Pascal Mayalla, Ndivyo Italy na US walivyokuwa wakijisifu mwezi wa January na wa February. Kawaulize leo, miezi miwili baadaye, kama bado wana nguvu ya kuyatamka maneno hayo.
Leo Waziri Mkuu wa Italy anatoa machozi na kusema walifanya upumba.vu mwanzoni, la sivyo hali isingekuwa kama ilivyo leo.
Tuchukue tahadhari zote. Tumwombe Mungu atujalie hekima a njia sahihi za kupambana na ugonjwa huu.
Mungu wetu alitufanyia muujiza mkuu kuliko yote kwa kutuumba kwa mfano na sura yake. Akatumegea sehemu ya ufahamu wake, sehemu ya utash na hekima yake na akili yake ili tuvitumie hivyo vyote kuyamudu mazingira aliyotupatia.
Tuombe sana hekima na ufahamu kuliko kukaa tu na kusubiria muujiza. Miujiza haijawahi kutuondolea malaria, kipindupindu, ebola, cancer, kisukari, na mengine mengi. Lakini Mungu anatenda miujiza kwa kupitia watu wake kwa kutupatia ufahamu. Na tunapotumia ufahamu aliotupatia, huku tukiomba neema na ulonzi wake, zile jitihada zetu huzibariki, na kuzijalia matunda.
Mtume Paulo anasema, tufanye kazi. Kuyatambua mazingira yetu na kutenda kazi zinazotufanya tuyamudu kwa kutumia karama mbalimbali, tofautitofauti, ndipo tunapata ushindi dhidi ya majanga.
Wataalam wafanye tafiti
Matabibu watibu na kutoa elimu
Umma ufuate maelekezo
Waombaji wakeshe wakiomba
Makuhani, washekhe wahubiri kwa usahihi
Watawala wasimamie maelekezo
Kila mmoja akifanya kazi, tutashinda. Lakini usibweteke kusubiria muujiza wakati hakuna jitihada yoyote unayoifanya.