Kwa hiki kisa changu naweza kupata madai yangu NSSF?

Kwa hiki kisa changu naweza kupata madai yangu NSSF?

Habari wakuu! Nilikuwa nafanya kazi mkoa wa kusini Songea ajira ya mkataba wa muda baada ya mkataba kuisha nilienda kuulizia taratibu za kufungua madai wakaniambia mimi bado kijana nitapata kazi nitaendelea kuchangia..

Imepita almost miaka miwili nikiwa Sina kazi nikakumbuka Kuna hela nilikuwa nachangia NSSF itakuwa wakati sahihi kuidai kutokana na ugumu wa maisha nayopitia.

Nimeeanda tawi la Ubungo kuulizia utaratibu wananiambia inabidi niwe na barua ya kumaliza mkataba, cheti Cha muajiri wangu kimsingi hivyo vyote Sina nilipewa na muajiri wangu ila Sina idea yoyote vipo sehemu gani kwa kifupi nimepoteza.

Nikaambiwa kwenye fomu ya madai inabidi nipeleke kwa muajiri Kuna section yake ya kujaza muajiri wangu yupo Ruvuma mimi nipo Dar.

Binafsi kitu nilichonacho kinachohusiana na kazi yangu ya zamani ni Mkataba na salary slip pekee.. je Kuna possibility ya kupata madai yangu ukizingatia ndio tumaini pekee nililonalo kwa Sasa??
Tafuta documents unapewa less.juzi wamenipa mzgo wangu 5m plus
 
Pambana kupata vielelezo hivyo uwaibukie tena mkuu.

"wewe bado kijana utapata kazi" hivi hawa wasenge huwa wanatumia masaburi kufikiri? Hela yangu halafu wewe unipangie muda wa kuichukua, inaingia akilini kweli?
Nyumba jenge mimi veve lale bure kenge kabisa hawa jamaa.
🤣🤣🤣🤣🤣
 
Kuna mwanangu yalimkuta kama hayo, alikuwa anafanya kazi kwenye shirika fulani, mkataba ukaisha wazee wakasepa...
Akaunti ya nssf inasoma milioni 30+ lakini anagongea mpaka hela ya gesi nyumbani kwake.. Kila anavyofurukuta wapi, ni mpaka alivyopata kazi kwingine maisha yakarudi kwenye matari,
Maisha yalipokaa sawa Sikuwahi tena kumuuliza kama alifanikiwa au lah, na ukaribu ukaisha😂🤣
 
Duh inakatisha tamaa
 
Sema kupata pesa zako NSSF ukiwa kama proffesional ni mziki ,hapo watakupa 33% kama fao la kukosa ajira
Ilikuwa siyo professional qualifications ilikuwa kujua kusoma na kuandika
 
Back
Top Bottom