Kwa hesabu hizi Yanga SC anamzidi Simba SC kimapato mikataba wa Jezi

demigod

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Posts
8,292
Reaction score
15,250
SIMBA SC:

Tarehe 20.03.2023 Simba SC waliingia mkataba na VUNJABEI wenye thamani ya Bilioni 2 tu kwa muda wa Miaka miwili (Yaani Misimu Miwili)

VUNJABEI alitengeneza jezi kwa misimu miwili yaani
2021/22 na
2022/23

Katika kipindi hiko cha misimu miwili Simba wataingiza Bilioni 2 Tu.

Tarehe 16/6/2023 Simba SC waliingia mkataba na SANDALAND wenye thamani ya Bilioni 4 tu kwa muda wa Miaka miwili (Yaani Misimu Miwili). Ikimaanisha kila msimu wataingiza Bilioni 2

SANDALAND atatengeneza jezi kwa misimu miwili yaani
2023/24 na
2024/25

Katika kipindi hiko cha misimu miwili Simba wataingiza Bilioni 4 Tu.

HIVYO BASI SIMBA WATAINGIZA JUMLA YA BILIONI 6 KATIKA MISIMU 4.

YANGA SC:
Tarehe 12/02022 YANGA SC waliingia mkataba na GSM wenye Jumla ya thamani ya Bilioni 10.9 tu kwa muda wa Miaka mitano (Yaani Misimu mitano)

Kwa maana ya msimu wa:-

2022/23, 2023/24, 2024/25, 2025/26, 2026/27.

Kwa hesabu ya haraka haraka Bilion 10.9 ukiigawa kwa kila msimu unapata Bilion 2.18. Hivyo ulichukua misimu minne tu ya kwanza yaani

2022/23,
2023/24,
2024/25,
2025/26,

Ni sawa na 2.18 Bilioni X 4 = Bilioni 8.72. Kimsingi kwenye misimu minne tu ya mikataba ya jezi kwa upande wa Simba & Yanga,

Yanga SC wanatengeneza Bilion 8.72

Simba SC wanatengeneza Bilion 6.00.

YANGA SC WAMEWAZIDI BILIONI 2.72 WENZAO KWENYE DILI LA JEZI.

HAPO HATUJAHESABIA ILE 1,300/= YA KWENYE MAUZO YA KILA JEZI YA KLABU KUTOKA KWA GSM.

View attachment 2669392
 
Tunajua kwenye kila mauzo ya jezi Yanga anachukua 1,300.

Yani buku moja na mia mia tatu

Au jero jero mbili na mia mia tatu

Mia mbili hamsini nne na mia mia tatu

Sawa na mia mia 13

Ambapo kwa hamsini hamsini ni sawa na 26.

Hiyo ndio hela ambayo Yanga anachukua.
 
Aaahaaaa
 
Kwenye soka la bongo ninachopenda ni ujinga wa mashabiki yaani hakuna mwenye afadhali sio simba wala yanga. Endeleeni kutufurahisha wadau
 
Nje na mkataba na SANDALAND

Simba ana ingiza kiasi gani kingine tofauti na Bilion 4.
 
Homa lako likiisha rudia hotuba ya juzi kwenye mkutano mkuu wa utopolo kuwa mauzo ya jezi kwa mwaka mzima ni Tsh milioni 300 tu
Klabu inanunua jezi kutoka kwa GSM na kuziweka kwwenye maduka rasmi ya Klabu.

Hivyo basi mwisho wa msimu Duka rasmi la klabu lililoko HQ nalo lina make profit.

300 ni faida ya hilo duka.
 
Nje na mkataba na SANDALAND

Simba ana ingiza kiasi gani kingine tofauti na Bilion 4.
Simba haihitaji mauzo ya jezi ili apate hela.

Simba inachukua pesa cash baada ya hapo mzabuni ndio atajua anauzaje ili apate faida.

Incase mauzo yakaenda hovyo kutokana na changamoto zozote, mzabuni ndio atakuwa na loss.
 
Kamlipeni Luc E....kabla mambo hayajawa mabaya. ...
Si mnahela?
Milion 150 ni pesa ndogo sana.

Tunataka tumtese kwa kumlaza na njaa kwanza mpaka siku ya payment deadline ndipo tutamlipa.

Tunamtesa kwakuwa aliwaita watu weusi MANYANI.
 
Simba haihitaji mauzo ya jezi ili apate hela.

Simba inachukua pesa cash baada ya hapo mzabuni ndio atajua anauzaje ili apate faida.

Incase mauzo yakaenda hovyo kutokana na changamoto zozote, mzabuni ndio atakuwa na loss.

Kwa hiyo hata 1300 ya mauzo ya jezi (nje ya mkataba wa utengenezaji jezi) nyinyi hamuitaki?
 
Milion 150 ni pesa ndogo sana.

Tunataka tumtese kwa kumlaza na njaa kwanza mpaka siku ya payment deadline ndipo tutamlipa.

Tunamtesa kwakuwa aliwaita watu weusi MANYANI.
Hakuita watu weusi Manyani. Kamsikilize vizuri. Alikuwa specific kabisa. Usimlishe maneno.
 
Kwa hiyo hata 1300 ya mauzo ya jezi (nje ya mkataba wa utengenezaji jezi) nyinyi hamuitaki?
Yanini sasa?

Juzi mmesema mmepata 300M ina maana kwa 1,300 hiyo ni sawa na jumla ya mauzo ya jezi around 250K

Hivi unajua kwa 1,300 ili wewe uifikie 2B unatakiwa uuze jezi ngapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…