Kwa hawa watu wanaobadili dini, Ndugu na wanafamilia wa dini tofauti wajiandae kwa lipi kwenye mazishi yao?

Nimeshawahi kushuhudia mvurugano wa hali juu kwa suala hili kutoka kwa familia za wanandoa,
Bint wa kimakonde Mkristo alikubaliwa na wazazi wake abadili Dini ili aolewe na kijana Muislam,
Shida ikaja pale bint alipofariki, ndugu za mume wanataka kumzika yule bint kwakufuata taratibu za kiislam kwasababu mauti yamemfika akiwa Muislam,
Baba na mama wa yule bint hawakuleta shida ila ndugu zao (wanafamilia)wakakataa kabisa na walikuwa tayari kususia msiba iwapo atazikwa Kiislam.
Baba na mama wa yule bint hawakuwa tayari kutengana na ndugu zao (wanafamilia Wakristo)sasa afanyeje ili aweze kushirikiana na nduguze wakristo kumzika bint yake!?
Alichofanya yule baba ni kuwakabili ndugu wa mume wa mwanae ambao ni waislam na kuwaeleza waziwazi kwamba haitawezekana mwanangu kuzikwa kwa taratibu za kiislam kwahiyo basi yule Ustadh aliemsilimisha mwanae aende akamsilimue wamzike!
Hili kauli aliitoa kwa lafudhi yake ya Kimakonde"Alienchilimicha mwanangu aje anchilimue tunnjike"
Waislam wakakataa kwasababu suala la Dini mwenye mamlaka yakuchagua ni muhusika mwenyewe ambae ameshafariki na amefariki akiwa Muislam.
Hatimae maiti haikuzikwa na kesi ikapelekwa Mahakamani.
 
Asante kwa mchango

Nimeiweka kwenye post ya kwanza hii
 
Dini ya kweli?
Naamini katika kuishi na watu vizuri
Kutoa misaada Kwa wajane,yatima na wenye uhitaji.
Hiyo kwangu ni Dini
Maana nikitoa pale palipo na uhitaji mi hufarijika sana moyoni mwangu .
Ubarikiwe zaidi mkuu
 
unapobadil dini fikiria na future consequences
 
Mbaya zaidi anaefanya watu waende mahakamani hana analolijua. Keshafanya yake akiwa hai anaachia msala wenzie baada ya mauti.
na inakuwa vuta nikuvute si mchezo

baba na mama wanaweza kuruhusu azikwe kwa dini aliyobadili ila mtiti unaanza pale ndugu hawataki, wazazi nao inakuwa ngumu kupuuza msimamo wa ndugu
 
Cha muhimu ni watu kuheshimu maamuzi ya mhusika.
Pili kubadili dini kuwekwe hadharani, isiwe siri ya familia tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…