R-K-O
JF-Expert Member
- Jun 27, 2023
- 482
- 2,178
MKASA WA BINTI MKRISTO ALIEBADILI DINI:
Nimeshawahi kushuhudia mvurugano wa hali juu kwa suala hili kutoka kwa familia za wanandoa, Bint wa kimakonde Mkristo alikubaliwa na wazazi wake abadili Dini ili aolewe na kijana Muislam, Shida ikaja pale bint alipofariki, ndugu za mume wanataka kumzika yule bint kwakufuata taratibu za kiislam kwasababu mauti yamemfika akiwa Muislam, Baba na mama wa yule bint hawakuleta shida ila ndugu zao (wanafamilia)wakakataa kabisa na walikuwa tayari kususia msiba iwapo atazikwa Kiislam.
Baba na mama wa yule bint hawakuwa tayari kutengana na ndugu zao (wanafamilia Wakristo)sasa afanyeje ili aweze kushirikiana na nduguze wakristo kumzika bint yake!?
Alichofanya yule baba ni kuwakabili ndugu wa mume wa mwanae ambao ni waislam na kuwaeleza waziwazi kwamba haitawezekana mwanangu kuzikwa kwa taratibu za kiislam kwahiyo basi yule Ustadh aliemsilimisha mwanae aende akamsilimue wamzike!
Hili kauli aliitoa kwa lafudhi yake ya Kimakonde"Alienchilimicha mwanangu aje anchilimue tunnjike" Waislam wakakataa kwasababu suala la Dini mwenye mamlaka yakuchagua ni muhusika mwenyewe ambae ameshafariki na amefariki akiwa Muislam.
Hatimae maiti haikuzikwa na kesi ikapelekwa Mahakamani.
..................................................................................
Sisemi kwamba watu wasibadili dini bali wakae na kutulia kabla ya kuchukua uamuzi huo,
Nimekuwa nikiona mara kadhaa familia / ndugu wanaingia migogoro na makanisa / misikiti ya kuwania maiti ya mtu aliebadili dini, inafikia mpaka kufikishana mahakamani ama maiti kufukuliwa kabisa kuzikwa kwengine, kuna muda hugeuka vita kabisa, Ningependa hapa tupeane elimu zaidi
Siku ikitokea aliebadili dini kafariki, hii inaathiri vipi mazishi hasa kwa wanafamilia na ndugu ?
1. Kutakuwa na vurugu za kugombania maiti kati ya wanafamilia/ndugu dhidi ya kanisa / msikiti ?
2. Maiti itazikwa kwa misingi ya dini ipi
3. Urithi ?
4. Washiriki katika misiba wanawake wataruhusiwa endapo akizikwa kiislam?
5. Atazikwa kwa sanda ama jeneza
6. Shughulu nyingine je?

- Mkristo kabadili dini kuwa muislamu huku ndugu na wanafamilia ni waisalam (Mfano mchezaji wa Yanga Mzize)
- Muislamu kabadili dini kuwa mkristo huku ndugu na wanafamilia ni waisalam