Kwa hili la Mbunge kwenda Dubai bila kujua dhumuni la safari, Spika anatakiwa kujiuzulu!

Kwa hili la Mbunge kwenda Dubai bila kujua dhumuni la safari, Spika anatakiwa kujiuzulu!

Kama analolisema huyu Mbunge ni kweli basi Spika wa Bunge jiuzulu tafadhali.

Soma >> Mkataba wa Bandari: Mbunge Aida Khenani akiri kupelekwa Dubai, lakini mpaka wanarudi hakujua walikwenda kufanya nini

Mbunge anasema alisafiri mpaka Dubai hajui anaenda kufanyaje? Kweli Kodi zetu mnazitumia kuwalipa au kulipana pasipo tija kiasi hiki?

Yaani Mbunge anasema alienda Dubai lakini hakuambiwa anaenda kufanyaje mpaka anarudi? Analipwa na Bunge anashangaa kuona analipwa kwa fedha za Dubai? Mbunge anasema alilipwa na TPA, kwa mantiki hiyo tunataka tujue TPA ilipataje fedha za kulipia wabunge?

Hivi wajua kwanini Mwendazake alizuia safari za nje ya nchi? Sasa hapo ndio maana yake jueni

Eeee Mwenyezi Mungu mrehemu Rais wa wanyonge - Ta Magufuli!
Sema tu magufuri dio tena rais wa wanyonge
 
Jamani mi naomba tu kujua hivi hawa waarabu watakua wanalipa sh. Ngapi kwa mwezi na sisi tulikua tunaingiza sh. Ngapi ili tujue tu kama inalipa kama mm nipo nipo tu shule sina hata sielewi
Vado hawana mkataba wa uendesha bandari ndiyo wapo kwenye mazungumzo. Na. TPA.

Malipo ya bandari siyo ya kukisia yana vigezo vyake. Kuwa na amani.
 
KUUZA nchi yetu hatutaki kabisa..Kwanza Mmetukosea sana hivi hata hawa watu mnawatoa wapi??? Yaani mtu mnatoa sijui wapi hana ushawishi wowote hajafanya la maana kwenye jamii tukaona anakuja kuwa Kiongozi ndio hayo sasa mnapelekwa huko hamjui..
Kwani ishauzwa!
Bei gani?
Si wananchi mmempigia kura ama ametokea kusiko julikana?
 
Unalitia sana aibu jina lako ulilolinda miaka mingi .anyway wewe.ni mdini n'a ni mweusi tii unajiita mwarabu
Kams kwa "mdini" umemaanisha Muislam, elewa kuwa nafurahi na najivunia sana Uislam wangu, wewe unajivunia nini?

Kwani kuwa mweusi haramu? Au kuwa Mwarabu haramu?

Uislam unatufundisha mbora kati yetu ni mcha Mungu, siyo rangi yake wala kabila lake wala mali zake.
 
Kuna mtangazaji yuko huko kavaa baibui kabisa, hayo mambo pascal Mayala na njaa zote hawezi kufanya
 
Pale hamna spika, Anna Makinda alishiriki kuuza gesi ya Mtwara, huyu kashiriki kupiga mnada nchi
Gedi si inakwenda tanescobaukuna nyingine inauzwa bila sisi kujuwa?.. Na nchi unayosema ineuzwa, wewe uko wapi sasa hivi?

Hatukuelewi.
 
Hapa hakuna kurembua nchi inaharibiwa na Rais. ndo mnenepeshaji wa rushwa nchini. Huyu angekuwa bold kuhusu hili la rushwa wote wangefata ikiwemo mihimiri .huyo wa huo mhimiri mwingine ndo kabisa Hana idea
 
Na Bado yataibuka mengi tu. Mbona wabunge hawajifunzi?! Kuna watu serikalini wapo Kwa ajili ya wizi ufisadi na kutumbuwa hela za mlipa kodi kama hawana akili timamu!
Raia hatuwezi kusema na kudai eti EHH MWENYEZI MUNGU TUSAIDIE!
Raia tuiulize serikali kupitia vyombo vya habari. JE MNAONA MNAWATENDEA HAKI RAIA?!
 
Chadema wameanza kampeni za kuwagawa Watanzania kuelekea 2025.

qenyekiti wao akiwa Sweden kwenye tamasha la kishetani la ngono, anaebidhanuhusu hilo atazame tarehe alizokuwa Sweden na awaambie alikwenda kufanya nini? Alianza kwa makusudi kabisa kuzusha la Zanzibari na Utanganyika.

. Mimu nbauhakija wameshawatanya wale vijana wao wa. Mitabdao waisambaze chuki kula kwenye fursa.

Uongo ukisemwa sana huonekana kuws ukweli.
Waelewe kuwa tutakula nao sahani moja

Hawa nchi ikiwa naamani, kama ilivyo sasa hawana turufu. Maana hawana uongo wa. Kuzuwa.
 
