Ninarudia tena, una udhaifu mkubwa kwenye uandishi wako, ni vyema ukafanyia marekebisho eneo hilo. Hasa uwekaji wa koma na nukta.
Naendelea kusisitiza kuwa wazungu wako juu yetu sana, na wana ustaarabu kuliko sisi. Hili kwanza sikuambii ili ukabali au ukatae, lakini ndio ukweli mchungu. Ninaposema wazungu wako juu na wastaarabu kuliko sisi, haimaanishi wako perfect bali wanatuzidi kwenye eneo hili. Na wao kuwa wastaarabu kipimo chake ni kwa ujumla wake, ila kama ni suala la mtu mmoja mmoja hilo ni suala jingine. Ni kweli kuna wazungu baadhi sio wastaarabu na wanaweza kuwa washenzi, lakini hilo halizuii wao kuwa wastaarabu kwa umoja wao. Siafiki mzungu kuniita nyani maana hiyo ni dharau, lakini ww kama wewe, umekutana na wazungu wangapi wakakuita nyani? Mimi sijawahi kuitwa nyani na mzungu yoyote.
Kuhusu polisi kuua huko kwao na kupewa dhamana, hilo ni kwa mujibu wa sheria zao. Je polisi waliomuua Aqwilina walichukuliwa hatua gani kwenye mahakama ipi hapa kwetu? Sihitaji polisi waje na majibu niyatakayo, lakini naweza kupima bila kuacha shaka na aina ya majibu. Sina shaka na hilo nisemalo kuwa polisi wanatumikia siasa chafu. Sio kwamba ninajua mfumo wa CCTV ufanyavyo kazi, bali hiyo ni kazi yangu, hivyo ninajua ninachozungumza.
Ninaposema mimi ni mtu makini, sina chembe ya shaka na hilo. Fananisha uandishi wangu na wako, ili upate tofauti ya haraka haraka kati yangu na yako. Ninaposema umakini ujue ninaweza kutofautisha serikali na nchi. Najua yapi ni matamko dhidi ya nchi, na yapi ni matamko dhidi ya serikali. Unavyoongea inaonekana hujui tofauti ya nchi na serikali. Lakini kupitia mijadala kama hii na sisi watu makini, utajua tofauti ya nchi, na serikali.