugha zao, elewa basi.Kama daktari anaweza kuokoa maisha kingereza kinasaidia nini?, Nenda China, urusi, Spain, uarabuni, uone Kama kuna mtu anahusudu kingereza.
Sijawahi kuona watu wanaongea kiingereza kibovu tena kwa lafudhi mbovu kama waGandaKama muda karibu wote unaongea Kiswahili (98%), Kiingereza 1%,halafu utegemee uongee English safi kama mganda itakuwa ndoto za mchana, au utegemee mtu anayeishi mjini ambaye muda wote anazungumza Kiswahili hawezi kuongea kilugha kilichonyooka kama mtu wa kijijini, lugha ni kuifanyia mazoezi haipimi kiwango cha elimu
Mi nadhani mother tongue ndio inaathiri kiiingereza cha mtu!sio kila mtu anaweza kuongea pure english mf.kenyans kile sio kiiingereza bali ni lugha zao za asili the same to Nigerians!!!mfano A sukuma can't speak like an englishman!mi nadhani swala la kiiingereza ni pana Sana kuliko tunavofikiri!!halafu kiiingereza cha kuongea mtu sio sawa na cha kuandika wala cha kuelewa maana halisi ya maneno yenyewe!!inaweza ukawa mzuri kwenye kuandika na kuelewa lakini lafudhi ikawa sio!!!Materials za Taaluma ya Udaktari nyingi zipo Kwa lugha ya kingereza.
Na kutokana na mabadiliko ya magonjwa na madawa Udaktari kila siku unahitaji ku-update.
Huwezi kuwa Daktari mahiri bila kujua Lugha ya kingereza