Kwa hiki wanachokifanya DP WORLD bandarini, maadui zetu wakubwa ni viongozi wetu walioruhusu upuuzi kudumu muda mrefu

Kwa hiki wanachokifanya DP WORLD bandarini, maadui zetu wakubwa ni viongozi wetu walioruhusu upuuzi kudumu muda mrefu

KING MIDAS

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2010
Posts
8,589
Reaction score
16,936
Wananzengo, mu Hali gani?

Kwa masikitiko makubwa Leo nawatangaza hadharani maadui wakubwa wa taifa letu.

Laiti tungekuwa na uongozi imara tungekuwa mbali sana kwenye mafanikio ya kiuchumi.

DP WORLD wamepewa bandari bure, wamepewa na vitendea kazi bure. Leo wameongeza Terminal Trucks kumi na trailers 27. Wameleta Rubbered Tyred Gantre (RTG) nane. Na sasa hamna meli inakaa mwezi mzima dock ikisubiri foleni. Container ships zinaingia moja kwa moja kupakua mzigo.

Pia soma: DP World yashusha meli nzima ya vifaa bandarini, TPA wasema walishakabidhiana tangu April 7

Walichofanya DP WORLD ni kujaza vipuri kwenye warehouse, TPA wao hawakuweka kipuri hata kimoja warehouse, hadi magurudumu yakiisha kwenye Rich Stacker, wanatafuta Rich Stacker mbovu wanaivua gurudumu.

Viongozi wetu walikuwa wanayaona haya lakini wakishirikiana na CCM wakawa wanachukulia poa sana.

Mapapapa fisadi wa CCM wakanunua Quay Crane mbili kwa mabilioni ya pesa, kwa miaka nenda rudi hizo QC hazikufanya kazi, wamekuja DP WORLD wamenunua jenereta mbili, QC zinafanya kazi sasa, wamepata bure.

Folk lifts zinakuwa grounded kwa kukosa matairi; ni aibu gani hii?
 
Kwahiyo waliamua kufanya makusudi ili ionekane hakuna ufanisi ili wawauzie binamu zao wa dubei?
Unafikiri pale bandari kuna cha maana , urasimu pale wa kuchelewa ilikuwa ni awatu wenyewe ...Wale wafanyakzi ambao sasa wapo Dp world ndio hao hao wanapiga kazi maana huku wanaweza kutimuliwa.

Hakuna cha maana zaidi ya kubweteka kwa watanzania , kufanya kazi kwa mazoea ...Lazima wamuogope Muarabu wafanye kazi .

Kama tungekuwa na utaratibu wa kuwa na DG kutoka nje labda wachina , wazungu , wahindi , basi wabongo wangefanya kazi kwa shuruti tungefika mbali sana .​
 
Ameeleweka sana hapo!
Anashangaa haya maboresho yangefanyika hata kabla ya dp world kuja. Anashangaa idara ilikuwa wapi? Mpaka mambo yalikuwa yanasuasua?
Ukiona mtu hafanyi matengenezo madogomadogo nyumbani kwake basi huko kazini ujue kupo mifupa tupu anachoweza yeye ni kuvaa suti, kuchonga ndevu na kuinua mabega kutaka utukufu, ndivyo walivyo maboss wengi wa nchi hii
 
Unafikiri pale bandari kuna cha maana , urasimu pale wa kuchelewa ilikuwa ni awatu wenyewe ...Wale wafanyakzi ambao sasa wapo Dp world ndio hao hao wanapiga kazi maana huku wanaweza kutimuliwa.

Hakuna cha maana zaidi ya kubweteka kwa watanzania , kufanya kazi kwa mazoea ...Lazima wamuogope Muarabu wafanye kazi .

Kama tungekuwa na utaratibu wa kuwa na DG kutoka nje labda wachina , wazungu , wahindi , basi wabongo wangefanya kazi kwa shuruti tungefika mbali sana .​
So ilitengenezwa scenario ya kuonekana hatuwezi kujiendesha ili bandari iuźwe. Maana kama shida inajulikana kwanini tusinge deal nayo wenyewe?

Na je unafikiri sasa hivi hakuna upigaji? Unafikiri waliosaini huo mkataba hawajapiga na hawaendelei kupokea fungu?

Hii nchi ni ngumu sana asee unahitaji kuwa na upeo sana kuelewa kinachoendelea

ephen_
 
Wananzengo, mu Hali gani?
Kwa masikitiko makubwa Leo nawatangaza hadharani maadui wakubwa wa taifa letu.

Laiti tungekuwa na taasisi imara ya intelijensia tungekuwa mbali sana kwenye mafanikio ya kiuchimi.

Idara ya usalama wa Taifa wamejaza mashushu bandarini tangu enzi za Mwalimu, wanachokifanya ni aibu. Zama za Mwalimu Idara ya Usalama wa Taifa ilikuwa vizuri kweli kweli, lakini kipindi cha fursa Idara inaenda likizo hadi alipikuja magufuli

DP WORLD wamepewa bandari bure, wamepewa Na vitendea kazi bure. Leo wameongeza Terminal Trucks kumi Na trailers 27. Wameleta Rubbered Tyred Gantre (RTG) nane. Na sasa hamna meli inakaa mwezi mzima dock ikisubiri folenj. Container ships zinaingia moja kwa moja kupakua mzigo.

Walichofanya DP WORLD ni kujaza vipuli kwenye warehouse, TPA wao hawakuweka kipuli hata kimoja warehouse, hadi magurudumu yakiisha kwenye Rich Stacker, wanatafuta Rich Stucker mbovu wanaivua gurudumu.

Idara ya Usalama wa Taifa walikuwa wanayaona haya lakini wakishirikiana na CCM wakawa wanachukulia poa sana.

Mapapapa fisadi wa CCM wakanunua Quay Crane mbili kwa mabilioni ya pesa, kwa miaka nenda rudi hizo QC hazikufanya kazi, wamekuja DP WORLD wamenunua jenereta mbili, QC zinafanya kazi sasa, wamepata bure.

Folk lifts zinakuwa grounded kwa kukosa matajiri, ni aibu gani hii?
Dpp wote wamepeqa bandari Bure,hapo ndio uongo wako umeanza
 
Unaweza ukawa na hoja nzuri ila umechanganya uongo mwingi sana hv Dpp wote tuwape bandari ya bure
 
Back
Top Bottom