Kwa hawa Madaktari huko mbeleni tutapata tabu

Kwa hawa Madaktari huko mbeleni tutapata tabu

Mbona Mtoa Mada ameweka kila kitu wazi kabisa? sijui kwanini watu wana vichwa vigumu kuelewa... Ngoja nimsaidie

Kwa nchi yetu.. Tanzania, English ndo lugha inayotumika kufundisha, vitabu vyote vipo katika lugha hii, machapisho n.k hivyo kitendo cha kukutana na mtu anaejiita mtaalamu katika fani fulani (Daktari) halafu english inampiga chenga kiukweli kabisa ni swala la kujiuliza na mara nyingi huwa amefika hatua hio kwa kukariri = sio daktari mzuri. Unaongea na daktari hawezi hata kuwasilisha taarifa kwa Kingereza halafu unaamini kabisa kasoma molecular structure akaielewa?? [emoji23][emoji23]

Mataifa yaliyoendelea yana mifumo ya kutafsiri vitabu na machapisho kwa lugha zao. hata waandishi wanaandika kwa lugha zao. Urusi mfano hata "Google" haipo.. wana system zao, china hamna whatsApp n.k nimetaja hivi kuonesha namna walivyo independent.
Kujua contents za udaktari na kuongea fluent english ni vitu viwili tofauti, unaweza ukasoma vitu vilivyoandikwa kwa kiingereza na ukavielewa vzuri sana lakini ukiambiwa jielezee kwa english ukawa unachapia, mfano daktari wa meno amesoma root canal treatment na akajua vizuri kuperform hiyo huduma na kila mgonjwa akasifia huduma yake lakini ukimwambia aongee kiingereza anaungaunga, pia kuna watu wanaongea english safi lakini ukiwaleta kwenye taaluma zao ni majanga
 
Udhaifu wa kitaaluma upo kwenye kada zote sio kwa madaktari tu,japo kwenye Afya kufanya kitu bila kua na uhakika ni hatari kwa kua wana deal na maisha ya watu,...nakubaliana na mtoa uzi changamoto zipo lakini sio kubwa kama inavyosemwa,hata kwenye taaluma ya mtoa uzi sio wote wako smart.
 
Kama daktari anaweza kuokoa maisha kingereza kinasaidia nini?, Nenda China, urusi, Spain, uarabuni, uone Kama kuna mtu anahusudu kingereza.
Hao uliowataja hawakusomea huo udakatari na wala hawatibu kwa kiingereza. Sisi tumekubali madaktari wetu wasomeshwe na kutibu kwa lugha hio. Sasa kama lugha tu yenyewe inampiga chenga, lazima tutilie mashaka anachokijua
 
Anazaliwa anaongea kilugha, kiswahili anajifunza mtaani na shuleni , akifika secondary Anaanza kujifunzakwa lugha ya kiingereza. Then unataka awe fluent? Nitamlaumu kama hatakuwa fluent kwenye lugha yake mama.

Wataalamu wenu wengi wako competent isipokuwa kuna changamoto imeibuka miaka ya hivi karibuni biashara Vs taaluma .
Chuo ni private utaruhusu wanafunzi wako 20% wadisco ? utaendeshaje chuo?

Wazazi nao wanafurahi mtoto an D3 anaenda kuwa tabibu? sasa ukikutana naye After 3 years unaanza kulia lia.

Let go back to basics, tujifunze kwa kiswahili level zote , Au tujifunze kwa kingereza level zote

kiswahili hatutakisahau kwa sababu kinaongelewa mtaani.
 
Class mate wangu alikuwa na div 4.28, ala akaunga kibishi(kuhonga) akapata diploma Safi ya nursing na mwaka wa 3 kutoka alipohitim kidato cha 4 alikuja nikampeleka wizarani sijui wanasema kujisajiri na next 4 weeks akawa tayari kuripoti kibaruani mji wa katikati ya nchi.
Mwingine nimekutana nae mtaani tu anauza duka la dawa Ila anayo sijui wanaita ADO (naweza kusahihishwa), Ila akawa hajui kiingereza (maelekezo)rahisi ya kuunganisha simu janja mpya ianze kutumika.
Mwaka juzi nilikuwa mkoa mmoja wa baridi(nyanda za juu) nikawa najisikia siko poa. Kichwa kuuma, viungo kuuma, mwili kuchoka, kukosa hamu ya kula, n.k. nikaenda hospital moja kubwa tu inamilikiwa na wahindi japo wahudum wengi ni waswahili wenzetu. Kumuona Dr akanipa list ya vipimo niende lab. Kuna baadhi ya maswali yake yalinifanya nikose Imani nae kidogo, nikapima vipimo kibao(ilinigharimu Kama 57k) Ila simuonekana na tatizo lolote. Nikaenda hospital nyingine nikapata vipimo 3 tu tatizo likaonekana.
Kwa ufupi, mada yako iko sahihi 100%.
 
Taikon bana wewe unashangaa tu madaktari hawajui kiingereza wakati hadi tulipata Rais hakijui.
 
