Kwa hili la huyu mpenzi wangu acha pesa zangu ziishie kwa mama tu!

Ila we jamaa mkorofi sana🤣🤣
 
Yeah labda hujaelewa kikubwa alichomaanisha mleta mada na inawezekana pia you don't have a broad understanding of a word "GIRLFRIEND"
Haimaanishi kuwa na mahusiano ya kimapenzi tu bali " Expression of love or liking to any woman"
Sawa mwalimu wa English
 
Yaani katika moja ya vitu mabinti wengi wa kizazi hiki wanafeli ni kukosa shukrani kama hivi
Mimi nikiona mdada yuko hivi huwa naachana naye fasta maana sipendagi kabisa!
mwingine anakuomba vocha unamrushia hata kukutumia text ya asante hakuna unamwona online yuko busy mpaka umpigie wewe kumuuliza kama vocha imefika..ila nilichojifunza asilimia kubwa ukiona hivyo jua mwanamke hakupendi kabisa ila yuko na wewe kwa shida zake
 
Hii nimeipenda hii nimeipenda tena 😆😆😆🤪 wapo wengi wenye hayo matabia ya kiduanzi Ila kuna wengine hata ukimrushia 500 anakushukuru km umemrushia 100,000 tatizo ni tabia na malezi na makuzi kuna mabinti wamekulia malezi ya ajabu hawajafunzwa kusema Asante na kushukuru mwingine kusema Asante anaona km utumwa na kujidogoza na kujishusha yaan ana kiburi na jeuri ya ndani kwa ndani nikuambie Asante kwani we nani kwangu? We Mungu? Hivyo ndio hujisemea kimoyomoyo 🤪
 
Natamani huu uzi uwe pinned post tujifunze kitu kuna jamaa angu anaonga hadi millions wakati mm nadaiwa na jirani angu elfu 60 hadi nimehama mtaa.

Sent from my SM-A042F using JamiiForums mobile app
 
Hawa ndugu zetu hawana shukrani sana.
Jana ilikuwa mahafari ya chuo kimoja hapa Tz.

Kuna dada alinialika kwenye mahafari hayo, bila hiyana nikaenda kumpa kampani maana sio baba yake wala ndugu yake yeyote aliyeweza kufika.

Niko eneo la tukio namuulekeza nilipo mtu hatokei, nilikaa almost dk 15 sehem hiyohiyo anaesema yeye yupo hatokei.
Badae ananiambia ooh nimeona mvua imeanza so niko sehem fulan, mimi hapo nime mind kinoma nacheki tu video za tiktok kupunguza jazba.

Tukaja kuonana, tukaongea yakaisha. Jioni nikasema naenda kumpa company, imefika night niko kwenye boda namwambia nakuja ananiambia yeye na mwenzie anaenda kula hawezi kumuacha mwenzie akale pekeyake sabab mwenzie hajazoea kula peke yake, NONSENSE hivi kuna mtu kweli njaa ikimpiga hawez kula hadi awe na company,

Nikamwambia poa ila mimi nishafika ulipofikia akasema basi niwasubiri wakafate msosi, nikajiuliza hivi kwann asiende mmoja mwingine abaki namimi mgeni kuliko kuniacha nje napigwa na mvua.

Nikamwambia kama vipi weken vitu vyenu fresh mimi nichill room nyie mtanikuta, oooh tumeshaondoka tunarudi sasa hivi ,tunafata tu msosi tunakuja kulia room, nikasema sawa.

Nimekaa pale kuondoka nashindwa mvua inapiga inaacha inapiga inaacha, boda hazipiti.

Nimekaa almost nusu saa hawajarudi, simu ina asilimia 2 nikamtext mimi nasep tutaonana wakat mwingine.

Nikaweka flight mode nikaenda kuloa na mvua.

Badae natoa flight mode, nakutana na sms nyingi za samahani sana najua sijafanya vizuri, nikamwambia yameisha kuwa na amani



Nikajiuliza maswali huyu dogo kanionaje nimeacha issue zangu mob, kwenda kumpa company asiijisikie mnyonge yeye ananiweka nje napigwa na mvua wakati angeweza kuniachia key ya room yake.

Kama issue ni msosi angeenda mmoja na boda nibaki na mwingie mgeni nisiwe mjonge.

Nikaona hawa watu akili zao finyu sana.

Nimeapa siji rudia tena kujikuta baba huruma
 
mwamba huyu hapa...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…