Kwa hili la Corona, Magufuli anaenda kuonekana shujaa

Kwa hili la Corona, Magufuli anaenda kuonekana shujaa

Siku zote waweza kumdharau masikini Ila mawazo yake ni Lulu, matajiri wengi hufanikiwa kupitia mipango na mawazo mazuri ya maskini

Mwenye Mali hujivunia Mali zake huku akili zake akiziweka pembeni, Hapa, lazima Jemedari Jembe Magu wamheshimu na Tanzania Kwa ujumla wake,
 
Kosa walilofanya wanasiasa ni kushindwa kuwaelimisha watu namna ya kutumia khanga vitambaa ,hijabu na hata Maski kwa wenye buwezo kuziba misomo na pua zao. Hii inasababisha watakaoupata waueneze kwa kukohoa au kupiga chafya.

Mfano kwenye mabasi hakuna anayeziba pua wala mdomo. Hata kwenye Hospitali ni madaktari na manesi zanaziba lakini wagonjwa na watu wengine wapo midomo wazi bila kujali athari ya maambukizi kwa wagonjwa ambao bado hawajagundulika.

Tamko la kazi ni zuri ila watu wazibe midomo yao na pua. Kuna mgahawa mmoja niliwauliza wapishi inakuaje hawazibi midomo na pua wakati wanauza chakula. Chakula ni dawa namba moja kwa kiumbe hai. Inabidi kitolewe kwenye mazingira masafi.

Mh.Rais tunamuomba atoe wito wa watu kuvaa nguo au vitambaa au maski zinazoziba midomo kwa wakati huu nchi nzima hasa mijini.

Wanawake watumie khanga au hijabu kuziba midomo wanaume watumie hata leso au maski a ujenzi au wananune vitambaa wafue na maji ya moto na sabuni Mara kwa Mara na kunawa mikono .

Dunia iliulenga huu ugonjwa kwa waafrika lakini Mungu muumba bado anatulinda kwa wema wake.

Magufuli ni baba laooo!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Incubation period ya coronavirus unaielewa? Ni kati ya siku 14 - 32. Italy na US iliingia mwezi January. Maafa ni sahizi. China ilianza mwezi December, maafa yalikuwa February. Afrika maambukizi yameanza March. Tusubiri tufike May, ndipo tuseme, tumebahatika. Na tumshukuru Mungu wetu kwa ulinzi wake. Sahizi ni mapema mno.
Mkuu hapo kwenye IP nafikiri utakuwa umeteleza kinamna flani. Highly Virulent organisms hawawezi kuwa na Incubation Period ya up to 32 days. It’s less than that..!
 
Nimegundua una tatizo la kiingereza. Trump alitaka kufanya jambo ambalo kisheria liko mikononi mwa serikali za majimbo - ndio sababu ya kutofanya karantine ya kitaifa. Serikali za majimbo zinashauri wananchi wafanya mambo sahihi na wakae nyumbani. Trump alitaka kuzuia watu wa majimbo matatu wasiruhusiwe kuondoka majimbo yao (kama ilivofanga Hubei huko China).

Rais wetu amafanya uamuzi wa kutoweka lockdown kutokana na sababu za kiuchumi. Uchumi wetu ni cash based, lazima mtu akafanye kazi ya mikono ili apate ujira. Lazima uende sokoni/dukani kununua vitu. Mahitaji yanahusisha movement ya mwenye pesa!! Kwa ujumla lockdown ingeleta shida kuliko korono yenyewe!!

Ulichosahau ni kusema kuwa hata Rais kaiga mambo mengine kama forced self-isolation, kunawa mikono nk. Naona unajaribu kumuona kama ni smart sana - yuko sawa na viongozi wengine tu! Nothis is special here.
 
Sisi tukiwa makini kwenye kuzuia maambukizi, tutavuka.

Mtu mwerevu hujifunza kutokana na makosa ya waliotangulia.

Naam, nimekupata vizuri.

Sasa labda kitu cha kufanya tuweke hivyo vigezo vya kuzuia ugonjwa, na vigezo hivyo tuvipigie assessment pia ya faida vs challenge za kuvifikia.

Naomba nianze na wewe, niambie tufanyaje.
 