Yaani Mbunge anasema alienda Dubai lakini hakuambiwa anaenda kufanyaje mpaka anarudi? Analipwa na Bunge anashangaa kuona analipwa kwa fedha za Dubai? Mbunge anasema alilipwa na TPA, kwa mantiki hiyo tunataka tujue TPA ilipataje fedha za kulipia wabunge?
Vipi kuhusu ile rushwa waliyogawiwa wabunge kwenye hiyo safari amesemaje? Alipokea au aliikataa?
 
Kama analolisema huyu Mbunge ni kweli basi Spika wa Bunge jiuzulu tafadhali.

Soma >> Mkataba wa Bandari: Mbunge Aida Khenani akiri kupelekwa Dubai, lakini mpaka wanarudi hakujua walikwenda kufanya nini

Mbunge anasema alisafiri mpaka Dubai hajui anaenda kufanyaje? Kweli Kodi zetu mnazitumia kuwalipa au kulipana pasipo tija kiasi hiki?

Yaani Mbunge anasema alienda Dubai lakini hakuambiwa anaenda kufanyaje mpaka anarudi? Analipwa na Bunge anashangaa kuona analipwa kwa fedha za Dubai? Mbunge anasema alilipwa na TPA, kwa mantiki hiyo tunataka tujue TPA ilipataje fedha za kulipia wabunge?

Hivi wajua kwanini Mwendazake alizuia safari za nje ya nchi? Sasa hapo ndio maana yake jueni

Eeee Mwenyezi Mungu mrehemu Rais wa wanyonge - Ta Magufuli!
Huyo mbunge ndiyo anatakiwa afubguliwe mashtaka, kama anakiri kupokea rushwa, basi sheria ya rushwa inamhusu. Aliripoti kwa nani kuwa aluoeqanrushwa? Kwsnininaliipokea?

Apande. Ndege, aende. Mpaka Dubai na wabunge wengine halafu ademe. Alikuwa hajuwi kilichompeleka. Huyo ni pathetic liar.

Tulia usimwache bungeni huyo.
 
Huyo mbunge atakuwa ni poyoyo wa mwisho bungeni. Aondolewe bungeni. Haelewi hata maana ya "study tour".

Utalii wa kujifunza hatakiwi kuambiwa anaenda kufanya nini, anaambiwa tu hii ni study tour. Baada ya hapo ajifunze yeye mwenyewe chochote atachojifunza huko. Sasa kama poyoyo hajajifunza umlaumu Spika?

Wameenda wabunge 30 Dubai, yeye peke yake ndiye hajuwi alienda kufanya nini, hayupo sawa kabisa. Ni poyoyo.

Mama anaupiga mwingi Kimataifa.
Kwanini kalipwa kama alienda study tour, wapi duniani watu waliambiwa unaenda study tour na wasiambiwe wanaenda kusoma nini?
 
Huu ndio wakati sahihi kudai katiba ya wananchi. Ni bora mle ndani kubaki na wabunge 100 wasomi wanaojitambua kuliko kubeba mzigo wa wabunge zaidi ya 300 halafu wote vilaza wasio na manufaa kwa taifa letu la Tanganyika.
Hii katiba unamdai nani!? (Kama yupo)~ Na akupe kwa ajili ya nini!?....hao wananchi ni akina nani!? Na wapo kwa ajili ya akina nani!? Wasomi wa wapi!? Kwa nini wasomi ...!? Kimsingi siamini kuwa mtu kuwa msomi kwa dhana ya msomi wa kusoma na kukariri maandishi na namba, huku akiamini kuwa ndio kupata elimu....huku akisahau maarifa...na pia kushindwa kutambua namna ya kuyatumia hayo "maarifa" (maana hana hayo ndani yake)... tutaendelea kuwa hapa ! Hatuwezi kupata mabadiliko kwa kuendelea kutumia njia zile zile.
 
Huu ndio wakati sahihi kudai katiba ya wananchi. Ni bora mle ndani kubaki na wabunge 100 wasomi wanaojitambua kuliko kubeba mzigo wa wabunge zaidi ya 300 halafu wote vilaza wasio na manufaa kwa taifa letu la Tanganyika.
Ujumbe wako umebeba mambo mawili makuu (nadhani ndio kiini au lengo la kuleta ujumbe); katiba, na wabunge wasomi. Je, unataka kutuambia kuwa, katiba ianishe moja ya sifa ya wabunge ni kuwa wasomi? Na usomi huo uwe wa kiwango gani?
 
Mbunge huyu itakuwa ni Mbumbumbu, aukaficha ukweli.
Haiwezekani kwa mtu mzima , Mbunge ,afunge safari kwa kufuata mkumbo tuu bila ya kujua dhamira ya safari yake?
Huu ni uongo wa kupitiliza .
Kama angelijikuta ankwenda kuliwa uroda kwa Wafalme je angejitetea vipi?
Angevaa bukta ya jeans [emoji158] yenye komeo
 
Mbunge Alitakiwa Kukamatwa Chap Na Kutupwa Ndani Ili Aseme Yote
Alikwendaje Huko Akitumia Kodi Zetu
 
Back
Top Bottom