Kwa hili la huyu mpenzi wangu acha pesa zangu ziishie kwa mama tu!

Lau km nisingekuta umesitisha muamala ningekuona bonge la fala, umefanya la maana saana kusitisha muamala.
 
Iliniumiza sana msichana tumeanza naye mahusiano siku tatu tu akaniambia ana changamoto anahitaji tsh 150,000. Nikamwambia sina yote nina Tsh 100,000 nikamtumia. Hakusema hata amepokea, akanyamaza tu.

Ikabidi nimpigie simu kujua kama amepokea au laah, akapokea simu nikamuuliza "umeona kuna pesa kidogo nimekutumia Tsh. 100,000", akasema "Nimeona." Nikasubiri hata aseme asante hakusema, akaniambia, "Nipo natafuta hiyo 50,000 kwa rafiki zangu waniongezee maana nilitaka tsh 150,000 na nilikuambia hivyo."

Nikasema sawa nisamehe sikuwa nayo yote, akanijibu "Basi baadaye." Nikaingia kwenye menu yangu ya Tigo Pesa nikaomba kuirudisha ile pesa, nashukuru haikuchelewa sana ikarudishwa, nikamshukuru Mungu.

Nikamtumia mama yangu Tsh. 20,000 nikanyamaza. Akapiga simu dk hiyo hiyo akishukuru sana na kunitakia mibaraka mingi mingi, nikamwambia mama hiyo kidogo, akasema hapana hakuna pesa kidogo, akashukuru na kuniombea pale nilipopungua parudishwe.

Basi alivyokata tu simu nikammalizia na ile nyingine 80,000, akanipigia simu tena this time nikamwambia mama naingia kwenye kikao, nashukuru Mungu akubariki.

Niliona angenishukuru sana mpaka nakuwa najisikia vibaya. Siku zote mama yangu yupo hivyo umtumie 10,000 ya voucher umtumie 200,000 ya matumizi shukrani zake zipo pale pale. Nikawaza sana kuwa hawa wanawake wa sasa hivi wanakwama wapi kuwa that much cold?

Yule msichana mpumbavu akanipigia simu kuwa mbona tena ile pesa nimeichukua, nikamwambia niliona ni ndogo sana nimeichukua nimemtumia mama, yeye asubiri nikipata nyingi nitamtumia, nikakata simu.

Mpaka leo hatuna tena mawasiliano, nime-mblock.
Ukiona hivyo huyo demu ni MKALI SANA/ chuma
Hakika ndio wanavyo kuaga hivyo... Tafuta mwanamke sura ya baba yake hakika utakuja nipa mrejesho..
 
Shida ni huyo dada alitakiwa kuwa na shukrani atakama pesa haikutosha lbd next time angepata nyingine angemtumia, unajua nikwel wanaume tumekuwa tukitoa pesa kwa wapenzi wetu kwasababu tunataka kuonyesha tunajali.wazazi wetu wanapata asilimia ndogo sana ya kile walicho wekeza kwetu lkn wapenzi wetu wamekuwa wakipata zaidi hata ya uhalisia wa kipato chetu,kuwa na shukran mwanamke hujui mazingila ya hio pesa inako patikana hujui ukituma text ya kuomba pesa vile tunachukulia halaka na tukikosa tunapambana kweli kwa nguvu kupata hio pesa mladi kuonyesha uwanaume wangu basi kuwa na shukrani

Habari ya kusema genye zako sijui zipeleke kwa mama au sijui mwanamke matunzo kwel tunalitambua tunafanya kama upendo sio genye maana kama ishu ni genye wapo huko mtaani wanajua kwel na kagoli kamoja hajisemeshi kala 50k yake kaenda,tena ukiwa mteja na siku nyingine unapewa ofa

Sisi tunatoa kwa upendo pokeeni kwa upendo na shukrani pia
 
Nipe namba za huyo dem nimtumie hio hela fasta..
IMG_20240317_105105_413.jpg
 
Ati mama yako awe girlfriend wako?
Its not about girlfriend.. its about gratitude you dumb ass..
Wanawake wa aina yenu huwaga ni washenzi washenzi ambao hamtakiwi kuhurumiwa hata kidogo kunapokua na chance
 
F you. Umekuja umekurupuka baada ya kukuta uzi umebadilishwa title na content. Mfyuuuu
 
Iliniumiza sana msichana tumeanza naye mahusiano siku tatu tu akaniambia ana changamoto anahitaji tsh 150,000. Nikamwambia sina yote nina Tsh 100,000 nikamtumia. Hakusema hata amepokea, akanyamaza tu.

Ikabidi nimpigie simu kujua kama amepokea au laah, akapokea simu nikamuuliza "umeona kuna pesa kidogo nimekutumia Tsh. 100,000", akasema "Nimeona." Nikasubiri hata aseme asante hakusema, akaniambia, "Nipo natafuta hiyo 50,000 kwa rafiki zangu waniongezee maana nilitaka tsh 150,000 na nilikuambia hivyo."

Nikasema sawa nisamehe sikuwa nayo yote, akanijibu "Basi baadaye." Nikaingia kwenye menu yangu ya Tigo Pesa nikaomba kuirudisha ile pesa, nashukuru haikuchelewa sana ikarudishwa, nikamshukuru Mungu.

Nikamtumia mama yangu Tsh. 20,000 nikanyamaza. Akapiga simu dk hiyo hiyo akishukuru sana na kunitakia mibaraka mingi mingi, nikamwambia mama hiyo kidogo, akasema hapana hakuna pesa kidogo, akashukuru na kuniombea pale nilipopungua parudishwe.

Basi alivyokata tu simu nikammalizia na ile nyingine 80,000, akanipigia simu tena this time nikamwambia mama naingia kwenye kikao, nashukuru Mungu akubariki.

Niliona angenishukuru sana mpaka nakuwa najisikia vibaya. Siku zote mama yangu yupo hivyo umtumie 10,000 ya voucher umtumie 200,000 ya matumizi shukrani zake zipo pale pale. Nikawaza sana kuwa hawa wanawake wa sasa hivi wanakwama wapi kuwa that much cold?

Yule msichana mpumbavu akanipigia simu kuwa mbona tena ile pesa nimeichukua, nikamwambia niliona ni ndogo sana nimeichukua nimemtumia mama, yeye asubiri nikipata nyingi nitamtumia, nikakata simu.

Mpaka leo hatuna tena mawasiliano, nime-mblock.
Safi kabisa bora tuwape pesa watu walioangaika na sisi sio hawa vipepe
 
Hiki Kizazi cha Vijana waliolelewa na SINGLE MOTHERS ni shida. Enyi kina dada ulizeni kwanza kabla ya kuingia kwenye mahusiano. Kijana wa Kiume aliyelelewa na Single Mother ni kimeo sana, wameanza ooooh kataa Ndoa ili muishi kama mama zao. Mwingine ooooh mama awe girlfriend wangu. Hiii mitoto ni shida tupu
Umeongea kwa hasira sana.
 
Back
Top Bottom