Molembe, Wakushukuriwa ni mungu Pekee, elewa kuna Nchi nyingine hazina hata maambukizi ya MTU hata mmoja mpaka sasa na hawajafunga mipaka na maisha yanaendelea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naam, nimekupata vizuri.

Sasa labda kitu cha kufanya tuweke hivyo vigezo vya kuzuia ugonjwa, na vigezo hivyo tuvipigie assessment pia ya faida vs challenge za kuvifikia.

Naomba nianze na wewe, niambie tufanyaje.
Kimsingi vigezo vinatolewa na wataalam kwa kuujua ugonjwa wenyewe vizuri na njia sahihi. Kwa sasa yote tunayoyafanya yameegemea taarifa zao.

Ningekuwa mimi ndiye mwenye mamlaka, kikubwa ambacho ningekifanya zaidi ni kuwatumia wataalam ambako ugonjwa ulianzia. Hawa wanaujua vizuri. Wanafahamu wapi wslipokosea na wapi walifanya vema. Ili pale walipokosea, nasi tusiipitoe njia hiyo hiyo.

Bahati yetu kubwa, ugonjwa haukuanzia kwetu. Kwa hiyo tuna nafasi kubwa ya kujifunza kupitia kwa waliotangulia kuathirika.

Hali yetu kwa sasa, ni sawa na mtu anayesafiri majira ya mvua. Mbele yako kuna gari limetangulia. Mnafika kwenye mto uliofurika, hujui kama daraja lipo au halipo, na hata kama lipo, bado hujui upana wa daraja unaishia wapi. Aliyetangulia anasema anajua daraja linapoishia. Anatangulia, kisha anatumbukia na kuzama majini. Utakuwa mpum.bavu hasa kama na wewe utasema, mwenzangu amepata hapa, ngoja na mimi nimfuate.
 
Pascal Mayalla,
Mkuu umesomeka vizuri katikati ya mistari "between the lines". Huyu ni Papa wa kanisa katoliki ambalo Mh. analiamini kikamilifu. Hapa ilibidi aendeshe maombi St. Peter Square peke yake kutokana na hali kuwa tete.
images (10).jpeg
images (11).jpeg


Hapa ni kipindi cha nyuma mambo yalipokuwa kawaida.
images (13).jpeg
images (12).jpeg

Tunacheza bahati nasibu, ikikubali atakuwa shujaa, yakienda kombo akubali kubeba lawama zote. Yote kwa yote tutakaoumia ni sisi wananchi akifunga nchi tutakufa kwa njaa akituachia huru sana tunaweza vunja rekodi ya maambukizi duniani... wahenga walisema mwenzako akinyolewa, zako tia maji.
 
Naunga mkono hoja, rais Magufuli ni shujaa.
Wakati nchi za wenzetu wanaona Corona kama ugonjwa hatari hivyo kufunga mipaka, kusimamisha shughuli zote na hadi kufanya lock down kwa kutegemea nguvu za binaadam, shujaa rais Magufuli ameishtukia Corona sio ugonjwa bali ni shetani limekuja kwa mfano wa ugonjwa hivyo alichofanya ni jambo dogo tuu, kulikabidhi kwa Mungu ambaye ni kiboko ya shetani.

Mungu ameisha tukingia mkono wake, Tanzania bado hakuna kifo wala maambukizi ya ndani kwa ndani, local transmissions. Hivyo tuungane na rais wetu Magufuli, tusitishane, na Watanzania tuendelee kuchapa kazi, kwenda Kanisani, msikitini na kichanga na watu kama kunywa kawawa mitaani kwa kukaribiana as if nothing happened huku tukichukua tahadhari kama tunavyoelekezwa na wataalamu iliwemo kunawa mikono kwa sabuni na maji tiririka.
P
Kama nchi itatuchukua siku 21 hadi 30 kujua ugonjwa umetapakaa au la ili tujisifu. Kumbuka wamarekani na nchi za ulaya imechukua mda tangu walipofanya evacuation ya watu wao toka uchina hadi ulipoanza kuwafanya Kama kuku wenye mdondo. Bado hatujavuka mto tusitukane mamba.
 
