Kwa hesabu za haraka, Stiegler's Gorge itaifanya Tanzania kuipiku Afrika Kusini kiuchumi ndani ya miaka 10

Gasi ya mtwara tayari imechimbwa na ipo ktk matumizi mkuu! Kinachotusumbua ni kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja, gasi ina zaidi ya miaka 2 tangu ifike Dar, unatumia kuzalisha umeme na Tanesco huko Kinyerezi, ubungo, na Tegeta. Bado matumizi ya gasi hii ya Mtwara ni kidogo sana.
 
kwani TANZANIA tumeanza kufanya mining ya uranium ? sorry sikujua naomba uniambie ni mgodi gani tunakochimba uranium?
 
Hiyo gesi inayotumika kuzalisha umeme kinyerezi na ubungo ni ya Songosongo iligunduliwa miaka ya 1970 na imeanza kutumika hivi karibuni tu, hiyo gesi ya Msimbati iliyogunduliwa mwaka 2010 uzalishaji bado sana
 
Unafikiri sauzi afrika ilijengwa kwa miaka10??
Wee sikiza story za vijiweni thn ziweke akilini alafu impact yake utakuja kuiona baadae...
Sauz iko mbali wewe...
 
Kuna haja ya kufahamishwa, kama tuliyonayo haiwezi kuzalisha umeme kwa kiwango tunachohitaji?
Mtwara, kampuni ya ARTUMAS, ilifua umeme kwa kutumia gesi, hata SONGAS, anafua umeme kwa kutumia gesi.
Naamini matumizi ya gesi ingekuwa ni rahisi kutumika, bila kuharibu mazingira.
Masuala ya kutumia maji ya maporomoko ya mabwawa,yamekuwa na zile habari za kutegemea mvua,mara matope yamejaa.!
Ulinganifu ukifanyika, tuokoa gharama, tunafahamu Ethiopia anajenga bwawa kubwa kwa ajili ya kuzalisha umeme, labda kwa vile hana gesi.
Sisi tuongeze jenereta zenye uwezo wa kuzalisha MEGAWATI nyingi pale KINYEREZI,tuokoe gharama.
 
Ulipwe hewa? Wanakuogopa?
 
Tunaweza kuipiku south afriaca ki uchumi ya kweli hayo? Mtu anazitengeneza gar sisi hata sindano bado mkuu bado sana
Hii kweli kaongeza chumvi exaggeration ya hali ya juu.
Note: Mimi diehard shabiki wa Magufuli.
 
Kwa hesabu za papuchi sawa
 
wooi ngachoka kabisa..πŸ™„πŸ™„πŸ˜³
 
Imeanza tangu 2005... Tatizo mnawaamini saba wana siasa badala ya wataalamu wa mambo hayo
 
Pia tuliwahi kuambiwa gesi ya Mtwara ingetufanya Tz kuwa bora kiuchumi kuliko Kenya, Namibia, South Africa, Botswana, Misri na Ghana. Sijui ile gesi iliishia wapi?
 
Pia tuliwahi kuambiwa gesi ya Mtwara ingetufanya Tz kuwa bora kiuchumi kuliko Kenya, Namibia, South Africa, Botswana, Misri na Ghana. Sijui ile gesi iliishia wapi?
Tofautisha ya Songosongo (onshore) na ya Mtwara (offshore)
 
Kuna ukweli kuwa tutapiga hatua,Ila tujiulize tunafanya nini kuzuia hujumaa,au ndio tuko kwenye usingizi kuwa Kila mtu anapenda hizo juhudi zetu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…