sinza pazuri
JF-Expert Member
- Aug 16, 2014
- 3,704
- 9,932
Leo nilipita mitandaoni nikakutana na comment ya mtu mmoja, nadhani ni watoto walioanza kufatilia mpira juzi. Alikuwa anauliza, "Huyu Mzee Leakey ni nani?" Hakuwa anamfahamu.
Kilichonivutia si swali lake, bali sababu iliyomfanya atake kumjua. Alisema amevutiwa na uwezo wa Dr. Leakey kuuchambua mpira kwa kina lakini kwa lugha nyepesi sana kiasi kila mtu anaelewa.
Sisemi wachambuzi wa sasa hawafanyi vizuri. Wapo wengi wanaojitahidi kama Kumwembe, Ambangile, Nazir Khalifan, Mbwaduke na wengine.
Lakini Dr. Leakey ana kitu tofauti.
Yeye hachambui matukio ya mechi tu. Anaelezea historia, mbinu, tamaduni za mpira na mazingira yanayoufanya mchezo huu uwe wa kuvutia zaidi.
Kwa mtazamo wangu, Dr. Leakey ameshavuka kiwango cha "mchambuzi". Yeye ni storyteller wa mpira.
Katika dunia ya leo ya uchambuzi wa soka, mchambuzi bora anatakiwa awe na macho ya kuona mfumo wa timu, afafanue mambo magumu kwa lugha rahisi, awe neutral dhidi ya ushabiki, aelewe data za kisasa, ajue mbinu za makocha na pia aelewe saikolojia ya mchezo.
Ukimsikiliza Leakey, utaona mengi ya hayo yapo ndani yake bila kujilazimisha.
Ndiyo maana nina ombi moja tu:
Dr. Leakey, anzisha podcast yako.
YouTube, Spotify, Apple Podcasts au popote. Nina uhakika watu wengi tutafuatilia.
Tusije tukaendelea kukuona wakati wa World Cup pekee, halafu maarifa yako yabaki simulizi za mdomoni bila kurekodiwa.
Madini kama haya yanahitaji kuhifadhiwa ili yawe rejea kwa vizazi vijavyo.
Mimi binafsi napenda kutazama podcast kama The Rest Is Football na Stick to Football kwa sababu zina-connect experience, uchambuzi na simulizi. Package fulani amazing.
Bado sijapata podcast ya Kiswahili inayojikita strictly kwenye football kwa kiwango hicho.
Dr. Leakey, hili si suala la kushindana na vijana.
Ni suala la kuacha urithi.
Mpira wa Tanzania unahitaji maarifa yako yaendelee kuishi hata baada ya camera za World Cup.