Nchi zote duniani zimechukua tahadhari kubwa kuhusiana na hili gonjwa la corona, kuna serikali zimefungia raia wake wasitoke nje ikiwemo nchi za Africa Isipokuwa Tanzania.

Kwa hakika hili la rais Magufuli kuruhusu shughuli ziendelee anapaswa kupongezwa na sio kubezwa, watanzania wengi ni masikini sana kipato chao kinategemea atoke arudi na chochote kumzuia akae ndani atakufa njaa.

Kwa kweli rais wetu ameona mbali kuruhusu shughuli ziendelee, cha muhimu ni sisi watanzania kumuunga mkono kwa kuuchukua tahadhari zote tuwapo kwenye shughuli zetu, na kwa hakika baada ya hili janga rais Magufuli ataonekana shujaa hasa katika ukanda wetu huu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Na kwa mfano tukiangamia kama Italy ataoekanaje?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watanzania ombré ni mungu huu ugonjwa usitokee mlipuko,Najionea kwa macho yangu hawa mnaowaita mashujaa Leo kesho mtawalaumu
 
Ila nimejaribu kutembea huko mitaani Yan wananchi hawajali kabisa kuhusu huu ugonjwa. Hakuna tahadhari yoyote wanayoichukua ndio Kwanza wapo busy na mambo yao bila tahadhari yoyote,

napata shaka endapo ugonjwa huu utaingia mitaani kwa lugha nyingine uswazi tutamdisapppoint rais wetu, maana kwa mtindo huu wa maisha maambukiz yatakuwa kwa kiwango Cha juu sana ambacho akijawahi shuhudiwa tokea janga hili limeikumba Dunia hii.
Ugonjwa huu sio kama unavyopambwa huku kwetu Aftica
 
Nchi zote duniani zimechukua tahadhari kubwa kuhusiana na hili gonjwa la corona, kuna serikali zimefungia raia wake wasitoke nje ikiwemo nchi za Africa Isipokuwa Tanzania.

Kwa hakika hili la rais Magufuli kuruhusu shughuli ziendelee anapaswa kupongezwa na sio kubezwa, watanzania wengi ni masikini sana kipato chao kinategemea atoke arudi na chochote kumzuia akae ndani atakufa njaa.

Kwa kweli rais wetu ameona mbali kuruhusu shughuli ziendelee, cha muhimu ni sisi watanzania kumuunga mkono kwa kuuchukua tahadhari zote tuwapo kwenye shughuli zetu, na kwa hakika baada ya hili janga rais Magufuli ataonekana shujaa hasa katika ukanda wetu huu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sikupingi ✔️✔️✔️
 
Naunga mkono hoja, rais Magufuli ni shujaa.
Wakati nchi za wenzetu wanaona Corona kama ugonjwa hatari hivyo kufunga mipaka, kusimamisha shughuli zote na hadi kufanya lock down kwa kutegemea nguvu za binaadam, shujaa rais Magufuli ameishtukia Corona sio ugonjwa bali ni shetani limekuja kwa mfano wa ugonjwa hivyo alichofanya ni jambo dogo tuu, kulikabidhi kwa Mungu ambaye ni kiboko ya shetani.

Mungu ameisha tukingia mkono wake, Tanzania bado hakuna kifo wala maambukizi ya ndani kwa ndani, local transmissions. Hivyo tuungane na rais wetu Magufuli, tusitishane, na Watanzania tuendelee kuchapa kazi, kwenda Kanisani, msikitini na kichanga na watu kama kunywa kawawa mitaani kwa kukaribiana as if nothing happened huku tukichukua tahadhari kama tunavyoelekezwa na wataalamu iliwemo kunawa mikono kwa sabuni na maji tiririka.
P
Tanzania inazungukwa na nchi kama saba hivi,kama nchi hizo zote zimefunga mipaka yake maana yake hakuna raia wa nje anayeingia tz wala kutoka tz maana majirani wamefunga mipaka yao,tunachokifanya ni kuacha wananchi wetu waendelee na shughuli zao kama kawaida kule kwenye viwanja vya ndege tuna dhibiti kwa kuwapima na kukaa karantini kwa siku 14 baadae maisha yanaendelea bila kuathiri waliomo ndani.ndo maana mpaka sasa maambukizi ni kidogo sana tz

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom