Kwa heshima na taadhima, nawaomba CCM 2025 mtuletee Mgombea bora mwenye uchungu na nchi hii

Kwa heshima na taadhima, nawaomba CCM 2025 mtuletee Mgombea bora mwenye uchungu na nchi hii

ngebe

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2020
Posts
1,789
Reaction score
5,117
Baada ya kuona kabisa kwamba tuko kwenye uelekeo ambao hauna dira, napemda kutoa Rai kwa Chama cha Mapinduzi 2025 mtuletee mgombea Urais mwenye dira maono na mwenye uchungu na Rasilimali za nchi hii.

Hatuhitaji mtuletee mtu ambaye kutwa kucha anawaza uchaguzi na jinsi ya kuendelea kuwa Rais badala ya kuwaza maendeleo ya watanzania,

Hatuhitaji mtu amabye yuko radhi kuwaruhusu watu wafanye ufisadi ili wampe sapoti aendelee kuwa Rais hatutaki!

Lakini pia mimi kama mwananchi wa kawaida mwenye uhuru wa kutoa maoni katika nchi hii, ninapenda kumueleza Rais Samia kwamba Sisi tunampemda na tunamuheshimu sana, aendelee kuchapa kazi kwa kipindi hiki kilichobaki lakini chonde chonde 2025 aamue tu kwa hiyari yake kutogombea tena nafasi ya Urais ili kulinda heshima yake.

Asanteni sana
 
9C73A329-9616-40BB-AD4C-9E710F51B780.jpeg
 
Makonda au Sabaya? Maana nyie wafuasi wa Magufuli hawa wahalifu ndio mnawatetea kwa nguvu zote kuwa ni wazalendo, licha ya ushahidi mwingi wa wazi kutolewa dhidi ya Uhalifu wao

Samia ana mapungufu yake, lakini hana uchungu na nchi? kuwa uchungu na nchi ndio kutufugia wahalifu na kufanya mauaji ya wakosoaji wako?

Unasema Samia anawaza kila mara uchaguzi wakati, kipindi cha Magufuli ndio tulikuwa tunafanya uchaguzi kila mwezi kisa kuhonga na kutishia wapinzani wamuunge mkono?

nani aliyekuwa na siasa chafu kati ya Magufuli na Samia?
 
Mwenye uchungu na nchi hii ni wale walio shuhudia utawala wa Ally Hassan Mwinyi, (Rais wa awamu ya pili) jina linalofanana na Samia Suluhu Hassani.
 
Mgombea yupi wakati aliyepo ametoa ajira za miaka 9 kuendelea kumletea yeye kama rais, maoni ya watu kuhusu katiba mpya?
 
Makonda au Sabaya? maana nyie wafuasi wa Magufuli hawa wahalifu ndio mnawatetea kwa nguvu zote kuwa ni wazalendo, licha ya ushahidi mwingi wa wazi kutolewa dhidi ya Uhalifu wao
Samia ana mapungufu yake, lakini hana uchungu na nchi? kuwa uchungu na nchi ndio kutufugia wahalifu na kufanya mauaji ya wakosoaji wako?

unasema Samia anawaza kila mara uchaguzi wakati, kipindi cha Magufuli ndio tulikuwa tunafanya uchaguzi kila mwezi kisa kuhonga na kutishia wapinzani wamuunge mkono? nani aliyekuwa na siasa chafu kati ya Magufuli na Samia?
nani mfuasi wa magufuli?
 
Back
Top Bottom