Kwa hili la Corona, Magufuli anaenda kuonekana shujaa

Mzee leo at least nimepata usingizi, nimekosa usingizi muda mrefu sana kwa karibia week mbili sasa.

Mkuu wapo wanapata na nguvu ya kuleta mada za siasa (hata leo) humu jamvini na hata kuangazia uchaguzi mkuu 2020.

Aliimba prof. Jay - "tuko tofauti".
 
Unaota ww sio bure

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Mkuu ni mashaka makubwa kama jpm mwenyewe anakubaliana nawe kwenye hili.

Ila kwa vile wengine tumejiapiza kusifu kila juhudi, amini nakwambia mtampongeza kwa juhudi zozote atakazochukua bila kujali zina mashiko au la.

Hapa ndipo jpm alipaswa kuona. Afanye uamuzi sahihi bila kujali pongezi zenu maana mtapongeza pongeza tu.
 
Bado unaamini hivyo?
 
Afadhali wenzetu angalau mnapata usingizi mnalala na mnaamka.
Sisi wenzenu usingizi hatupati, unapanda tuu kitandani na kuishia kughalaghala hadi kunakucha.
P
Uwe unasali mkuu, Mungu hashindwi kitu.

Katika hizi siku 3 za kuitokomeza corona,weka pia dua zako uwe unapata usingizi.

Maana yanenwa,bila Mungu wakeshao wajisumbua bure.

Sent using iphone pro max
 
Umesema kweli kbs hata China walisali tu sijui kanisa gani mpaka ugonjwa ukakimbia wenyewe. Waliwndelea kuchapa kazi. Mungu bariki hekima za viongozi wetu

Jana China karipoti vifo 1,290 ambavyo anasema eti alisahau kuvitolea taarifa.

Na hii ni baada ya presha kutoka USA kwamba China alificha data.
 
Jana China karipoti vifo 1,290 ambavyo anasema eti alisahau kuvitolea taarifa.

Na hii ni baada ya presha kutoka USA kwamba China alificha data.
Nasisitiza
China inaonekana kuna vifo vingi hajavitangaza

Mbona katangaza baada ya shinikizo la Marekani, na inaonekana China kuna kitu anakijua kuhusu huu ugonjwa
 
Hata jpm akisema anafunga kila kitu hawa jamaa watakuja tena kusifu
 
I wish kama wangeruhusiwa kutoka wale tu wenye ulazima...lakini wafanyakazi wangebaki nyumbani...hii ingepunguza msongamano kwenye baadhi ya maeneo mfano kwenye usafiri wa umma

"corona ipo tuchukue tahadhari"
 
Hii coment tui pin, naona inakuwa vice versa now

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shu
Shujaa dhidi ya nani??? Hili tatizo halina mshindi wala anaeshindwa. Dunia nzima itashinda kwa jina la Yesu alie hai. Kuna watu watakufa na wengine wamekufa tayari, wengine watapona. Na tatizo litakapoisha kutakuwa na tatizo lingine KUBWA. Uchumi utakuwa hohehahe utadorora. Huo muda wa kushangilia au kuonekana bingwa hautakuwepo. Watanzania tuache KUJIPENDEKEZA na siasa za jalalani kwenye matatizo makubwa kama haya ambayo Dunia nzima hailali inahangaika. Mungu ibariki Tanzania na watu wake Amina.
 
Tatizo ni pale ulipoamua kuwa mpiga ramli, bado unafikiri ulichokiandika ni sahihi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…