Kwa heshima na taadhima, nawaomba CCM 2025 mtuletee Mgombea bora mwenye uchungu na nchi hii

Kwa heshima na taadhima, nawaomba CCM 2025 mtuletee Mgombea bora mwenye uchungu na nchi hii

Ukweli mchungu mama 2025 nafasi hii aachie wengine amalizie hicho kiporo.

Kwa sasa anasifiwa na wanaojuwa kufisadi nchi huku wakimvisha kilemba ukoka kuwa anaupiga mwingi wengine wakiumia tena kuumia kupitiliza!

Tayari wengine baada ya kuanza kutafna keki ya taifa wanajiita nyuki wa mama.

Na mama mwenyewe ni kama ameziba masikio. Akumbuke alienda mkoa wa mara alijiona mwenyewe jinsi wakuu wa idara walivyokuwa wakikwamisha baadhi ya miradi na kujilipa fedha za umma !

Huo ni mkoa aliofanyia ziara je mikoa mingine huko pakoje?
Msoga back in office for a third term.
 
Lakini pia mimi kama mwananchi wa kawaida mwenye uhuru wa kutoa maoni katika nchi hii, ninapenda kumueleza Rais Samia kwamba Sisi tunampemda na tunamuheshimu sana, aendelee kuchapa kazi kwa kipindi hiki kilichobaki lakini chonde chonde 2025 aamue tu kwa hiyari yake kutogombea tena nafasi ya Urais ili kulinda heshima yake.
Acha kumpangia cha kufanya.
 
Baada ya kuona kabisa kwamba tuko kwenye uelekeo ambao hauna dira, napemda kutoa Rai kwa Chama cha Mapinduzi 2025 mtuletee mgombea Urais mwenye dira maono na mwenye uchungu na Rasilimali za nchi hii.

Hatuhitaji mtuletee mtu ambaye kutwa kucha anawaza uchaguzi na jinsi ya kuendelea kuwa Rais badala ya kuwaza maendeleo ya watanzania,

Hatuhitaji mtu amabye yuko radhi kuwaruhusu watu wafanye ufisadi ili wampe sapoti aendelee kuwa Rais hatutaki!

Lakini pia mimi kama mwananchi wa kawaida mwenye uhuru wa kutoa maoni katika nchi hii, ninapenda kumueleza Rais Samia kwamba Sisi tunampemda na tunamuheshimu sana, aendelee kuchapa kazi kwa kipindi hiki kilichobaki lakini chonde chonde 2025 aamue tu kwa hiyari yake kutogombea tena nafasi ya Urais ili kulinda heshima yake.

Asanteni sana
Yupo Mbowe au Lisu uje umchague tuu
 
Kama taifa kwa muda tunatembea na sera ipi maana viwanda naona imetushinda.

kuna muda najaribu kufananisha CCM na Chama cha kikomunisti cha china nikagundua utofauti mkubwa baina yao ni uzalendo wa dhati,ccm wengi ni wanafki,wabinafsi na wasiolitakia taifa hili maendeleo...
Ulipo hapo unaelewa hata dira ya Taifa?
 
Ukiona mtu anasema Rais Samia hafai ujue mrija wake wa kula umekata.

Watumishi wamekaa miaka 5 hawajaongezewa mishahara, fao la kujitoa nssf wamekula pesa zetu, ajira zilikua hazitolewi hayo ni baadhi ya machache tu lkn kipindi hicho chote hukuona Rais aliyekuwepo hafai.

Sasa hivi unaleta mdomo wako kwasababu mrija wako umekatwa[emoji28].

Tuliza mbupu hizo
Ajira zilikua hazitolewi alafu ww huyohuyo tena uliitwa interview ya TRA
Screenshot_20220323-160817_1.jpg
 
Naunga mkono hoja.Ikibidi aliyepo sasa ajiuzulu tu ili kupisha kiongozi mzalendo na mwenye uchungu na nchi
Ili waje wateke watanzania na kutumbukiza mtoni kwenye viroba?

Hivi huo uzalendo wenu mbona uko tofauti na neno lenyewe?

Uzalendo wa kuua na kunyang'anya watu Mali zao ndo mnaona unafaa?
 
Back
Top Bottom