Hyo kazi ya kutafasiri kingereza[emoji3591] kiswahili [emoji3591] kingereza tena, ni ngumu sana hujui tu
 
Yaani Mimi pia Ni mmoja wa watu ninaosikitishwa Sana na wimbi la ongezeko la hutu tu vyuo twa afya,Kuna failures wakutosha humo,nilienda hospital na mtoto kipimo kikataka atolewe damu ya mshipa imagine mtu hawezi,kamchoma Mara ya kwanza kachokonoa kashindwa,kabadili sindano kachokonoa kashindwa,eti anataka kuchukua ya tatu, Aiseeee nilikuwa mbogo..namuuliza wewe huyu mwanangu ndio wa majaribio au vipi?nilikiamsha Hadi alikuja mtu mwingine kummalizia zoezi.....tangu siku hiyo Kama ulivyoshauri Niko selective Sana kwa watoa huduma.
Private hosp nyingi wanaokoteza watu wenye elimu kidogo ..wanataka Cheap labor..
Hawataki kuchukua maMD wanaoeleweka kwa kuogopa gharama.
 
Kama daktari anaweza kuokoa maisha kingereza kinasaidia nini?, Nenda China, urusi, Spain, uarabuni, uone Kama kuna mtu anahusudu kingereza.
Kingereza kwa Tanzania kwa daktari ni lazima kwasababu ndyo lugha inayotumiwa kumpatia hayo maarifa ya udaktari pia ndyo lugha inayotumika kwenye medical instructions zao, kwenye madawa, kwenye vitabu vyao vya miongozo ya kutoa dawa mbalimbali kulingana na ugonjwa husika. Kwahiyo hakuna excuse ya kutokujua Kingereza. Hizo nchi unazitaja wanatumia lugha zao since wakiwa shuleni kupata hayo maarifa ya udaktari na kazini ndyo lugha inayotumika.

Sent from my TECNO KB8 using JamiiForums mobile app
 
Sabato NJEMA!

Kuna madaktari waliotokea moja Kwa moja Kidato cha Sita kwenda kusoma MD, na wapo ambao wametokea Diploma(Clinical Officer, CO) kwenda kusomea MD.

Kiukweli nimeshtushwa mno baada ya kukutana na Baadhi ya Madaktari watarajiwa wasomao MD na wengine waliomaliza CO.

Mambo yaliyonishtua;

1. Hawajui Lugha ya kingereza.
Kuna kipindi nilifika Pale Mloganzila ambayo Kwa wasioijua ni sehemu ya Hospitali ya taifa ya Muhimbili ambayo kimsingi madaktari wake inatakiwa wawe vipanga na wenye uwezo Mkubwa.

Madaktari waliomafunzoni walinishtua Sana Kwa kingereza Chao kibovu kilichowafanya mara Kwa mara kucheka CHEKA Kwa aibu.

Sitaki kuzungumzia Ma-CO, ambao wengi wao nao kingereza kinawapiga chenga.

Kuna watu watasema, kingereza sio muhimu kwani ni lugha Kama lugha zingine.
Kumbuka materials nyingi za Taaluma ya Udaktari zipo katika Lugha ya kingereza, kutokujua kingereza kutamfanya Daktari kutokuwa mahiri.


2. Clinical officers wa Zama hizi wengi wao sio mahiri, hawako competent katika Taaluma Yao.

Nikikutana na wahitiu wa Diploma ya Clinical officer katika Stori nikiwasabahi nikawauliza mmoja mmoja aelezee concept ya Physiology, mwingine aelezee concept ya anatomy, na mwingine aelezee jinsi damu inavyozalishwa ndani ya Mwili WA mwanadamu.
Unajua hizo ni concept ndogo Sana ambazo hata mwanafunzi wa Kidato cha nne na sita wanaweza Kueleza.

Lakini wakaishia kubwabwaja.


Ukienda baadhi ya Hospitali, madaktari hawajui ku-take patient History, baadhi Yao wanakulazimishia vitu ambavyo havikuumi.

Na hapa nazungumzia madaktari Vijana. Unakuta kijana CV kubwa lakini uwezo unatia Shaka.

Hakuna kitu kinakera Kama uende Hospitalini alafu ukute Daktari anauwezo mdogo katika Fani yake, yaani ukimsikiliza unagundua kabisa hapa hamna kitu.

Ni Sawa na Mwanafunzi afundishwe na mwalimu kilaza, yaani inakera Sana.

Ushauri wangu, siku hizi ukienda Hospitalini kuwa Makini Sana, madaktari wa siku hizi sio wakuwaamini 💯 hasa hawa Vijana.

Serikali iangalie Kwa umakini hivi vyuo vya Kati ambavyo ongezeko lake limekuwa kubwa.

Kuna watu hawatanielewa.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Dar es salaam
TATIZO UTAALAMU WA TIBA, AU KIINGEREZA?, KIINGEREZA SIO ISSUE, ISSUE IPO KWENYE UTAALAMU WAO,MLOGANZILA NI HOSPITALI SAFI KABISA HUDUMA ZAKE NI NZURI KABISA, HAKUNA TATIZO LOLOTE E PALE.
 
Back
Top Bottom