Kwa hili la Corona, Magufuli anaenda kuonekana shujaa

Hivi bro, unadhani ni tahadhari gani US, UK, Spain, Italy nk hawajachukua?

Hizi ni first world countries, kila siku watu wanaugua na wanakufa.

Sisi tuchukue tahadhari zipi ambazo wao hawakuchukua?
Wamechukua tahadhari wakiwa wameshachelewa. Watu wao walipoanza kupukutika kama kuku ndiyo wamepata akili kwamba huu ugonjwa is not a joke, Wakaanza lockdown kila mahali.
Italy waliaminishwa na viongozi wao kuwa ni flu tu, hakuna hatari yoyote.
Marikani Trump alifanya mzaha akasema ni chinesevirus kama vile wao haiwahusu. Sasa wanahaha hawana hata vitanda vya kutosha kuwalaza wagonjwa
Kuna rais wa Brazili naye juzi kasema "It is just a little flu"
Spain nao walizembea hivyo hivyo wakidai ni flu.
Baada ya mlipuko kutokea ndio wanachukua tahadhari..too late.
Sisi hatujachelewa, bado tunaweza kuchukua tahadhari na tukafanikiwa. Tuwe serious huu ugonjwa hautaki kufanyiwa mzaha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nchi zenye viongozi wacwanyonge zimesema raia kaeni ndani serikali itawaletea chkula kuliko serikali kuingia gharama kutibu watu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unasema maambukizi ni kidogo mpaka sasa, umewapima watu wangapi, na walioonekana positive ni wangapi?

Kama hujawapima watu wako, wewe upo gizani. Hujui kiwango cha maambukizi. Unaendesha mambo kama wapiga ramli.
 
*Anaandika Padre Titus Amigu*

*HEBU TUONYE HATA WAKATI USIOFAA (2Tim 4:1-5).*

Ukitaka kujua uongo wetu au wa wachungaji na manabii na mitume n.k. itokee shida ya kweli kama sasa corona virus.

Kila mchungaji na nabii na mtume kakunjia mkia wake kwenye begi.

Katika kiboko hiki hakuna mbabe wa miujiza katika kanisa wala dini yoyote.

Lakini shida hii ikipita eti tutaanza kupigiana kelele na kudanganyana tena.

Sasa hivi hakuna maleso yenye upako wala keki zenye upako wala mafuta ya kukanyaga dhidi ya coronavirus.

Wala wafufua watu hawapo sasa.

Mbona maiti za bure zi tele huko na huko! Wote kimyaa! Wote wananawa mikono na konani wana "sanitizer" na "mask."

Hesh, sala kwa mbali na woga papo!

Kumbe, tukome kujigamba. Na yawezekana Mungu anaruhusu ugonjwa huu uendelee hivi kusudi atufumbe vinywa kwanza.

Wapenzi, tuache maneno ya kujitukuza wenyewe.

Tumepatikana sote! Kumbe tufanye nini?

Wanadamu wote tusali kwa kujidhili tukiomba kama mkoma wa kwenye Injili tukisema, "UKITAKA WAWEZA KUTUTAKASA" halafu tumwache Mungu aseme kwa wakati wake, "NATAKA TAKASIKENI" (Mt 8:3, Lk 5:13); hapo ndipo ama moja kwa moja au kwa kupitia wanasayansi tutaoneshwa suhulu ya coronavirus.

La sivyo tutakoma.

Tutubu majigambo yetu.

Mzee wenu Pd. Titus Amigu
 
Sijawahi kumkubali jiwe ila kwa hili naona kama yupo sasa hivi hasa ile Statement yake imesaidia kuondoa hofu
 

Hao wote wame ambukizwa kwa njia ya hewa sio kushikana mikono au kukumbatiana - ziara, makongamano na press conferences, sherehe za kukata utepe wa majengo mapya na projects mpya and what have, njia hizo ndio conduit iliyo tumika kuambukiza akina Price Charles, Waziri Mkuu wa Uingereza, Waziri Mkuu wa Ujerumani nk. Mikusanyiko ya watu ni hatari sana virus vina diffuse na kubaki hewani kwa dakika arobaini na tano!! Chunga sana.
 
Pasi, tukipata confirmed cases 100 mezani hali itaendelea kama ilivyo?

Linapokuja suala la Corona kwa nchi za kiafrika sio la kulipigia chapuo, hata uwezo mkubwa wa kupima na kujua ukubwa wa tatizo haupo wengi hatuna.

Sema kwamba tumeamua kuikaushia kama unavoona ngoma aka waya aka VVU kuwa isiwe nongwa tuendeshe harakati za kimkakati zisizoumiza kichwa.

Hakuna mshindi kwenye hili isipokua elo lilebhaka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu ndiyo uthibitisho halisi kwetu sisi wasoma biblia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ameamua kupingana na ushauri wa kitaalamu, ni sawa na mtu anayekataa kuchemsha maji ya kunywa kwenye mlipuko wa kipindupindu, hata familia yake isipokufa kwa kipindupindu bado hatuwezi kumsifu mzazi huyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sadly huku mtaani tunaishi chini ya muujiza kwani hakuna hatua zozote zinazochukuliwa baada ya kuweka vindoo vya maji na solution ya omo kama sanitizer mlangoni pa duka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamani sisi wabongo hakuna utafiti wowote ulitoa jibu kuwa uongozi nyeusi ni ngangari dhidi ya Coronavirus,,,, tusiache ,tusichoke kujikinga.. Mungu atusaidie.[emoji120][emoji120]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kusema ukweli huu ugonjwa ukiamua kuchanja mbuga unachanja tu.
Wee hao huko hali tete mno na tahadhari zote walizochukua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…